Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu katika viwanja vya Zakheim Mbagala, TBC Wafukuzwa

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu katika viwanja vya Zakheim Mbagala, TBC Wafukuzwa

Salaam Mkuu,

leo Ijumaa tarehe 28 Agosti 2020 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kinafanya uzinduzi wa kampeni za urais wa Tanzania zinazofanyika, Uwanja wa Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Tundu Lissu ndiye anayepeperusha bendera ya Chadema kwenye nafasi ya urais na Salumu Mwalimu mgombea mwenza.

Kampeni za Uchaguzi Mkuu zilifunguliwa rasmi tarehe 26 Agosti na zitahitimishwa tarehe 27 Oktoba 2020 ambapo kesho yake yaani Jumatano itakuwa ni siku ya uchaguzi. Katika uchauzi huu, Lissu atachuana na wagombea wengine 14 akiwemo Dk. John Magufuli, mgombea wa Chama cha Cha Mapinduzi (CCM), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi).


Nitawaletea Kila kinachojiri.
View attachment 1550719View attachment 1550720View attachment 1550721
Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema bara na Mwalimu, naibu Katibu Mkuu-Zanzibar tayari wamewasili uwanja hapo.

Ulinzi umeimarishwa katika viwanja hivyo, ambapo kuna baadhi ya askari polisi wa kawaida na wale wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU).

Pia, kuna walinzi maalum wa Chadema ambao wanafanya kazi ya kuongoza watu waliofika katika kampeni hizo.

======

UPDATES: 1600HRS

Mkutano Umeanza kwa Kuimba Wimbo wa Taifa na kufuatiwa na Maombi kutoka Madhehbu mbalimbali

TBC wanaingilia kati bora kuangalia face book
 
Wamekata Tena, Lema alianza kuichambua serikali.
Kwikwikwikwi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]nimecheka kweli

Niko Makini sana na TBC kuliko speech za chadema maana najua watakata tu
 
Pwahahaha!!! Mwe mwe mwe yamekuwa hayo.
Si mpo uwanjani, pigeni picha mtupie.

Yaani leo ufunguzi watu hakuna, siku zijazo watu watakuwa hawaji.
watu ni wengi ila TBC wanachakachua. wanatakiwa wachukue aerial view ndiyo itaonyesha uhalisia!
 
Amani iwe kwenu !

Leo chadema wanazindua kAmpeni rasmi pale mbagala, !

Kwa kifupi mapungufu niliyoyaona !

_Kitengo Cha habari hakiko vzr, kuazia mitandaoni mpaka live !

_Mshereheshaji/Mc mlomchagua kapoa Sana ! Hajui kazi Yake vyema
_ratiba zenu hazijakaa sawa !

Ona Sasa mnaumbuka , mtu akishindilia msumari TBC wanatoa live, watangazaji wanaongea uongo na ukweli, tumeona kwa yule mgombea ubunge wa ilala na lema !

Mlishindwa kwenda live stream hata kwa itv kwa Leo tu ? Kama Ni hela Amna mmngechangisha ! Poor kabisa!

Kazi kweli kweli !
 
Jamani mnamuona Lema hapo wakuu? Leo ndio tutajua rangi halisi ya Viongozi wa CHADEMA tutaijua busara iliyo vinywani mwao hapa live bila chenga.
 
Duuuh kweli hakuna nyomi aisee naona Hapo vijana Hadi wanapata Nafasi ya kuchati kwa smartphone bila hata shida kabisaa.

Nafikiri hapa CDM tutajifunza kitu kutoka kwa Watanzania.
Watakuambia wao wamezuiliwa kuja ndo maana mahudhurio kiduchu
 
Naangalia hapa TBC uzinduzi wa kampeni za Chadema. Lakini kitendo cha kukata kata matangazo na wao kuanza kuelezea misimamo yao na kufundisha watazamaji hatukitaki.

Waendelee tuu na CCM yao maana mbona ccm hawakatizi mikutano yao?
 
Back
Top Bottom