Jana mkutano wa CHADEMA ulikuwa na watu kiduchu kwa kuwa Mhe. Kisu alipokuwa anazunguka kutafuta wadhamini alikuwa anafanya kampeni pia. Watu walijitokeza kwa wingi akiwa anatafuta wadhamini kwa kuwa walikuwa wanaenda kumwangalia mtu aliyepigwa na risasi nyingi kuwahi kutokea duniani na akapona.
Jana watu wameona hakuna sababu ya kwenda uwanjani kwa kuwa walishamuona.
Jambo lingine watanzania hawajawahi kuongozwa na Miujiza. Kitendo cha kutoa kwenda jana ni baada ya kuwasikia viongozi wa CHADEMA wakisema Lisu ni Muujiza unaotembea, Watanzania wamekata kuchagua Miujiza wakati binadamu bado wapo.
Ikumbukwe 2015 CHADEMA walijaza watu kwa sababu ya nguvu ya Lowasa na si nguvu ya CHADEMA. Leo CCM wanaenda kuijibu CHADEMA kwa watu kuujaza Uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma.
2020 Watanzania tutachagua Rais, hatuchagui miujiza.