Uchaguzi 2020 Yaliyojiri uzinduzi wa Kampeni za CCM jijini Mwanza - Septemba 7, 2020

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri uzinduzi wa Kampeni za CCM jijini Mwanza - Septemba 7, 2020

Hakika waswahili wanasema kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.

Umejenga SGR Barabara ndege Umezunguka miaka 5 kwenye kampeni nchi nzima.....Bado unajitembeza kuomba Kura.

BILA FIESTA TAMASHA LA DIAMOND KIBA MAROLI YA KUBEBA WATU NK HAJI MTU HAPO
Unateseka sana pole. TZ hatujapata upinzani wa kweli mbadala wa chama tawala. Tunaona ni bora CCM iendelee tu.
 
Nimekutana na basi la Kisire linaelekea vijijini maeneo ya Ilallila, Mwakarundi, Shibula kusoma wananchi mida hii kwenda kujaza uwanja wa Kirumba wakamsikilize jiwe.
 
Ama kweli CCM wameishiwa

Leo ni uzinduzi wa kampeni za CCM mkoa wa Mwanza zinazozinduliwa pale uwanja wa Kirumba.

Kama kawaida yao leo mabasi mengi yameingia vijijini kusomba watu wakaujaze uwanja.

Kubwa kuliko ni hili la kuwaachisha masomo watoto wetu na kuwataka waende uwanja wa CCM Kirumba kujaza uwanja ili ionekane CCM inapendwa.

Yaani CCM mmeishiwa hadi mnalazimisha watoto wa chini ya miaka 18 ambao sio wapiga kura waje kwenye kampeni zenu.

Huu ni wakati wa kuikataa CCM na hila zao, CCM mlikua mnatamba hamna haja ya kufanya kampeni, sasa ili la kusomba Hadi Wanafunzi na kuwaachisha kusoma na kwenda kuwapeleka kwenye kampeni linatoka wapi.

Acheni watoto wetu wasome

Mwanza.JPG
 
Usitupangie.

Kwa msisitizo zaidi.


USITUPANGIE.
 
PM ana sababu gani kuteka, kutesa wapinzani wake apite bila kupigwa!? Kiongozi mkuu, anahubiri ubaguzi maendeleo, rejea eti Bunda hakuna taa, barabara pia ya lami iliishia jimboni kwa Lugola, dharau kwa watumishi, biashara zimedumaa na kufa, huduma za afya umma bora liende huna pesa wewe kufa na maiti utailipia, nani anafuraha na utawala huu!?
 
Na wakubwa sasa hivi wanapitia Jengo la CCM mkoa hapo Makongoro road kugawiwa tisheti za njano.
Mleta habari wangu huko Mwanza nimemtaka apige picha kutuletea ili tu shee na wenzetu hapa JF
 
Lowassa aliamini Elimu bado Sana Tanzania, ni kweli kupitia post yako, elimu bado Sana hapa.

Achilia mbali kwamba inaweza kuwa ulichoona ni kweli, Sasa hapo unathibitishaje kuwa hapo wanaenda uwanjani na si shule?

How can you go to the people in here (JF) with such idiotic presentation.
 
Hakuna kilichonikera kama kuzuia watoto kwenda shule.

Watoto asubuhi hii wanaenda shuleni wanaambiwa hakuna masomo eti kwa sababu ya mkutano wa kampeni wa Maguguli. Tena unaenda unarudishiwa kwenye gate la shule. Wakuu wa shule wanasema, nao wamepewa hiyo taarifa leo asubuhi,

Walimu wote wamelazimishwa kuhudhuria.

Nashindwa kuelewa busara za CCM. Hiki chama inaonekana kinaishi kwa ulaghai. Kwa mtu muungwana, ungependa ujue unaungwa mkono na watu wangapi, na siyo kuwalazimisha watu kuhudhuria mikutano yako. Hii ni dalili kuwa unaweza kulazimisha hata matokeo.

We are really in shithole rule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom