Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo imewapitisha Tundu Antipas Lissu Lazaro Nyalandu na Dr Mayrose Majige kusaka nafasi ya kuwania Urais Tanzania.
Katika kikao chake Cha Kamati Kuu kilichomalizika usiku mnene majina hayo Leo yataletwa ndani ya Baraza Kuu ambao watakata mzizi wa Fitna kumpata mgombea mmoja baada ya kupigiwa kura na jina moja kuwasilisha ndani ya Mkutano Mkuu kesho kuidhinishwa.
Yeyote atakayepitishwa na Baraza Kuu anafaa kuwania Urais Kama vigezo vilivyowekwa na kuchambuliwa na chama hicho.
Stay Tuned.
======
UPDATES:
======
Ratiba ya leo Tarehe 3, Agosti 2020, Baraza Kuu la Chama litakutana katika kikao chake, ambapo litajadili masuala mbalimbali ikiwemo “kufanya mapendekezo ya wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuyawasilisha katika Mkutano Mkuu kwa uamuzi,” inavyoelekezwa kwenye ibara ya 7.7.12(a).
Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.12 (n) Baraza Kuu litajadili rasimu ya Ilani (manifesto) ya Uchaguzi Mkuu na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu kwa maamuzi.
Hotuba ya Freeman Mbowe
Kwa niaba ya chama kama kiongozi mkuu wa chama nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa kukiimarisha chama na kukipigania chama wakati watesi wetu walitegemea mkate tamaa nyinyi mlisimama kukuza thamani ya chetu.
Yawezekana tulikwazika sana na kuumia kuona baadhi yetu tuliokuwa tukiwaamini na kufanya kazi pamoja walipokisaliti chama, na malipo ya dhambi yanaweza kuwa hapahapa na si akhera na wala hatuna sababu ya kujutia.
Chama cha siasa ni watu na tunahitaji chama kinachokua, na ili chama kikue tunahitaji watu wapya kwa niaba ya chama tunatamani ndani ya chama chetu kila mtanzania awe mwana chama wa CHADEMA.
Kutamka kuwa mtu akitoka chama kingine akataliwe hiyo sio sera ya CHADEMA mtu akitoka chama chochote anakaribishwa CHADEMA lakini atambue akifika anawajibu wa kuishi kwa sera na taratibu za chama.
Tunapowakataa wanachama wa chama cha Mapinduzi eti kwa kuwa tunasomo kwa waliotuhama je wakitupa kura zao tutazikataa au tutazikubali.
Tunahitaji kuonesha upendo ndani ya chama chetu na si kuonesha ubaguzi ndani ya chama chetu.
Hatutaki kurudia makosa wanayofanya wenzetu chama cha mapinduzi kutubagua.
Tunahitaji watanzania wote wawe wanachama wa chadema Tunahitaji ushirikiano kukiimarisha chama hiki.
Tufanye nini tofauti zetu za ndani zikiharibu chama hiki hakuna aliebora na hakuna kipindi kibaya cha kukigawa chama kama kipindi cha uchaguzi.
tumepita hatua mbaimbali za kujifunza leo tumefika wakati wa kuwa chama kikuu kwelikweli.
Kazi hiyo na matunda haya ni lazima tuyalinde kwa nguvu zetu kwamba yoyote asitutoe kwenye reli chaguzi zinapita na chama kitabaki na tunawajibika kukiacha salama.
Chama hiki kilikuwa kidogo kweli kweli Mwaka 2010 tukasema mweshemiwa Wilbroad Silaa akiwa katibu wa Chdema alipendekezwa kuwa mgembea wa urais
Hatukumpigia kura Dr Slaa.
Naposema chama hiki kimekuwa ndugu viongozi kwa mara ya kwanza tunakwenda kwenye uchaguzi wa rais na madiwani na tunawagombea 214 katika majimbo yote 214. Halafu anatokea mtu anasema chama hiki kinakufa inabidi tucheke kidogo
Tuliweka mipango kwamba ikifika 2020 Zanzibar tuwe na uwezo angalau wa kusimamisha asilimia 50.
Katika baraza la wawakilishi 112 tunawagombewa asilimia 53 katika bara tuna kata 3659 tunawagombea kata 3920 kuna kata kama 40 tunakamilisha na mpaka kufika mwisho tutasimamisha kata na wabunge asilimia miamoja.
Huko nyuma tuliingia kwenye mazungumzo na vyama vingine. Tusijenge tabia ya kujimwambafai ya kufikiri sisi ni chama kikubwa na ukubwa wetu usitujenge kiburi tumuheshimu kila mtu. Tukiona kuna maslahi mapana kwa chama na nchi tutafanya hivyo. Hatuta ingia kwenye ushirikiano kama fashion.
Na hatutaingia kwenye ushirikiano na watu ambao hawatatuuza njiani. Na sasa tunamazungumzo na chama kimoja ambacho ni ACT. Tunazungumza vilevile kuhusu kuachiana nafasi ya urais kwa visiwa vya zanziabar.
Nimezungumza kwa kifupi nyufa za kiuchaguzi tunafanya kampeni za kuchafuana wenyewe kwa wenyewe.
Tutamaliza mkutano mkuu kesho tutatoka na jina moja la mgombe na tukimaliza wote na wamoja tutoke tumeshikana. Fikiria leo unamkashifu na kumtukana mtu halafu kesho mnataka kunia mamoja
Ni kwa nini tusijifunze kwa chama cha mapinduzi ambacho kimeshindwa kujenga umoja wao kwa makundi ua uchaguzi.
Ni matumaini yangu wagombea wote watatu waliopendekezwa kwenda baraza kuu watania mamoja.
Nguvu yetu ni umoja wetu tutoke hapa na nyuso za furaha tumpate mgombea wetu kwa furaha na sio kujenga mpasuko.
Ni vyema tuwe na akiba kwa hiyo kila mmoja kwenye chama chetu ni wajibu wetu kumpigania na kumpendekeza anaemtaka.
Sisi ni familia Chadema na familia inaimirika wakati wa majaribu na tuioneshe dunia sisi tutaimarika wakati wa majaribu.
Sisi tumeonewa sana tumebezwa sana tumefungwa sana uchaguzi huu tukasema sasa basi.