Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Nimemsikia bwana mbowe na nimekuelewa sana kwenye kipande hicho[emoji116]yani chama kinahitaji Sana watu wapya Hili kikue ila chama akihitaji watu wapya kwenye nafasi ya uwenyekiti taifa ili kikue chama kinamuhitaji Mbowe tu kwenye nafasi hiyo very shame!!
 
alimshinda wapi?

Kwenye mchujo wa watia nia 10 ndani ya CHADEMA na kubaki hawa wa3....

Ndo nauliza, ni vigezo gani vilitumika hata mama huyu akaonekana bora kuliko mtia nia mwenzake Mch. Peter Simon Msigwa?
 
Mbona mnakuwa wambeya!? Uchaguzi ndio unaendelea na upigaji Kura haijaisha, hao Viongozi wakuu wanaporaje Kura!?
 
Akilihutubia Baraza kuu LA Chadema, Mwenyekiti wa Chadema Taifa mhe Kamanda mkuu Freeman Mbowe amesema SASA BASI.

Kuonewa, kuibiwa kura, kushambuliwa, kupigwa risasi nk sasa mambo hayo BASI.

Uchaguzi mkuu 2020 unaelekea kuwa mtamu sana, na kondoo wanaenda kugeuka Nyati na huo muziki wake sio mchezo.
 
Mbona mnakuwa wambeya!? Uchaguzi ndio unaendelea na upigaji Kura haijaisha, hao Viongozi wakuu wanaporaje Kura!?
Kwa nini hamjaruhusu watu wa habari waingie? Au mnaogopa mtapigana makonde ?Upigaji kura ulipoanza naona live online tv hazionyeshi tena.
 
Alichokiongea Mh. Mbowe ndicho nilichohitaji kisemwe mapema ili "sisi" tusioamini katika ushirikiano tujue umuhimu na jinsi ya kushirikiana kwa faida isiyokoma.
 
Akae mstari wa mbele tu, sio kuwatanguliza wasiojitambua.
 
Jamaa kwa kuongea tuu yupo vizuri, tatizo utekelezaji. Atawaweka bavicha mbele yeye haonekani
 
Mhe.Msigwa hakuchukua form ya urais bali alitiania tu

1. Mpaka hatua hii bado wote wapo kwenye hatua ya kutia nia tu ndani ya vyama vyao.

2. Hatua ya awali ilikuwa na watia nia 10 kutaka wapitishwe na chama kuwa wagombea rasmi. Wakachujwa na kubaki "watia nia bora" wa 3 ambao ndiyo hawa walio katika mchujo wa hatua hii.

3. Hakuna mgombea aliyekwisha kuchukua fomu ya kugombea Urais toka NEC mpaka sasa.

CCM wameshamthibitisha tayari mgombea wao aitwaye ndugu John Pombe Magufuli. CHADEMA bila shaka atakuwa Tundu Lissu.

Baada ya hapo kuanzia tarehe 5/8/2020 NEC imefungua dirisha la wagombea kuchukua fomu za uteuzi wa NEC kuwa wagombea rasmi kwa tiketi za vyama vyao.

Sasa sijaelewa unamaanisha nini kusema Msigwa hakuchukua fomu ya uteuzi? Kama ni fomu ya NEC, yes, hakuchukua na hawezi kuchukua mpaka sasa kwa kuwa ni illegible.
 
Nimepita hapo Mlimani city muda huu, hakuna bendera za CDM nje zilipozoeleka kuwekwa. Je wamepigwa mkwara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…