Maneno hayo ameyasema wakati akiomba kura kwa wajumbe wa baraza kuu la Chadema ili aweze kupeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi ya urais.
Amesema uchaguzi wa mwaka huu hautakuwa rahisi kwa kuwa Tume ya uchaguzi haiko huru na vyombo viko upande wa CCM.
Amesema yeye hatamwachia Mungu ila kwa Mungu atapeleka mahesabu tu!
Amesisitiza kuwa yeyote akaye jaribu kuiba uchaguzi atasombwa na kimbunga!
Maneno hayo yanashabihiana na yale aliwahi kuyesema wakati alipokuwa akizungumza na Watanzania waishio Marekani kuwa 'CCM itang'olewa madarakani kwa Tsunami'!
Tuwape tahadhari CCM, uchaguzi huu hamtabebeka kirahisi, jipangeni kutafuta kura halali, mipango ya kutangazwa bila kushinda inaweza isifanikiwe!