Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Unapo pambana na CCM mambo ya Ilani weka pembeni hayatakusaidia bali jikite kuelezea mapambano utapambanaje.
Unapambana na jambazi wewe una unataja vifungu vya sheria ya trespass? CCM ni mfano wa majambazi hayo mambo ya ilani hayana mpango, mbona hata UDP wana ilani!
Basi kama vyama vya upinzani vinashindwa kuweka ilani inayoweza kushawishi wapigakura hawafai kuchukua nafasi ya uongozi
 
Unapo pambana na CCM mambo ya Ilani weka pembeni hayatakusaidia bali jikite kuelezea mapambano utapambanaje.
Unapambana na jambazi wewe una unataja vifungu vya sheria ya trespass? CCM ni mfano wa majambazi hayo mambo ya ilani hayana mpango, mbona hata UDP wana ilani!
Chakaza kunywa divai, umenena vyema.
 
Ushauri wako wako unasukumwa May uoga, unaogopa chama cha kijani kinaenda kupigwa!
Huo siyo ushauri, ujue watu wanapoungana kupambana na mmoja ni kwamba bado hawajatosheleza. Kama ukawa ulishindwa unadhani kuna kipya gani
 
Kati ya makosa makubwa ambayo CHADEMA wanapaswa kuyaepuka kwa gharama yoyote ni kuacha kumpitisha Lissu.

Muda wa majaribio uliisha kipindi cha Lowassa hivyo makosa ya 2015 yasijirudie tena. Mbali na uwezo wa kifedha Nyalandu hana ushawishi wowote ndani ya Chadema ,kwa kifupi hakuna mtu wa kumpa Nyalandu kura.

Naamini Nyalandu yupo kwa ajili ya kumsafishia Jiwe njia apite bila kipingamizi na mwisho wa siku Nyalandu maslahi yake yanalindwa.
 
Mpaka hapo Nyalandu kashinda, Lisu hana uwezo wa kupambana na Nyalandu, Nyalandu ana pesa za kampeni wakati Lisu kapuku hana kitu
Tusingekuwa tunafanya uchaguzi basi miaka yote hiyo. Kwa sababu hatukuwa na pesa za uchaguzi. By the way JPM 2015 alikuwa na pesa za kampeni? Kama Lissu hana pesa za kampeni akipitishwa sisi tuko tayari kumchangia!
 
Kwenye mchujo wa watia nia 10 ndani ya CHADEMA na kubaki hawa wa3....

Ndo nauliza, ni vigezo gani vilitumika hata mama huyu akaonekana bora kuliko mtia nia mwenzake Mch. Peter Simon Msigwa?
msigwa alijitoa
 
Tusingekuwa tunafanya uchaguzi basi miaka yote hiyo. Kwa sababu hatukuwa na pesa za uchaguzi. By the way JPM 2015 alikuwa na pesa za kampeni? Kama Lissu hana pesa za kampeni akipitishwa sisi tuko tayari kumchangia!
Kwani Obama alikuwa na pesa. Those people are crafting for Nyalandu in order to give ccm a downhill task a scheme that will never be allowed to prevail.
 
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo imewapitisha Tundu Antipas Lissu Lazaro Nyalandu na Dr Mayrose Majige kusaka nafasi ya kuwania Urais Tanzania.

Katika kikao chake cha Kamati Kuu kilichomalizika usiku mnene majina hayo Leo yataletwa ndani ya Baraza Kuu ambao watakata mzizi wa Fitna kumpata Mgombea mmoja baada ya kupigiwa kura na jina moja kuwasilisha ndani ya Mkutano Mkuu kesho kuidhinishwa.

Yeyote atakayepitishwa na Baraza Kuu anafaa kuwania Urais Kama vigezo vilivyowekwa na kuchambuliwa na chama hicho.


Stay Tuned.


UPDATES:

======

Ratiba ya leo Tarehe 3, Agosti 2020, Baraza Kuu la Chama litakutana katika kikao chake, ambapo litajadili masuala mbalimbali ikiwemo “kufanya mapendekezo ya wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuyawasilisha katika Mkutano Mkuu kwa uamuzi,” inavyoelekezwa kwenye ibara ya 7.7.12(a).

Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.12 (n) Baraza Kuu litajadili rasimu ya Ilani (manifesto) ya Uchaguzi Mkuu na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu kwa maamuzi.

= > Viongozi Wakuu wa Chadema wameshafika hivyo shughuli rasmi inatarajiwa kuanza hivi punde. Kwa sasa Viongozi hao wapo mbele na Wimbo wa Taifa unaimbwa.

= > Baada ya wimbo wa taifa imefanyika dua kwa ajili ya kufungua Mkutano.

= > Baada ya dua utambulisho wa Kanda mbalimbali zilizohudhuria, Wajumbe wa Bodi ya Udhamini, Wajumbe wa kamati kuu na wageni waalikwa unafanyika.

Katibu Mkuu wa chama John Mnyika akabidhiwa kipaza sauti kwa ajili ya kuongoza mkutano
Nimesimama kufanya kazi mbili tu kwa sasa. Kazi ya kwanza ni kueleza hakiki ya kikao hiki. Baraza kuu letu kwa sasa lina jumla ya Wajumbe 456 wa kikatiba na mpaka nasimama kuzungumza na nyinyi jumla ya Wajumbe 367 sawa na asilimia 80.5wamekwisha ingia kwenye kikao.

La pili ni kueleza kwa muhtasari Ajenda za kikao hiki. Kikao hiki kina jumla ya ajenda saba;

Ajenda za Kikao/ Mkutano:
  • Ufunguzi wa Kikao ambao utafanywa na Mwenyekiti wa Chama
  • Ajenda ya pili ni kuthibitisha ajenda zitakazofuata
  • Ajenda ya tatu ni kujadili rasimu ya ilanio ya Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2020
  • Ajenda ya nne ni kupendekeza majina ya Mgombea wa Urais, Mgombea Mwenza na Mgombea Urais wa Zanzibar
  • Ajenda ya tano ni kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
  • Ajenda ya Sita ni kufanya mapendekezo ya ajenda za kikao kitakachofanyika kesho
  • Ajenda ya saba ni kuhitimisha kikao.

Ufunguzi wa kikao

Freeman Mbowe
Kwa niaba ya chama kama kiongozi mkuu wa chama nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa kukiimarisha chama na kukipigania chama wakati watesi wetu walitegemea mkate tamaa nyinyi mliopo katika ukumbi huu mmesimama kukilinda chama, mmekipigania chama, mmekuza thamani ya Chama chetu.

Na binadamu anasema kila jambo ni mpango wa Mungu. Yawezekana tulikwazika sana tulipoona baadhi yetu tuliowaamini na kufanya kazi pamoja wakikisaliti chama chetu, wakiisaliti dhamira yetu. Natambua ni namna gani tuliumia tulipoona Wabunge wetu wakitukana viongozi, wakikidhalilisha chama hiki. Hatukuwaombea mabaya kwa sababu anayetoa adhabu ni Mwenyezi Mungu. Lakini binadamu tunasema malipo ya dhambi yanaweza kuwa hapahapa na si lazima akhera.

Lakini niwaambie ndugu viongozi, hatuna sababu hata moja ya kusikitika. Waliokata shauri la kuondoka katika chama chetu hatuna sababu ya kujutia, tuna sababu ya kujifunza. Lakini tutambue wakati wote, chama cha siasa ni watu. Ili muweze kuwa chama kinachokua lazima utamaduni wa kuwapata wanachama wapya, viongozi wapya, watu wapya uwe ni utamaduni wa kudumu katika chama cha siasa.

Nasema hili kama kiongozi wa Chadema, kwamba chama hiki tumekijenga na kimefikia hapa kwa kuwa siku zote tumefungua milango. Tumeruhusu watu waje hapa kwa mamia, tumeruhusu watu waje hapa kwa maelfu. Chama hikitumekijenga kuwa chama cha watu na sio kikundi kidogo cha watu kinachojiita Chadema ambacho hakitaki kufungua milango wengine waingie. Tunatamani siku moja kila Mtanzania awe mwanachama wa Chadema.

Nimesikia kauli kutoka kwa viongozi mbalimbali wakitamka kuwa mtu yoyote akitoka Chama cha Mapinduzi asiingie katika chama hiki hiyo sio sera ya CHADEMA mtu akitoka chama chochote anakaribishwa CHADEMA lakini atambue akifika anawajibu wa kuishi kwa mila, desturi, katiba, kanuni na muongozo wa Chadema.

Tunapowakataa wanachama wa chama cha Mapinduzi eti kwa sababu tunasema tunasomo kutoka kwa waliotuhama je wakitupa kura zao tutazikataa au tutazikubali? Tunapoenda kwenye Uchaguzi Wapiganaji wenzangu, tunatamani kura za wote, wa CCM wasio wa vyama vingine, wasio na chama. Haiwezekani tukabaguana, tukawabagua wa vyama vingine halafu kesho tukawashawishi wakatupe kura zao.

Tunahitaji kujenga umoja wa chama wakati huo huo tukijenga umoja wa taifa. Inawezekana tukawachukia sana baadhi ya viongozi wanaofanya maamuzi katika Chama cha Mapinduzi lakini ikaja kama chama hatuwezi kuwachukia wanachama wote wa CCM kama ni maadui zetu.

Tunahitaji kujenga ushawishi wa kisiasa tunahitaji kuonesha upendo huo ndani ya nchi yetu. Tunataka tukiongoza nchi hii tuwe united as a country. Hatuhitaji tuongoze nchi ambayo imepasuka pasuka vipande vya kiitikadi. Tunahitaji umoja wa kitaifa tunahitaji mmoja, tunahitaji wawili tunahitaji Milioni moja.

Ndugu viongozi lazima tuendelee kukilinda chama chetu. Mimi kama kiongozi Mkuu wa Chama wakati wote nafikiria tufanye nini kukiimarisha chama hiki. Tufanye nini migogoro yetu ya ndani isikiumize chama chetu. Kwamba miongoni mwetu hakuna mbora kuliko chama chetu. Umoja wetu ndio nguvu yetu na hakuna kipindi kibaya cha kukigawa chama kama kipindi cha uchaguzi.

Chama hiki kinakuwa hakijawahi kuwa na historia ya kusinyaa. Ukitaka kupima ukuu Chadema leo, usipime propaganda za vyombo vya habari. Pima kwa kuangalia chama hiki kimesambaa mikoa mingapi, wilaya ngapi, majimbo mangapi, wilaya ngapi ndo namna ya kuipima Chadema. Kazi hiyo na matunda haya ni lazima tuyalinde kwa nguvu zetu kwamba yoyote asitutoe kwenye reli chaguzi zinapita na chama kitabaki na tunawajibika kukiacha salama. Matendo yetu ya leo yasitutoe kwenye dhamira hiyo.

Mwaka 2005 Chama hiki kilikuwa kidogo kwelikweli. lakini safari ile ndio ilikwenda kutufanya kuwa chama kikuu cha Upinzani. Kiukubwa tulikuwa chama cha nne. Lakini sisi tulisema tutakijenga chama hiki kwa kupokea yoyote anayetoka katika chama kingine ndio ilikuwa roho ya kuijenga Chadema.

Mwaka 2010 tukasema tufanye utafiti ni nani miongoni mwetu amabye tumtume akabebe bendera ya chama. Kila miaka mitano ya kisiasa ina dynamics zake. Hatulazimiki kutumia mbinu za miaka mitano iliyopita kukabili matakwa ya wakati huo. Tukampitisha Dkt. Wilbroad Silaa akiwa katibu wa Chdema alipendekezwa kuwa mgembea wa urais hatukumpigia kura Dr Slaa. Tulivyofika mwaka 2015 kwa mazingira ya siasa yalivyokuwepo tukakubaliana lile jina moja.

Naposema chama hiki kimekuwa ndugu viongozi kwa mara ya kwanza tunakwenda kwenye historia ya nchi yetu tunakwenda kwenye uchaguzi wa rais na madiwani tukiwa na wagombea katika majimbo yote 214. Halafu anatokea mtu anasema chama hiki kinakufa inabidi tucheke kidogo. Tuliweka mipango kwamba ikifika 2020 Zanzibar tuwe na uwezo angalau wa kusimamisha asilimia 50 ya wagombea wa Ubunge na asilimia 50 ya Wagombea wa udiwani.

Kwahiyo, ndugu viongozi hatukukijenga chama kwa bahati mbaya, tumekijenga kwa confidence na commitment. Tunamaliza mkutano Mkuu kesho tukiwa na mgombea mmoja. Tunahitaji tumalize mkutano mkuu wa kesho wa kesho tukiwa wamoja twende tukapambane tukiimba wimbo mmoja tukitamaliza mkutano mkuu kesho tutatoka na jina moja la mgombe na tukimaliza wote na wamoja tutoke tumeshikana. Fikiria leo unamkashifu na kumtukana mtu halafu kesho mnataka kunia mamoja.

Ni kwa nini tusijifunze kwa chama cha mapinduzi ambacho kimeshindwa kujenga umoja wao kwa makundi ua uchaguzi. Ni matumaini yangu wagombea wote watatu waliopendekezwa kwenda baraza kuu tutafanana katika hili. Natamani katika muda uliobakia tukaitengeneze amani. Tukaitengeneze amani katika chama hiki tusijenge makundi. Nguvu yetu ni umoja wetu tutoke hapa na nyuso za furaha tumpate mgombea wetu kwa furaha na sio kujenga mpasuko.

Ni vyema tuwe na akiba kwa hiyo kila mmoja kwenye chama chetu ni wajibu wetu kumpigania na kumpendekeza anaemtaka. Sisi ni familia ya Chadema na familia inaimirika wakati wa majaribu. Huu ni wakati wetu wa majaribu na tuioneshe dunia sisi tutaimarika zaidi wakati wa majaribu.

Nimalize kwa kuwaambia Viongozi tumeonewa sana tumebezwa sana tumefungwa sana uchaguzi huu tukaseme enough is is enough kwa kiswahili tunasema sasa basi. Nikisema tumeonewa sana sasa sasa baasi.

Nyarandu ajielezea
Asema mimi nilikuwa kipofu nilikuwa sioni ni kama yule kipofu anaelezwa kwenye biblia baadaya kupakwa matope na mzee wa siku akaona tena.

Na mimi nimeguswa tena katika hiki chama naomba mkiona vyema mnipe nafasi ya kusisimama kama mgombea uraisi wa CHADEMA.

Nasema uwezo wa kuiondoa CCM tunao na tupate Urais madiwani na wabunge wa kutosha nipo tayari na nimejiandaa tufanye kampeni kwenye majombo manne kwa siku twende ardhini twende kwa anga na kwa maji.

Turudishe tena tabasamu la wazee wetu tunataka wazanzibar wamiliki tena rasilimali zao za mafuta na gesi na uchumi wa baraza kuu.

Tunataka CHADEMA wasiisome namba tena nao wana CCM wasiisome namba tena na watanzania wasiisome nammba tena, watanzania watamiliki rasmi rasilimali, tutahakikisha tunapunguza madaraka rukuki ya rais, na tutaandika upya katiba ya Tanzania tukianzia na rasimu ya jaji Warioba tutaanzisha benki ya vijana tutaanzisha tena bima ya afya.

Tutashusha kodi, tutaimarisha uchumi wa nchi yetu, tutarekebisha ubora wa elimu kote nchini na tutashirikiana na wanachama wetu tutashusha kodi na kuongeza uzalishaji na kuimarisha ushiriki wa wanawake katika uchumi na uzaishaji kote nchini. Na tutahakikisha CHADEMA inaendelea kukua kutoka utukufu hadi utukufu.

Nilijiunga na CHADEMA 2017 na nikawa kiongozi wa kawaida nikawa mjumbe wa
Kamati tendaji ya Wilaya Singida kasikazini.

Huyu mama bado sana, alivyokuwa anaongea hanusi hata kwa Bulaya wacha Mdee sauti ya zege.
 
Back
Top Bottom