Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

nimeomba matokeo nikapewa naona wameyafuta hata kabla sijampa asante aliyeniletea matokeo. alikuwa ameandika hivinkama sijakosea, Lissu 415, Nyalandu 36, Maryrose 1.

Huyo aliyefuta matokeo aeleze yana matatizo gani!
 
Naona sasa mahakama pekee ndio anaitegemea Jiwe kumkwamisha Lissu. Kama naona vile anatoa maelekezo pale Kisutu, simu zinapigwa kwa wingi kweli
 
Hongereni wajumbe wote CDM na wagombea wote...
Kazi sasa inaanza... hakuna kulala..
Nchi inahitaji mabadiliko makubwa... liwalo na liwe--- NEC heshimuni haki sawa kwa wagombea wote wa vyama vyote. wapeni uwanja sawa..hizi habari za kuwaengua watu kwa technicality ziishie huko huko kwenye coridors zenu... Tanzania ni yetu sote, watoto wa nyumba moja - tupendane na tuijenge nchi yetu kwa kadri ya ushindi wa halali..

Wote CCM na CDM Wamefanya kura za wazi- hakuna namna, tuleteeni njia ya uhesabuji wa kura kama wa CCM na CDM- uwazi na Ukweli- namna bora ya kumuenzi mkapa...
 
Back
Top Bottom