Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC asubuhi ya leo, Mgombea mteule wa urais, nguli wa sheria na mbobezi wa lugha ya kimataifa Tundu Lissu amesema nchi hii kwa miaka mitano wananchi wameendeshwa kama gari bovu kwa kunyimwa mambo yafuatayo:
Mosi,Uhuru wa vyombo vya habari umeminywa ,Hakuna mtu anayeweza kudadisi au kuhoji
Pili,Uchumi wa watu umeporomoka ,watu hawana kitu mifukoni,Wao wanajisifu tumejenga madaraja wakati watu wanahitaji uchumi mifukoni na sio uchumi wa vitu
Tatu ,Viongozi hawajali utu na heshima kwa Raia wanatumia maneno ya kejeli kwa waliowateua
Hawafuati katiba na sheria za nchi,wao ndio wafalme ,amesema hilo haliwezekani
Ametahadharisha kuwa uchaguzi huu utakuwa wa kipekee ,hoja kwa hoja ,Wanaoshindwa kujibu hoja wasitegemee mbeleko ya Tume ya uchaguzi wao hawatakubali
Amesisituza mambo mengi wananchi wa kawaida wameumizwa
Wafanyakazi na wafanyabiashara wameumizwa ,Wakulima nao wanalia
Aidha ametabiri washindwa kwa kujibu hoja wanaweza anza kuanzisha fujo kwani mambo ya kuongea safari hii ni mengi sana na hawana uwezo wa kuyajibu bali watapanic