Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Mlinzi analipwa elf 4 kwa siku na bado anakopwa mwezi ili asikimbie kwa hofu atapoteza mshahara wake anaodai.
Ulipwa siku 40 badala ya mwisho wa Mwezi.
Pana jamaa alikuwa anakanyaga Toka airport dar Hadi kawe lindoni.
Chocho zote za shortcut anazijua
Kampuni nyingi za ulinzi zinalipa tarehe 10 ili ukiach kazi uwe umefanya kazi siku 10 bure
 
Wacha kudanganya watu hapa,unanikumbusha ya Kikwete ujambazi ulipokithiri kipindichake alisema hata Japan ni hivihivi,serikali inawajibu wa kupanga kima cha chini kuanzia let says 20,000 kwa siku hawa watu ni muhimu sana kwenye hivo viwanda usiwadharau ati unskilled worker,hivo virobo hao kina Moh na Huko Mkuranga kama sio wao kiwanda kitaenda??
 
Wabongo wezi sana, kuna sehemu hua wanapaki Malori jamaa wakifika pale ni kufyonza mafuta tu alafu wanauza wizi wizi tu kila kona
 
Fanya kazi acha uvivu
 
Juzi WAnawake walichanga 120M kumchukulia raisi fomu ya kutetea nafasi yake, kumbe Kuna nguvu kazi inapotea viwandani Kwa ujira wa sh.4000/=
Kwani fomu ya urais si shilingi milioni 1 tu wakuu? Na waalimu si walishatoa hela za kununulia fomu?
 
Kuna ushindani mkubwa kwenye biashara wa ndani na kutoka nje ya nchi pia ndio maana mishahara iko hivyo. Ni lazima kudhibiti gharama au kiwanda au biashara itafilisika.
Soko la ajira pia lina ushindani mkubwa ndio maana ajira ni taabu kwa hiyo ukipata mahali jishikishe mpaka utakapi pata pazuri zaidi.
Haya ndio maisha ya mjini au rudi shambani ulime.
 
Mkuu hiv vitu haviend kwa hisia, vinaenda kwa hesabu tena kali sana,
Ukisema kina Mo walipe vibarua 20K per day, means energy drinks za bongo zitauzwa 2k, unga wa ngano unaweza fika hata 3.5k per kg, ili kufidia gharama za kuzalisha,

Unajua nn kitafuata sokoni ? Bidhaa za nje zitaingia kwa kuwa kwao ni cheap kutengeneza, bidhaa za ndani zitakosa soko, viwanda vitakufa, mwisho hata hio 5000 per day hatutapata, unemployment itakuwa juu sana, vijana watajiingiza kwenye magenge ya uhalifu, then boom Tanzania inakuwa kama Haiti

Uchumi hautaki siasa, unahitaji namba
 
Mkuu, serikalin mwalimu mwenye degree analipwa 710k kama kianzio (basic) sawa na 23 hiv kwa siku, hao ea diploma wanalipwa 520k sawa na kama 18 hiv kwa siku,

Halafu wew unasema unskilled labor walipwe 20k per day ?
Vitu vingine vichek vilivyo sio kwa siasa au hisia,

Serikali ipanue tu fursa vijana wajiajiri ila sio kuforce mishahara ya ajabu ya hisia,
Utaua uchumi wote
 
Je mimi nina content mkuu..
Nafanyaje kupata pesa...?
 
Kind of theories

Ku-unlock akili huku huna hat 100 utafanya nini na hip akili uliyo unlock, talking like tuna pretend kujifanya hatujui mtaji hakuna....You need initial money to move, hizo pesa hupati kwa akili yako kuwa unlocked.
Una unlock mind huku una njaa, watoto wamefukuzwa ada shuleni na mwenye nyumba amekutolea vitu nje... Hizi theories haziko general kila context
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…