Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Mlinzi analipwa elf 4 kwa siku na bado anakopwa mwezi ili asikimbie kwa hofu atapoteza mshahara wake anaodai.
Ulipwa siku 40 badala ya mwisho wa Mwezi.
Pana jamaa alikuwa anakanyaga Toka airport dar Hadi kawe lindoni.
Chocho zote za shortcut anazijua
Kampuni nyingi za ulinzi zinalipa tarehe 10 ili ukiach kazi uwe umefanya kazi siku 10 bure
 
Mkuu hio upo dunia nzima, unaposikia Wazungu wanakimbilia china kwa ajiili ya cheap labor ndio kama hao, saizi wanatoka china wanaenda India kwa ajiili ya watu kana hao,
Unskilled labor dunia nzima mishahara yao ni mbuzi tu, mana wanakuwa hawana mikataba, day worker tu,

Kwa kusema hivyo tuhimizane ndugu zangu kusoma sanaa
Wacha kudanganya watu hapa,unanikumbusha ya Kikwete ujambazi ulipokithiri kipindichake alisema hata Japan ni hivihivi,serikali inawajibu wa kupanga kima cha chini kuanzia let says 20,000 kwa siku hawa watu ni muhimu sana kwenye hivo viwanda usiwadharau ati unskilled worker,hivo virobo hao kina Moh na Huko Mkuranga kama sio wao kiwanda kitaenda??
 
Wanalipwa elf 4 kwa siku lakini muhindi mchina akijipindua TU ashapigwa wabongo kwa upigaji hatari.
Pana Moja boksi zinashushwa au pakiwa muhindi anahesabu mara anaitwa au semeshwa TU akigeuka TU boksi tatu nne za chapu chapu zishampita Dili la dereva na wapakiaji.
Kwa elf 4 hio hio mtu aachi kazi mwaka wa kumi na anajenga.
Mswahili humuwezi
Wabongo wezi sana, kuna sehemu hua wanapaki Malori jamaa wakifika pale ni kufyonza mafuta tu alafu wanauza wizi wizi tu kila kona
 
Kuna kiwanda kiko Pale Keko karibu na ukumbi wa DDC nadhani ni cha cello. Malipo kwa siku ni sh. 3500 kwa siku ilikuwa kwa muda mrefu. Sasa ni sh. 4000, kazi masaa 12 yaani lisaa limoja sh. Mia tatu na centi.

Viwanda vingi malipo ni sh. Elfu 5000 kwa siku, hii maana yake lisaa limoja la kazi ni sh. 400. Viwanda vyenye majina makubwa malipo kwa siku ni sh. 7000 hii maana yake lisaa limoja sh mia 6.

Hata kama ni non skilled labor ni haki Mtanzania alipwe sh. Mia 4 kwa lisaa limoja? Ni utumwa wa wazi uliopata baraka za serikali.

Hawa mabilionea wetu akina Bakhressa na Mo huwabebesha Watanzania viroba vya unga wa ngano kwa sh. 50 au pungufu kwa kiroba kimoja. Ni utumwa.

Nimewahi kufanya kazi siku moja tu kwa wahindi Kariakoo ni zaidi ya utumwa , kula juu yangu, nauli juu yangu malipo 7500 kwa siku na kazi very risk. Kazi ya kupeleka mizigo ghorofa ya 12 kutoka chini. Sikurudi tena.
Fanya kazi acha uvivu
 
Juzi WAnawake walichanga 120M kumchukulia raisi fomu ya kutetea nafasi yake, kumbe Kuna nguvu kazi inapotea viwandani Kwa ujira wa sh.4000/=
Kwani fomu ya urais si shilingi milioni 1 tu wakuu? Na waalimu si walishatoa hela za kununulia fomu?
 
Kuna ushindani mkubwa kwenye biashara wa ndani na kutoka nje ya nchi pia ndio maana mishahara iko hivyo. Ni lazima kudhibiti gharama au kiwanda au biashara itafilisika.
Soko la ajira pia lina ushindani mkubwa ndio maana ajira ni taabu kwa hiyo ukipata mahali jishikishe mpaka utakapi pata pazuri zaidi.
Haya ndio maisha ya mjini au rudi shambani ulime.
 
Wacha kudanganya watu hapa,unanikumbusha ya Kikwete ujambazi ulipokithiri kipindichake alisema hata Japan ni hivihivi,serikali inawajibu wa kupanga kima cha chini kuanzia let says 20,000 kwa siku hawa watu ni muhimu sana kwenye hivo viwanda usiwadharau ati unskilled worker,hivo virobo hao kina Moh na Huko Mkuranga kama sio wao kiwanda kitaenda??
Mkuu hiv vitu haviend kwa hisia, vinaenda kwa hesabu tena kali sana,
Ukisema kina Mo walipe vibarua 20K per day, means energy drinks za bongo zitauzwa 2k, unga wa ngano unaweza fika hata 3.5k per kg, ili kufidia gharama za kuzalisha,

Unajua nn kitafuata sokoni ? Bidhaa za nje zitaingia kwa kuwa kwao ni cheap kutengeneza, bidhaa za ndani zitakosa soko, viwanda vitakufa, mwisho hata hio 5000 per day hatutapata, unemployment itakuwa juu sana, vijana watajiingiza kwenye magenge ya uhalifu, then boom Tanzania inakuwa kama Haiti

Uchumi hautaki siasa, unahitaji namba
 
Tutafute namna ya kuwasaidia hawa watu wetu,sio kila mtu anaweza kuwa na hilo shamba,tuishinikize serikali isikubali watu wake wanyannyaswe kiasi hiki,hawa ni nduguzetu na hii ni nchiyao,mbona Zanziber hakuna upuuzi huu??? Day works sio chini ya 20,000.
Mkuu, serikalin mwalimu mwenye degree analipwa 710k kama kianzio (basic) sawa na 23 hiv kwa siku, hao ea diploma wanalipwa 520k sawa na kama 18 hiv kwa siku,

Halafu wew unasema unskilled labor walipwe 20k per day ?
Vitu vingine vichek vilivyo sio kwa siasa au hisia,

Serikali ipanue tu fursa vijana wajiajiri ila sio kuforce mishahara ya ajabu ya hisia,
Utaua uchumi wote
 
dunia haina huruma. unalipwa kwa jinsi unavyojipa thamani.

kwa sasa Tanzania hela ipo kwenye content creation ukiweza kujitoa akili, kina mwijaku wanajenga maghorofa, makonda wa ma bus Tilisho huko wananunua vi IST sababu ya content zinazoleta hela za matangazo. jitoe akili pata ma followers hela itakuja yenyewe
Je mimi nina content mkuu..
Nafanyaje kupata pesa...?
 
Kind of theories

Ku-unlock akili huku huna hat 100 utafanya nini na hip akili uliyo unlock, talking like tuna pretend kujifanya hatujui mtaji hakuna....You need initial money to move, hizo pesa hupati kwa akili yako kuwa unlocked.
Una unlock mind huku una njaa, watoto wamefukuzwa ada shuleni na mwenye nyumba amekutolea vitu nje... Hizi theories haziko general kila context
 
Back
Top Bottom