Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Jumatano, Tarehe 26 Novemba, 2014

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Jumatano, Tarehe 26 Novemba, 2014

Status
Not open for further replies.
wadau nazidi kutetemeka kadri muda unavyoenda, kitaalamu hii inasababishwa na nini? mjuzi anijuze tafadhali

Hahahaaa...bora wewe unatetemeka yani mimi presha iko juu na ninahofia chochote kinaweza tokea hio repot isisomwe.
 
Haya mambo ya mismanagements za nchi ndio yaliwafanya wananchi wa Reunion, kisiwa kimojawapo katika Bahari ya Hindi kupiga kura ya kuacha kuwa chini ya 'wakoloni' hawa wapuuzi na kuamua kurudia kuwa koloni la Mfaransa! Inauma lakini ndio njia pekee ya kupata dignity ya binadamu!
Tungependa efficiency ya mahakama zetu kama kwenye kesi ya PAP lakini sote tunajua ukienda mahakama kuu leo kufungua kesi ujue itaanza kusikilizwa labda Julai mwakani. Kwanza majaji wanaenda likizo Desemba yote na Januari. Watarudi ofisini Februari 2015! Sasa iweje PAP wao wafaili leo, wapangiwe majaji (sio mmoja) watatu leo, wasikilizwe leo, uamuzi utolewe leo! Najua watu watakuja na hadithi za certificate of urgency lakini hiyo speed ni exceptional kabisa. Lkn hatuwezi kuamini kuwa hakuna rushwa maana tumeona majina ya majaji katika listi ya migao ya escrow!
 
Kwa taarifa ya Mwenyekiti Wa Binge IDD Zungu kuwa hawajapata zuio la mahakama na na kuahidikutolea mwongozo jioni ,name kutoonekana kwa sipika Bungen inaashiria mama huyo yupo kufuatilia.
Hapo kunaashiria mchezo ushakwisha, hakuna cha kusomwa hapo walanini. Wananchi tuangalieni njia nyingine mbadala.
 
..mtu yeyote mwenye akili zake anaweza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu haya yanayotokea Tanzania....je tuna accountable detective system?.Je kiongozi mkuu anapata feedback?.Ni kwa vipi unaweza kuniaminisha kuwa Ikulu ilikuwa haijui kuhusu richmond?,kwa vipi unaweza kuniambia ikulu ilikuwa haijui kuhusu EPA?,KWA VIPI UNAWEZA KUNIAMBIA IKULU ILIKUWA HAIJUI KUHUSU ESCROW?...ONENI WENYEWE TATIZO LA MSINGI HAPO

...Nakwambia,hayo yote imewezekana sb tuna corrupt system
 
Zungu kusema hawajapokea taarifa yeyote kuhusu zuio la mahakama ina maana wakipokea kuna uwezekano wa kusitisha mjadala! Katika hili alitakiwa kuwa wazi kuwa bunge alitopangiwa jinsi ya kufanya kazi!

Zungu kusema miongozo yote ya Kuhusu Escrow ataijibu jioni ni wazi kuna uwezekano wa report kutosomwa hata hiyo jioni!
 
ever hili movie la hovyo kabisa sijawahi ona!
Yaani acha tu Linatia hasira sana unaweza chukua tv yako ukaipasua ukadhani umewapasua wao kumbe ni picha tu....yaani wametuvuruga.
 
Last edited by a moderator:
Sijakuelewa unaposema wana mfumo dhaifu kama Somalia, mfumo upi?
 
Jana niliweka uzi hapa nikisisitiza hakuna mjadala utakaoendele bungeni na mpaka sasa naona bado ni dana dana tu ndio zinaendelea kuhusu swala hili.

Waheshimiwa,spika si mtu wa kuaminika na msipokuwa na mkakati wa pamoja bila kujali vyama vyenu,hii ripoti haitawasilishwa ng'oo.

Waheshimiwa,baada ya mwenyekiti wa bunge, mh. Zungu kuahirisha bunge kisanii,mlipaswa kukutana kwa dharura na kuweka mkakati wa pamoja wakati mnasubiri maamuzi ya kiti leo jioni kuhusu kashifa hii ili wakiwapa majibu ya kutoridhisha muwe na uamuzi wa kuchukua.

Mkakati pekee hapa wa kuwasaidia ni kuweka mkakati wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali kwa maana ya waziri mkuu,spika wa bunge na hata raisi wa nchi.

Kaeni mtafakari ni nani kati ya hao ndio kikwazo kisha mumshughulikie ipasavyo kwa kutumia madaraka yenu kama wabunge.

Mkiendelea kuingia bungeni bila kujipanga(kuwa na mkakati wa pamoja),hakika mtaburuzwa na kuishia kuomba miongozi isiyokuwa na tija kwenu na mnaowawakilisha.

Nawasilisha.
Moderator naomba huu uzi usimame peke yake na msiuunganishe kama mlivyofanya.

CC: Invisible

Hii ni vita na kila mtu atimize wajibu wake hata kwa kushauri tu.

Nawaomba muuache ili wabunge wengi wausome.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom