Jana niliweka uzi hapa nikisisitiza hakuna mjadala utakaoendele bungeni na mpaka sasa naona bado ni dana dana tu ndio zinaendelea kuhusu swala hili.
Waheshimiwa,spika si mtu wa kuaminika na msipokuwa na mkakati wa pamoja bila kujali vyama vyenu,hii ripoti haitawasilishwa ng'oo.
Waheshimiwa,baada ya mwenyekiti wa bunge, mh. Zungu kuahirisha bunge kisanii,mlipaswa kukutana kwa dharura na kuweka mkakati wa pamoja wakati mnasubiri maamuzi ya kiti leo jioni kuhusu kashifa hii ili wakiwapa majibu ya kutoridhisha muwe na uamuzi wa kuchukua.
Mkakati pekee hapa wa kuwasaidia ni kuweka mkakati wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali kwa maana ya waziri mkuu,spika wa bunge na hata raisi wa nchi.
Kaeni mtafakari ni nani kati ya hao ndio kikwazo kisha mumshughulikie ipasavyo kwa kutumia madaraka yenu kama wabunge.
Mkiendelea kuingia bungeni bila kujipanga(kuwa na mkakati wa pamoja),hakika mtaburuzwa na kuishia kuomba miongozi isiyokuwa na tija kwenu na mnaowawakilisha.
Nawasilisha.
Moderator naomba huu uzi usimame peke yake na msiuunganishe kama mlivyofanya.
CC:
Invisible
Hii ni vita na kila mtu atimize wajibu wake hata kwa kushauri tu.
Nawaomba muuache ili wabunge wengi wausome.