Uchaguzi 2020 Yanayojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

Uchaguzi 2020 Yanayojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

Huu uchaguzi usichukuliwe poa kabisa, kuna jambo linaenda kutokea naamini kati ya Lissu au Membe mmoja anakabidhiwa funguo.

Kwa nini Membe?

1. Ifahamikee Lissu anaweza kushinda na akishinda ccm hawawezi kumpa nchi watatumia njia ya ku_bypass na ndipo dodo linamdondokea mbobezi Bernard ikiwa na maana siyo threaten kwa ccm.

Na kwa nini asiwe Lissu?
2. Endapo itafahamika kweli kashinda, msimamo wake na nguvu itakayopatikana kutoka kwa Umma pamoja na watu kusimama imara kwa lolote hii ndiyo njia itakayofanya kwa mara ya kwanza shetani aone haibu.
Uchambuzi wangu wa kijasusi unaonesha Lissu anapata kura nyingi kumshinda mpinzani wake. Kumtangaza ndipo itakapokuwa shida kwani kitendo cha yeye kuwa rais mpinzani wake anaweza kuburuzwa ICC jambo ambalo hayupo teyari kwenda mahakamani
 
Mlioko karibu na Lissu, mwambieni achanganye mabaya ya serikali hii na sera zake. Watu wanataka kusikia ubaya wa Magufuli na uzuri wa yale atakayofanya. Atafanya nini katika kilimo, uvuvi, ufugaji, elimu, mikopo elimu ya juu, afya, ajira kwa vijana, kodi nk nk. Tangu amalize kile kifungo onevu anarudia rudia alichokiona Chattle (uwanja wa ndege), uonevu wa Magufuli, toka mkutano hadi mkutano, mwanzo hadi mwisho.

Asiwachoshe wapigakura kwa malalamiko meeeeeeeengi dakika hizi za lala salama. He has to strike a balance between ubaya wa Magufuli na uzuri wake (sera zake). Hii ya kusahau sera siyo nzuri. Aanze na ubaya wa Magufuli na CCM halafu amalizie na kile atakachofanya yeye kama Rais. Siyo Magufuli mwanzo hadi mwisho, mkutano hadi mkutano. Siyo nzuri kwa kampeni zake.
Zikiwa zimesalia siku 7 tu kukamilisha muda wa kampeni , leo tena yule Mgombea wenu Jasiri Tundu Lissu anaendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa yenu , ambapo atamaliza kazi kwenye baadhi ya majimbo ya Kilimanjaro na baadaye kuingia Tanga.

Kama kawaida yetu tutakuwepo hewani tena kuwaletea kinachoendelea kila anapopita.

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za Uhakika.

View attachment 1605808

========
 
Uchambuzi wangu wa kijasusi unaonesha Lissu anapata kura nyingi kumshinda mpinzani wake. Kumtangaza ndipo itakapokuwa shida kwani kitendo cha yeye kuwa rais mpinzani wake anaweza kuburuzwa ICC jambo ambalo hayupo teyari kwenda mahakamani
Atashinda na atatangazwa , japo kwa kuchelewa
 
Wanategemea kucheza na mawakala....kwamba kiapo kipo kesho ila barua ya utambukisho hakuna...ati utaikuta kituoni ...

Pia mchezo wa mawakala kutekwa upo...yaani kama vilevile wakati wa kurudisha form za uteuzi... unapotea asubuhi unaonekana saa tisa mchana umelewa chakali

CDM kuweni makini msiseme hatukiwatonya.
 
Kila kitu kimejulikana , wazalendo ndani ya kundi lao wamevujisha kila kitu
 
Ninachojiuliza ni kwamba, Membe yupo hapo Dar. inamchukua gharama gani kwenda kuwanadi hata wagombea ubunge wa chama chake hapo Dar? Maana nauli ni sh. 400 kutoka anapoishi hadi kwenye mikutano ya kampeni!!!
Umemsikiliza maalim seif leo akiongea na waandishi wa habari?
Kuna mgogoro kati ya ACT na Membe
 
Zikiwa zimesalia siku 7 tu kukamilisha muda wa kampeni , leo tena yule Mgombea wenu Jasiri Tundu Lissu anaendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa yenu , ambapo atamaliza kazi kwenye baadhi ya majimbo ya Kilimanjaro na baadaye kuingia Tanga.

Kama kawaida yetu tutakuwepo hewani tena kuwaletea kinachoendelea kila anapopita.

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za Uhakika.

View attachment 1605808

========
Leo January anapasuka jane lowasa njoo huku
 
Back
Top Bottom