Mcheza kwao hutunzwa.Ndivyo tunavyoweza kuelezea mapokezi ya Tundu Lissu hapo Jana alipokanyaga Ardhi aliyozaliwa.
Leo Mgombea huyo anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda atafanya kampeni zake katika Jimbo la Mkalama na baadaye Singida Mjini.
Tundu Lissu ameandika historia mpya ya Mgombea anayependwa na maarufu zaidi kati ya wagombea wote ingawa hajaweka bango hata moja katika nchi nzima huku mshindani wake wa Karibu akiwa ametapaza mabango kila mahali mpaka kwenye miti ya watu mashambani na vichochoroni.
Katika hali inayochekesha na kushangaza vigenge vya wanaCCM vinavyofadhiliwa na chama hicho vimekuwa vikiandaa tafiti feki za kuonyesha mgombea wao atashinda ili kuhadaa watu na labda kuhalalisha wizi wa kura.
Tunatarajia kuwaletea kila kinachojiri katika kampeni za Leo za mgombea huyu ambaye anaonekana wazi ana kibali duniani na mbinguni
---------- ------------- ---------
Yaliyotokea saa 7 Mchana
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu akizungumza na wananchi wa Iguguno waliosimama barabarani kuzuia msafara wake uliokuwa njiani kuelekea Kata ya Nduguti viwanja vya gulio jimboni Mkalama Mkoa wa Singida.
Mhe. Rais amemnadi Mgombea Ubunge Jimboni hapo Oscar Alex Kapalale.