Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ni Mbowe au Lissu

  • Mbowe

    Votes: 179 14.7%
  • Lissu

    Votes: 1,038 85.3%

  • Total voters
    1,217
  • Poll closed .
Mpaka sasa kwa hapa JF Lissu anaongoza kwa kura zaidi ya asilimia 85 dhidi ya Mbowe mwenye asilimia 13.8.
 
Ikimahanisha kazi anaweza

Kapata 10 leo

Najua wengi wenye Mihemko wafata mikumbo lazima wamebaki mataa leo
Kazi anaweza na wengi tumempa recognition ya heshima kwa kazi yake yote nzuri aliyoifanya.

Ila kwa aina ya mpinzani aliye kutana naye na aina ya siasa ambazo Lissu anazifanya hapo ndio tunapoamua kuchagua mtoa siri dhidi ya mwenye busara.
 
Wakuu,

Leo mbali na kuwa ni Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA pia wanasherekea Miaka 32 ya CHADEMA kupata Usajili wa Kudumu, ambapo ulipatikana Januari 21, 1993.



Mbivu na mbichi kujulikana leo, tumeona mengi na kusikia mengi kila upande ukitetea kwake. Je, nani ataibuka kidedea? Nani atatolewa kimasomaso na wajumbe?

Katika uchaguzi huu wajumbe watachagua Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamu Mwenyekiti kwa Bara na Zanzibar, ambako ushindani mkubwa upo kati ya Mbowe na Lissu kwa nafasi ya Uenyekiti, na Wenje na Heche kwa nafasi ya Umakamu Uenyekiti.


Je, ni Mbowe au Lissu? Ni Heche au Wenje?

Orodha ya Wagombea wote ni;

Mwenyekiti Taifa
  • Freeman Mbowe
  • Odero Odero
  • Tundu Lissu
Makamu Mwenyekiti Bara
  • Ezekia Wenye
  • John Heche
  • Mathayo Gekul
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
  • Hafidh Saleh
  • Said Issa Mohammed
  • Said Mzee Said
  • Suleiman Makame Issa


Wagombea Wanatoa Salamu kwa Wageni Waalikwa na Wapiga Kura

Tundu Lissu


Lissu amshukuru Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe kwa kufanya nae kazi kwa kipindi cha miaka 20, licha ya kutofautiana kimitazamo lakini amekiri hawajawahi kugombana.

"Nimekaa pembeni ya Mwenyekiti wetu wa Chama mfululizo kwa miaka zaidi ya 20 na katika kipindi chote hicho hatajawahi kugombana, hatujawahi kupigana mimi na yeye binafsi. Ndio tumetofautiana kimsimamo lakini hatujawahi kugombani"

Freeman Mbowe

"Hiki chama tunawajibu wote wa kibinadamu na Wakimungu wakukilinda kwa gharama yoyote ile, na chama hiki hatutakiruhusu kwa gharama yoyote eti kwasababu pengine kura za mbowe hazikutosha au kura za Mhe. Lissu hazikutosha ama za Mhe. Odero yule mzee wetu wa kesho kuna mwanga kwamba kura hazijatosha".

"Uchaguzi huu usiwe vita unapashwa kuwa furaha ya ujenzi wa demokrasia"

"Wako watabiri wengi sana wamesema kuhusu uchaguzi wa CHADEMA, Mhe. Mbowe unaenda kukipasua chama, Mhe. Mbowe inakuaje, hawa ni wanademokrasia, wote kama mnavyowaona. Tofauti zetu kwenye mitazamo hii naamini tunakwenda kuizika mwisho wa kikao hiki tunanelea mbele stronger together"

Updates za Matukio
 

Attachments

  • VID-20250121-WA0005.mp4
    5.6 MB
Kazi anaweza na wengi tumempa recognition ya heshima kwa kazi yake yote nzuri aliyoifanya.

Ila kwa aina ya mpinzani alikuwa naye na aina ya siasa ambazo Lissu anazifanya hapo ndio tunapoamua kuchagua mtoa siri dhidi ya mwenye busara.

Haya nyie uamuzi wenu burudani kwa nchi


Akichukua cheo atanyamaza sanaaaaa, ata badilika mtamshangaaaaaa 😉
 
Mbowe muhuni sana, anatengeneza mazingira kuwa wajumbe wamemuelewa baada ya hotuba yake ya leo.
 
Naomba kuuliza, iwapo Lissu ataishind, na Wenje akashinda, itakuaje?
 
Haya nyie uamuzi wenu burudani kwa nchi


Akichukua cheo atanyamaza sanaaaaa, ata badilika mtamshangaaaaaa 😉
Huyo sio Lissu.

Nakupa mfano mmoja hapa uutafakari.

Siku ya mazishi ya Mzee Kibao Mwenyekiti alitoa wito kwa Raisi akitaka ufanyike uchunguzi wa tume ya kijaji kuchunguza mauaji ya Kibao.

Lakini siku mbili baadaye Lissu akiwa airport akitokea Genk alitoa tamko ambalo lilikuwa linapingana na kauli ya Mwenyekiti.

Lissu alisema kwa mahakama hizi ambazo zimekuwa zikitukandamiza, zisizokuwa huru zenye kupokea maagizo ya viongozi wa juu haviwezi kuwa sehemu ya uchunguzi wa matukio haya ya vifo.

Lissu alitoa maoni kuwa yaitwe mashirika ya kimataifa yaje kufanya uchunguzi akitaja na jina kabisa la hilo shirika.

Na kweli kesho yake Chama kikaitisha mkutano mpya wakatoa tamko upya wakifuta tamko la awali kuhusu tume ya kijaji na sasa kwenda na wazo la Lissu.

Hiyo inatoa tafsiri kuwa Lissu ni mtu ambaye yupo mbele zaidi kimawazo na focus yake siku zote ni kufanya siasa ngumu zaidi ambazo zinaweza kuleta mapinduzi katika mazingira haya ya ukandamizaji mkubwa wa Katiba.
 
Naona mwamba anajifanya kuzungumzia umoja baina ya wanachama baada ya uchaguzi.

Huyu Mzee anadhani watu ni wajinga.

Ila siyo mbaya! Maamuzi ni yao wenyewe wana Chadema. Wakiamua kukikuza chama chao ni wao wenyewe na wakiamua kukiuwa chama chao ni wao wenyewe.
Mkuu. Kwa umasikini wa waafrika, kumshinda tajiri ni kazi kubwa sana. Mimi nimejiandaa kisaikolojia. Hatuna chetu.
 
Back
Top Bottom