Yanayotokea Ulaya yana uhusiano gani na Uislamu kama baadhi ya watu wanavyodai hapa JF

Yanayotokea Ulaya yana uhusiano gani na Uislamu kama baadhi ya watu wanavyodai hapa JF

Kwamba kitu usipo kiproof ndio hua hakipo???

It becomes more probabilistic. Kwhy it doesn't mean hakipo but it becomes a believe not a fact example the idea that aliens is exists is a believe not a fact, same to God's existence is more on a believe not facts.
 
Hao wote walijua wamekutana na malaika wa Mungu. Mohamed hakujua na siyo hivyo tu , jibril wa waraq amekuja na ujumbe tofauti na injili na torati .

Unasema Muhammad hakujua kwamba alikuwa amekutana na malaika. Lakini Biblia inaonyesha kwamba hata watu waliokutana na wajumbe wa Mungu waliweza kuogopa, kuchanganyikiwa au kutokuelewa mara moja kilichokuwa kinaendelea.

Kwa mfano:

  1. Luka 1:29–30: Maria alifadhaika na kushindwa kuelewa salamu ya malaika Gabrieli. Malaika akamwambia: “Usiogope, Maria.”
  2. Waamuzi 6:22–23: Gideoni alipotambua kwamba alikuwa amemwona malaika wa Bwana, aliogopa kwamba angekufa. Mungu akamwambia asiogope.
  3. Waamuzi 13:21–22: Manoah na mke wake walitambua baadaye kwamba aliyewatokea alikuwa malaika wa Bwana. Manoah akaogopa sana.
Kwa hiyo, mtu kutotambua mara moja kwamba amekutana na malaika si ushahidi kwamba malaika huyo alikuwa pepo.

Kuhusu madai yako kwamba Jibril alileta ujumbe tofauti na Injili na Torati: ninakuelewa. Lakini kwanza tujiulize, je, Biblia inafundisha kwamba kila ujumbe unaodaiwa kutoka kwa malaika lazima ukubalike bila kuchunguzwa?

Hapana. Wagalatia 1:8 inasema hata kama sisi au malaika kutoka mbinguni akihubiri injili tofauti, ujumbe huo ukataliwe. Hiyo inaonyesha umuhimu wa kuchunguza ujumbe, si kuamua kwamba ni wa kishetani kwa sababu tu umetoka kwa malaika au kwa sababu mtu aliogopa.

Mimi kama Muislamu ninaamini Qur'an ilikuja kuthibitisha asili ya wahyi wa Mungu na kurekebisha yaliyopotoka katika mafundisho yaliyotangulia. Wewe unaweza kutokubaliana na imani hiyo, lakini hoja yako inapaswa kujengwa kwa ushahidi, si kwa hofu ya Muhammad SAW wakati wa ufunuo.
 
Uislamu unavyoiteketeza UFARANSA!!
 
Attachments

  • v26044gc0000dbkc7unog65hj07pbffg.mp4
    7 MB
Hebu kasome Hadith kuhusu Mohamed na experience yake ya Kwanza kule pangoni hira.

Sahih bukhari book 1,volume 1, number 3

Mwanzoni mwa Ufunuo wa Kiungu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani zimshukie) ulikuwa katika mfumo wa ndoto nzuri ambazo zilitimia kama mchana wenye mwanga mkali, kisha upendo wa upweke ukamjaliwa. Alikuwa akienda faraghani katika pango la Hira ambako alikuwa akiabudu (Mwenyezi Mungu pekee) mfululizo kwa siku nyingi kabla ya kutamani kuona familia yake.

Alikuwa anachukua chakula cha safari kwa ajili ya kukaa huko kisha akarudi kwa (mkewe) Khadija ili kuchukua chakula tena vivyo hivyo hadi ghafla Ukweli ukamteremkia alipokuwa katika pango la Hira. Malaika akamjia na kumwambia asome. Mtume akajibu, “Sijui kusoma.” Mtume akaongeza, “Malaika alinikamata (kwa nguvu) na kunibana sana hadi nisiweze kuvumilia tena. Kisha akanifungua na tena akaniambia nisome nami nikajibu, ‘Sijui kusoma.’ Kisha akanikamata tena na kunibana mara ya pili hadi nisiweze kuvumilia tena. Kisha akanifungua na tena akaniambia nisome lakini tena nikajibu, ‘Sijui kusoma (au nisome nini)?’ Kisha akanikamata mara ya tatu na kunibana, kisha akanifungua na akasema, ‘Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba (vyote vilivyopo), ameumba mwanadamu kutokana na donge la damu. Soma! Na Mola wako ni Mwingi wa Ukaramu.’” (96:1, 96:2, 96:3)

Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu akarudi na Ufunuo huo na moyo wake ukipiga sana. Kisha akaenda kwa Khadija binti Khuwailid na kusema, “Nifunike! Nifunike!” Wakamfunika hadi hofu yake ikapita na baada ya hapo akamweleza kila kitu kilichotokea na akasema, “Ninaogopa kuwa kitu kinaweza kunitokea.” Khadija akajibu, “Kamwe! Wallahi, Mwenyezi Mungu hatakuaibisha kamwe. Wewe unahifadhi uhusiano mzuri na jamaa zako, unasaidia maskini na wahitaji, unawahudumia wageni kwa ukarimu na unawasaidia wanaostahili walioathiriwa na majanga.”

Kisha Khadija akamsindikiza kwa binamu yake Waraqa bin Nawfal bin Asad bin ‘Abdul ‘Uzza, ambaye katika kipindi cha Kabla ya Uislamu alikuwa amekubali Ukristo na alikuwa akiandika maandishi kwa herufi za Kiebrania. Alikuwa akiandika kutoka katika Injili kwa Kiebrania kiasi alichotaka Mwenyezi Mungu amwandikie. Alikuwa mzee na alikuwa amepoteza macho yake. Khadija akamwambia Waraqa, “Sikiliza hadithi ya mpwa wako, ewe binamu yangu!” Waraqa akauliza, “Ewe mpwa wangu! Umeona nini?”

Mtume wa Mwenyezi Mungu akamweleza kila alichokiona. Waraqa akasema, “Huyu ndiye yule anayehifadhi siri (malaika Jibril) ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kwa Musa. Laiti ningekuwa kijana na ningeishi hadi wakati ambapo watu wako watakufukuza.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akauliza, “Je, watanifukuza?” Waraqa akathibitisha na akasema, “Yeyote (mtu) aliyekuja na kitu kama hicho ulichokileta alitendewa uadui; na ikiwa nitaendelea kuishi hadi siku utakapofukuzwa basi nitakusaidia kwa nguvu zote.” Lakini baada ya siku chache Waraqa alifariki na Ufunuo wa Kiungu pia ukasimama kwa muda.
Mbona hakuna neno jangwani?
Halafu pia jina Jibril hakulitaja alitaja jina Namus na henda ndio maana wamekuwekea kwenye mabano ili uelewe huyo Namus ni nani
 
Hukumu ndo iwe adhabu ya kifo je kwa kutoa adhabu ya kifo.uoni unatengeneza hofu na sio uadilifu
Kuna kisa kimetokea Saudi Arabia kijana wa miaka 28 anasubiri kunyongwa baada ya yeye kudhihakiwa juu ya imani yake ya kihindu na yeye aliporudisha mapigo kwa uslamu amehukumiwa kunyongwa ila walioanzisha dhihaka kwa imani yake wapo huru je haki ipo wapi?
Hapo haki haipo sawa wala haujakosea. Sehemu ya kwanza uislam umekataza kukashifu imani za watu hata kama hatuziamini. Sehemu ya pili haikutumika haki kuhukumu hiyo kesi. Pia naona jambo ni kama limekaa kichuki binafsi maana wahindi hata nchi zingine za kiarabu hunyanyasika kwa kiasi fulani kwasababu India pia hunyanyasa waislam.
 
Wahindi,wachina plus wajapani wote wana mila zao.Kasome shinto,hinduism plus buddism halafu uone kama zinafanana na mila za kiislamu.
Hoja ilikuwa kwanini Mungu awataje wayahudi plus wazungu kisha akawasahau hao hapo juu.

Utagundua yale maneno hakutamka Mungu bali ni mwanadamu coz ukisoma historia ya mwingiliano wa kijamii, kiuchumi, kijeshi plus kisiasa baina ya waarabu,wayahudi plus wazungu ulikuwa wa kiuhasama zaidi.
Subiri umeelewa lakini aya inasema nini?
Hapo **** kigezo maalum ndio maana wametajwa hao waliotajwa
 
Mbona hakuna neno jangwani?
Halafu pia jina Jibril hakulitaja alitaja jina Namus na henda ndio maana wamekuwekea kwenye mabano ili uelewe huyo Namus ni nani
Iwe jangwani au hapo zamani Musa hakuwahi kuonana na namus au jibril. Quran 10:94 Allah anamwambia Mohamed kama ana mashaka na wahi anaopewa (Qur'an) basi akawaulize wakristo na wayahudi.

Wakristo na wayahudi vitabu vyao havisemi kama Musa alikutana na malaka (namus/jibril). Maana yake nini? Quran imetengeneza tukio ambalo halipo kwa wayahudi(uongo).

Kwenye injili malaika Gabriel anasema kwa Mariam kwamba mtoto atakaye zaliwa ataitwa mwana wa Mungu. Jibril wa Mohamed anasema Yesu sio mwana wa Mungu.
 
Wanauliza kwanini Waislam hawakimbilii nchi za “kiislam” bali wanaenda nchi za “kikiristo”

Wanapotaka kutaja nchi za Kiislamu kwa lengo la kusukuma ajenda yao hasi, huwa hawataji nchi za Qatar, Malaysia, Tunisia, Kuwait, Saudi Arabia, UAE (Dubai), Brunei, Maldives, Bahrain, Oman, Morocco, Turkiye, Kazakhstan na Egypt.
Hizi ndizo nchi ambazo Wakristo wao wenyewe huzipanga foleni kwenda kutafuta maisha bora.

Badala yake, wanazitaja zile zilizovurugika na kukumbwa na machafuko waliyoyasabisha wao wenyewe kama Afghanistan, Yemen, Iraq, Syria, Somalia na Libya.

Wanapotaka kuzungumzia nchi za Kikristo, kwa urahisi kabisa hutumia mifano ya Marekani, Ufaransa, Uingereza, Scandinavia, Canada na Hispania.n.k

Lakini pia kwa makusudi kabisa wanazipuuza nchi za Cameroon, Venezuela, Burundi, Haiti, Congo, South Sudan, Cuba, Msumbiji, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Malawi ambazo nazo wameziharibu wenyewe

Watu hawa ni wanafiki.

NB: Congo ina tatizo la ugaidi, na kiongozi wa uasi ni Joseph (jina la baba wa kambo wa “mungu”, mume wa Maria “mama wa mungu”) ni nchi ya Kikristo, jirani hapo ila hawaisemi!
 
Wakristo na wayahudi vitabu vyao havisemi kama Musa alikutana na malaka (namus/jibril). Maana yake nini? Quran imetengeneza tukio ambalo halipo kwa wayahudi(uongo).
Wewe si umesema hayo maneno si alisema mkristo mwenzako sasa inakuwaje unadia Qur’an imetengeneza tukio la uongo🤣🤣🤣

Njia ya muongo ni fupi
 
Kwenye injili malaika Gabriel anasema kwa Mariam kwamba mtoto atakaye zaliwa ataitwa mwana wa Mungu. Jibril wa Mohamed anasema Yesu sio mwana wa Mungu.
Nimekuulizwa maswali mawili madogo kuhusu Taurat na Injil mpaka sasa haujajibu

1.Injil inayotajwa kwenye Qur’an alipewa Isa je hiyo Injili yenu pia alipewa Isa?
2.Taurat inayotajwa kwenye Qur’an haikuandikwa na Musa bali Musa alipewa na Allah je na ya kwenu ipo hivyo?

Jibu hayo maswali usikimbie
 
Hapo haki haipo sawa wala haujakosea. Sehemu ya kwanza uislam umekataza kukashifu imani za watu hata kama hatuziamini. Sehemu ya pili haikutumika haki kuhukumu hiyo kesi. Pia naona jambo ni kama limekaa kichuki binafsi maana wahindi hata nchi zingine za kiarabu hunyanyasika kwa kiasi fulani kwasababu India pia hunyanyasa waislam.
Nimekuelewa na umejibu vema mkuu
 
Ahsante sana.Samahani kama nimekukera kiimani.
Hapana wala hujanikera,mijadala kwenye Uislamu inaruhusiwa lakini yenye staha na kistaarabu

Wewe umekuwa mstaarabu sana,kama kuna lolote karibu sana
 
Unasema Muhammad hakujua kwamba alikuwa amekutana na malaika. Lakini Biblia inaonyesha kwamba hata watu waliokutana na wajumbe wa Mungu waliweza kuogopa, kuchanganyikiwa au kutokuelewa mara moja kilichokuwa kinaendelea.

Kwa mfano:

  1. Luka 1:29–30: Maria alifadhaika na kushindwa kuelewa salamu ya malaika Gabrieli. Malaika akamwambia: “Usiogope, Maria.”
  2. Waamuzi 6:22–23: Gideoni alipotambua kwamba alikuwa amemwona malaika wa Bwana, aliogopa kwamba angekufa. Mungu akamwambia asiogope.
  3. Waamuzi 13:21–22: Manoah na mke wake walitambua baadaye kwamba aliyewatokea alikuwa malaika wa Bwana. Manoah akaogopa sana.
Kwa hiyo, mtu kutotambua mara moja kwamba amekutana na malaika si ushahidi kwamba malaika huyo alikuwa pepo.

Kuhusu madai yako kwamba Jibril alileta ujumbe tofauti na Injili na Torati: ninakuelewa. Lakini kwanza tujiulize, je, Biblia inafundisha kwamba kila ujumbe unaodaiwa kutoka kwa malaika lazima ukubalike bila kuchunguzwa?

Hapana. Wagalatia 1:8 inasema hata kama sisi au malaika kutoka mbinguni akihubiri injili tofauti, ujumbe huo ukataliwe. Hiyo inaonyesha umuhimu wa kuchunguza ujumbe, si kuamua kwamba ni wa kishetani kwa sababu tu umetoka kwa malaika au kwa sababu mtu aliogopa.

Mimi kama Muislamu ninaamini Qur'an ilikuja kuthibitisha asili ya wahyi wa Mungu na kurekebisha yaliyopotoka katika mafundisho yaliyotangulia. Wewe unaweza kutokubaliana na imani hiyo, lakini hoja yako inapaswa kujengwa kwa ushahidi, si kwa hofu ya Muhammad SAW wakati wa ufunuo.
Mkuu Allah azidi kukupa upeo mkubwa wa mambo,tunapata elimu kubwa sana
 
Iwe jangwani au hapo zamani Musa hakuwahi kuonana na namus au jibril. Quran 10:94 Allah anamwambia Mohamed kama ana mashaka na wahi anaopewa (Qur'an) basi akawaulize wakristo na wayahudi.

Wakristo na wayahudi vitabu vyao havisemi kama Musa alikutana na malaka (namus/jibril). Maana yake nini? Quran imetengeneza tukio ambalo halipo kwa wayahudi(uongo).

Kwenye injili malaika Gabriel anasema kwa Mariam kwamba mtoto atakaye zaliwa ataitwa mwana wa Mungu. Jibril wa Mohamed anasema Yesu sio mwana wa Mungu.

Hoja yako kwamba Biblia haisemi Musa alikutana na malaika si sahihi. Hebu tusome Biblia yako:

  1. Kutoka 3:2: Inasema malaika wa Bwana alimtokea Musa katika mwali wa moto ndani ya kijiti kilichokuwa kinawaka.
  2. Matendo 7:30: Stefano anathibitisha kwamba malaika alimtokea Musa jangwani, katika mlima Sinai.
  3. Matendo 7:35: Stefano anasema Musa alitumwa na Mungu kupitia malaika aliyemtokea katika kijiti kilichowaka.
  4. Wagalatia 3:19: Inasema Sheria ilitolewa kupitia malaika.
Kwa hiyo, Biblia yenyewe inathibitisha kwamba Musa alikutana na malaika. Biblia haisemi jina la malaika huyo lilikuwa Jibril, lakini hilo halimaanishi kwamba tukio la malaika kumtokea Musa halikutokea.

Kuhusu Qur'an 10:94, aya hiyo inamwelekeza Muhammad kurejea kwa watu wanaosoma Maandiko yaliyotangulia. Hilo halimaanishi kwamba kila kitu katika Biblia ya sasa lazima kifanane neno kwa neno na Qur'an. Hata Biblia inahimiza kuchunguza mambo: Matendo 17:11 inawasifu Waberoya kwa kuchunguza Maandiko ili kuthibitisha walichofundishwa.

Kuhusu Yesu kuitwa Mwana wa Mungu, ni kweli kwamba katika Luka 1:35, malaika Gabrieli anamwambia Maria kwamba mtoto ataitwa Mwana wa Mungu. Lakini swali ni: je, maneno hayo yanamaanisha Mungu ana mtoto kwa njia ya kimwili, au ni cheo cha kiimani?

Hata Biblia inatumia jina “wana wa Mungu” kwa watu wengine. Kwa mfano, Kutoka 4:22 Israeli anaitwa mwana wa Mungu, na Luka 3:38 Adamu anaitwa mwana wa Mungu.

Kwa hiyo, tusichanganye maana ya cheo cha “Mwana wa Mungu” na madai kwamba Mungu ana mtoto wa kimwili. Uislamu unamheshimu Yesu kama Masihi na nabii, lakini haukubali kwamba yeye ni Mungu au mwana wa Mungu kwa maana ya uungu.

Unaweza kutokubaliana na Qur'an, lakini usiseme Biblia haijataja Musa kukutana na malaika wakati Matendo 7:30–35 inasema wazi hivyo.
 
Na hapo ndipo utagundua watu kama ipyax hawajui hata vitabu vyao vimeandikwa kitu gani ila kazi yao kupotosha tu maandiko ya Uislamu
 
Back
Top Bottom