Yanga ikitwaa Kombe la Shirikisho itapata Tsh. Bilioni 4.7, ikifungwa itapata Tsh. Bilioni 2.3

Ukiachana na zawadi ya UBINGWA, ina maana kwa lugha nyingine timu iliyofika fainali kwa ngazi ya SHIRIKISHO mpaka sasa hivi itakuwa imeshakusanya zaidi ya USD 2.0 MILLION kwa sababu kila hatua waliyokuwa wanavuka walikuwa wanapewa kitita cha pesa.
Si kweli,
Utaratibu ni kwamba, anayeishia ndiyo anabeba kiwango cha pale alipoishia.
 
Kila mnayekutana naye mnataka wachezaji wao, hii ni dalili bado hamjapevuka kwenye mambo haya ya kimataifa.
Yanga sio kama Simba, robo fainali wanajiona ndio mwisho wa mafanikio wanajilinganisha na Giants akina RAJA,WYDAD ALAHLY etc.
Yanga hata kama atafanikiwa kubeba Super Cup itakapo mrarua Mamelodi, bado haitakuwa imeridhika mpaka ichukue kombe la KLABU BINGWA YA DUNIA au kwa kuanzia hata kushiriki tu, so kujiimarisha kwenye usajili matata ni LAZIMA .
 
Huwa ipo hivi - unapofuzu kushiriki michuano ya KLABU BINGWA BARANI AFRIKA KWA NGAZI YA SHIRIKISHO au KLABU BINGWA BARANI AFRIKA huwa kuna kitita cha pesa ambacho timu inayoshiriki hatua ya mtoano huwa inapata.

Hii hatua ya kwanza, huwa wanaita ni pesa za maandalizi na huwa inatolewa kwa kila timu iliyofanikiwa kuingia hatua ya makundi.

Hatua ya pili, timu ikishafuzu hatua ya makundi huwa kuna kitita cha pesa ambacho timu iliyofuzu kucheza hatua inayofuata huwa inapata, yaani kwa lugha nyingine huwa kuna kitita cha pesa ambacho huwa kinatolewa kwa timu iliyofuzu hatua ya robo fainali.

Hatua ya tatu, timu ikishafuzu hatua ya robo fainali huwa kuna kitita cha pesa ambacho timu iliyofuzu kucheza hatua inayofuata huwa inapata, yaani kwa lugha nyingine huwa kuna kitita cha pesa ambacho huwa kinatolewa kwa timu iliyofuzu hatua ya nusu ya fainali.

Hatua ya nne, baada ya nusu fainali huwa kuna fainali ambayo inatoa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili.

Kwenye hatua ya fainali huwa inapatikana zawadi kwa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili, zawadi hizo huwa zinaambatana na pesa taslimu. Lakini pesa ambazo huwa zinatolewa kwenye hatua ya makundi hadi hatua ya nusu fainali huwa ni pesa ambazo zinatumika kwa ajili ya malazi na kujikimu pamoja posho za wachezaji na benchi la ufundi.
 
Viongozi wasitupe moyo tuu eti " timu ya wananchi" timu ikifilia kweli tunaichangia, tunaisapoti kwenye jezi, uwanjani na kamati za ufundi. Sasa timu imetoboa mshiko tugawane wote wenye kadi ndio nitaamini kweli ni timu yetu
 
Ulishaona wapi hiki kitu? Jaribu kufuatilia KOMBE LA AZAM CONFEDERATION CUP, huu ndiyo mfano mzuri wa kulinganisha kuhusu KLABU BINGWA KWA NGAZI YA SHIRIKISHO na KLABU BINGWA BARANI AFRIKA.

Kwa upande wa KOMBE LA AZAM CONFEDERATION CUP kila hatua huwa kuna kitita cha pesa ambacho timu huwa inapokea inapofuzu na kuendelea na hatua nyingine.

Kitita hiki cha pesa huwa kinasaidia kuwalipa wachezaji pamoja na benchi la ufundi na kujikimu wanapokuwa wanashiriki michuano ya AZAM CONFEDERATION CUP. Hali kadhalika kwa michuano ya KLABU BINGWA AFRIKA na KLABU BINGWA KWA NGAZI YA SHIRIKISHO.
 
Hizo hela za nyuma hazihesabiwi unapewa hela pale unapoishia
Ndiyo kitu gani hiki? Wachezaji watakuwa wanakula nini kama hamna pesa za maandalizi?

Posho nani atakuwa anawalipa wachezaji pamoja na benchi la ufundi kama hamna pesa za maandalizi?

Kila hatua kunakuwa na pesa za maandalizi, hii inajumuisha pesa za kujikimu na pesa kwa ajili ya posho ya wachezaji.
 
Si kweli,
Utaratibu ni kwamba, anayeishia ndiyo anabeba kiwango cha pale alipoishia.
Ulishaona wapi hiki kitu? Yaani anayeishia hatua fulani ndiyo anabeba kiwango cha pale alipoishia na yule aliyefuzu hatua inayofuata hapewi kitu chochote..😂😂

Timu zote katika hatua fulani huwa zinapata kitita cha pesa kwa ajili ya malazi na kujikimu pamoja na posho za wachezaji na benchi la ufundi.
 
Basi sawa. Wewe ndiyo uko sahihi. Kila hatua hizo timu zinapofikia, CAF wanatoa hizo hela ulizosema.
 
Chalesi, amini nilichoandika bro, huo ndiyo utaratibu.
 
Wewe jamaa ni mbishi aisee, halafu unashindwa kuleta uthibitisho wa hoja zako. Haya onesha ni timu ipi ilipewa pesa kwaajili ya maandalizi? Ingekuwa kuna pesa zinatolewa za maandalizi na usafiri, usiongeona timu ya Biashara imeshindwa kusafiri kwenda kurudiana mechi kipindi kile ana shiriki shirikisho. Tusingekuwa tunaombea timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa ziwe zibauwezo wakujimudu kiuchumi. Embu waza vitu kwa kina basi. Pamoja na kukupa evidence bado unakuwa mbishi halafu unashindwa kuleta evidence zako kuthibitisha hoja yako
 
Sio kweli. Kuna timu nyingi zimeshawahi kushindwa kusafiri kwa kukosa pesa. Wangekuwa wanapewa hayo mambo yasingejitokeza
Hizo timu ambazo zilishindwa kusafiri kutokana na kukosa pesa, tatizo huwa ni uongozi. Pesa huwa inatoka kwa mdhamini mkuu, lakini huwa inaliwa na viongozi wa timu na inapelekea timu kupoteza muelekeo.
 
Hizo timu ambazo zilishindwa kusafiri kutokana na kukosa pesa, tatizo huwa ni uongozi. Pesa huwa inatoka kwa mdhamini mkuu, lakini huwa inaliwa na viongozi wa timu na inapelekea timu kupoteza muelekeo
Hakuna kitu kama hicho. Jaribu kujielimisha, usifananishe Azam Confederation na CAF ni vitu havifanani
 
Jaribu kufuatilia michuano ya AZAM CONFEDERATION CUP kwa upande wa TANZANIA. Huo ndiyo mfano mzuri kwa KLABU BINGWA BARANI AFRIKA na KLABU BINGWA KWA NGAZI YA SHIRIKISHO.

Hii michuano mikubwa huwa wanatoa hadi jezi za timu kwa upande wa nyumbani na ugenini, timu husika huwa wanapeleka SAMPLE tu. MPIRA WA MIGUU ni biashara inayolipa sana 🙏🏽
 
Kwahiyo Yanga pamoja na kuwa mshindi wa pili wa CC atamzidi Simba aliyeishia robo fainali CL milioni 200 tu? Uto na mbwembwe zote hizo?
 
Hakuna kitu kama hicho. Jaribu kujielimisha, usifananishe Azam Confederation na CAF ni vitu havifanani
MFUMO WA MALIPO kwa upande wa AZAM CONFEDERATION CUP unafanana na MICHUANO YA CAF. Yaani ni kwamba - AZAM CONFEDERATION CUP wameiga kutoka MICHUANO YA CAF.
 
Kwahiyo Yanga pamoja na kuwa mshindi wa pili wa CC atamzidi Simba aliyeishia robo fainali CL milioni 200 tu? Uto na mbwembwe zote hizo?
Ndiyo! Kwa sababu kila hatua waliyokuwa wanavuka kulikuwa kuna pesa za maandalizi na fainali huwa kuna zawadi ya mshindi wa kwanza ambaye ni BINGWA na mshindi wa pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…