Yanga ilifungwa magoli 19 katika mechi 6 iliposhiriki makundi mara ya mwisho miaka 25 iliyopita

Yanga ilifungwa magoli 19 katika mechi 6 iliposhiriki makundi mara ya mwisho miaka 25 iliyopita

Mimi sijaanzisha uzi wa magoli aliyofungwa Simba, bali uzi wangu unajitegemea, haulinganishiwi na chochote. Uzi unasema Yanga alifungwa magoli 19 katika mechi zote 6 za makundi, na wewe ukitaka anzisha uzi mwingine useme Simba alifungwa magoli 10 katika mechi mbili (tena usitaje matokeo ya mechi nyingine nne, yataharibu uzi maana Simba alivuka kundi hilo hilo alilofungwa magoli 10 akatinga robo fainali)
Hata Yanga alikua robo fainali kumbuka kipindi kile makundi yalikua mawili na hatua inayo fuata ilikua nusu fainali
 
Hayakufika vipi wakati nyumbani na ugenini Raja alifunga 6 na 3, Manning Rangers alifunga 1 na 4, ASEC alifunga 2 na 3. Hebu jumlisha mwenyewe
Hujaelewa. Aliyesema hayakufika magoli 19 ni wewe, na ulikuwa unafananisha magoli 19 waliyofungwa Yanga kwenye mechi 6 na magoli 10 waliyofungwa Simba kwenye mechi 2. Mimi nime-quote hiyo post yako. Soma post namba 7.
 
Hujaelewa. Aliyesema hayakufika magoli 19 ni wewe, na ulikuwa unafananisha magoli 19 waliyofungwa Yanga kwenye mechi 6 na magoli 10 waliyofungwa Simba kwenye mechi 2. Mimi nime-quote hiyo post yako. Soma post namba 7.
Ahaa, kuna jamaa anaitwa redio alitaka kujaribu kubalance story kwa kuleta maudhui mapya 😁
 
Nakumbuka kipindi naanza kupata akili, kipindi team za Tanzania zikishiriki michuano ya CAF, zinapigwa nje ndani!

Kama watoto tukawa tunasema Waarabu hawachezi mpira, wanaweka majini uwanjani badala yao ili wacheze, binadamu ataweza wapi kucheza na majini na kuwafunga!

Kwa utu uzima huu naelewa kuwa ni uwekezaji na uongozi sahihi unaweza kukupata matokeo mazuri uwanjani,

Leo team zacTanzania zinaweza kucheza na Waarabu, ukawa na uhakika wa ushindi.
 
Hio manning rangers ilishafutwa.Haipo duniani.

Timu zilizohai leo kwenye kundi lile ni Asec, Yanga na Raja.

Mechi zile zote zilikuwa live..cha ajabu Leo clips zake hazionekani popote....zilikuwa enzi za kina Lunyamila, Ken Mkapa na marehemu katuba.
 
Kwenye goli 19 kwa mechi 6 ni matokeo ya kawaida katika soka.

Sasa mechi mbili goli 10 ni wastani wa hovyo kuwahi kutokea katika soka yaani ni wastani wa kufungwa 5 kila mechi.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app

Weka table acha kelele. Mtoa mada ameweka table, wewe unaleta maneno. [emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom