Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

Ondoa kwanza dhana ya kuichukulia kama Yanga ipo kwaajili ya Dar bali Yanga ipo kwaajili ya mashabiki wote dunia nzima. Sio watu wote waliopo Dar ni mashabiki wa Yanga hilo ulijue, na Yanga sio kitega uchumi cha watu wa Dar bali Yanga ni timu ya kuwapa burudani mashabiki zake waliopo kila pembe ya dunia. Acha kuwa mbaguzi wa timu, hizo mkoa hata zikipambana kuwa na timu ligi kuu lakini mtaji wao mkubwa ni Simba na Yanga basi. Kule Zanzibar kuna mashabiki wa Yanga wacha na wao wakapelekewe fursa.
Kaka Man U ni timu ya Manchester hata kama ina mashabiki dunia nzima, Liverpool ni timu ya Liverpool, Real Madrid ni ya jiji la Madrid, Barcelona iko pale Catalunya; Al-Ahly iko pale Cairo, watu wa miji hiyo ndiyo starehe yao na uchumi wao; wengine waende huko kama wakitaka kuzishuhudia zikicheza au wazisubiri zikija kucheza mechi zao na timu nyingine kwenye ligi au ngao ya jamii au pre-season. Marketing na kuwasogezea mashabiki wengine timu kunafanyika wakati wa pre-seasons tu.
 
Yanga ni team ya wanachama
Na Zanzibar Kuna wanachama wengi wa Yanga wanaowajibika kulipia ada za uanachama
Kwanini unapambana wasione timu yao
zanzibar na tanganyika wapi kuna wanachama na mashabiki wengi wa Yanga? kumbuka kuwa kuna wanachama na mashabiki wengi ambao walikosa nafasi ya kuiona timu yao kyokana na mechi kuchezwa kwenye uwanja mdogo wa Azam complex, hivyo haikuwa sawa kuwaambia waifuate timu hukoooo.
 
Kaka Man U ni timu ya Manchester hata kama ina mashabiki dunia nzima, Liverpool ni timu ya Liverpool, Real Madrid ni ya jiji la Madrid, Barcelona iko pale Catalunya; Al-Ahly iko pale Cairo, watu wa miji hiyo ndiyo starehe yao na uchumi wao; wengine waende huko kama wakitaka kuzishuhudia zikicheza au wazisubiri zikija kucheza mechi zao na timu nyingine kwenye ligi au ngao ya jamii. Marketing na kuwasogezea mashabiki wengine timu kunafanyika wakati wa pre-seasons tu.
Hujaona Manchester United, Barcelona, Real Madrid zikifanya tour nchi mbalimbali na kucheza friendly matches? Hizo zote ni namna ya kuwafikia mashabiki na kufanya biashara zao. Ingekuwa vyama vyao (FA na UEFA) zinawaruhusu kuamua kuchezea mechi nchi yoyote ya kimashindano basi wangefanya hivyo kwasababu timu mtaji wake ni mashabiki, na mashabiki wapo kila mahali. Ila kwa Africa hilo limeruhusiwa
 
Timu za JKU na UHAMIAJI ni timu za Zanzibar kindaki ndaki kuliko Yanga. Hatukuelezwa kwanini JKU na UHAMIAJI hawakutaka mechi zao za mashindano ya CAF wachezee Zanzibar, lakini Yanga wanataka kwenda kucheza CAF championship mzunguuko wa pili Zanzibar. Kuna nini hasa hapo?

Ufafanuzi unahitajika juu ya jambo hili. Michezo ni furaha, uchumi na undugu, kwanini JKU na UHAMIAJI walihamisha furaha, uchumi na undugu unaotokana na michezo kwenda Egypt na Libya na Yanga kupeleka Zanzibar furaha, uchumi na undugu Zanzibar kutoka dar es salaam?

Je, unawaweza kuwa mkatoliki safi kumzidi Pope?; muislam fafi kuliko mufti?
hauna hoja, ila wapo watakaokuunga mkono.

Maelezo yako yameegemea ubara na Uzanzibari kisha ukristo na uislamu.

Unaweza ona mtoa mada ni mteja mzuri wa vibanda umiza kuliko kuangalia mpira akiwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ngoja nikufundishe, tena kaa kwa kutulia, kuna kipindi uefa walipendekeza baadhi ya mechi za uefa zichezwe nje ya ulaya kwenda kwenye nchi kama vile Marekani na Morocco, tp mazembe walicheza mechi za mashindano yaliyoratibiwa na FIFA hapa Tanzania, na mifano mingine mingi tu ipo.
Mwisho nikuweke sawa kuhusu kuwa na imani thabiti dhidi ya viongozi wa imani husika, kuwa pope/mufti hakumfanyi mtu kuwa bora zaidi kiimani kuliko wengine, imani ya mtu ni siri kati yake na mola wake, unaweza kuwa pope/muft na ukafanya machafu makubwa zaidi kuliko waumini wako.

Kama unaipenda Yanga ifuate unguja.
Umelopoka tu .. hao To mazembe walikuja Tz pasina sababu au kutokizi vigezo?. Ni utahira wa viongozi.
We mbona una nyumba na bado unalipia chumba hotelini au lodge!
 
H

una maarifa, unaweza kuhamisha mechi kwenda mji, nchi au bara lingine kwasababu za kiuchumi na kiusalama TU baaasi. Yanga iliipeleka mechi kule Amani kwa sababu zipi?
Kaulizie vizuri kuhusu hilo.
Utakachojibiwa utaongeza kwenye uelewa wako.
 
Yanga ina mashabiki wengi Zanzibar kuliko hizo JKU na Uhamiaji kwa pamoja.
 
Hujaona Manchester United, Barcelona, Real Madrid zikifanya tour nchi mbalimbali na kucheza friendly matches? Hizo zote ni namna ya kuwafikia mashabiki na kufanya biashara zao. Ingekuwa vyama vyao (FA na UEFA) zinawaruhusu kuamua kuchezea mechi nchi yoyote ya kimashindano basi wangefanya hivyo kwasababu timu mtaji wake ni mashabiki, na mashabiki wapo kila mahali. Ila kwa Africa hilo limeruhusiwa
limeruhusiwa kwaajili ya migogoro ya kivita, mapinduzi, na viwanja vibaya. Yanga inakwenda kuleee kwasababu zipi? Ni kweli timu inafanya mageuzi ya uendeshaji, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba hii timu ni ya kariakoo, mali ya watu wa kariakoo, dar es salaam, ni sehemu ya vitegauchumi vya kariakoo na Dar es Salaam. Mageuzi hayajauondoa ukweli huu. Kwa Yanga kucheza mechi ya kimataifa DSM inaongeza pilikapilika za kariakoo na dar es salaam kibiashara na kijamii. Vyooote hivi mtu anavihamisha bila maelezo ya kina sawa na wale walioikosesha Zanzibar fedha za kigeni kutoka kwa wachezaji na msafara wa timu za Pyramids na Al-ahly Tripoli.
 
hauna hoja, ila wapo watakaokuunga mkono.

Maelezo yako yameegemea ubara na Uzanzibari kisha ukristo na uislamu.

Unaweza ona mtoa mada ni mteja mzuri wa vibanda umiza kuliko kuangalia mpira akiwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ngoja nikufundishe, tena kaa kwa kutulia, kuna kipindi uefa walipendekeza baadhi ya mechi za uefa zichezwe nje ya ulaya kwenda kwenye nchi kama vile Marekani na Morocco, tp mazembe walicheza mechi za mashindano yaliyoratibiwa na FIFA hapa Tanzania, na mifano mingine mingi tu ipo.
Mwisho nikuweke sawa kuhusu kuwa na imani thabiti dhidi ya viongozi wa imani husika, kuwa pope/mufti hakumfanyi mtu kuwa bora zaidi kiimani kuliko wengine, imani ya mtu ni siri kati yake na mola wake, unaweza kuwa pope/muft na ukafanya machafu makubwa zaidi kuliko waumini wako.

Kama unaipenda Yanga ifuate unguja.

We mbona una nyumba na bado unalipia chumba hotelini au lodge!
Takataka kabisa....!!
 
limeruhusiwa kwaajili ya migogoro ya kivita, mapinduzi, na viwanja vibaya. Yanga inakwenda kuleee kwasababu zipi? Ni kweli timu inafanya mageuzi ya uendeshaji, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba hii timu ni ya kariakoo, mali ya watu wa kariakoo, dar es salaam, ni sehemu ya vitegauchumi vya kariakoo na Dar es Salaam. Mageuzi hayajauondoa ukweli huu. Kwa Yanga kucheza mechi ya kimataifa DSM inaongeza pilikapilika za kariakoo na dar es salaam kibiashara na kijamii. Vyooote hivi mtu anavihamisha bila maelezo ya kina sawa na wale walioikosesha Zanzibar fedha za kigeni kutoka kwa wachezaji na msafara wa timu za Pyramids na Al-ahly Tripoli.
Kama ingekuwa imeruhusiwa tu kwasababu ya migogoro ya kivita, na viwanja vibaya pekee basi ungeona CAF wakiwachukulia hatua, au kuwapa onyo au kuomba ufafanuzi kutoka kwa JKU na Uhamiaji kwa kuhama uwanja bila kuwa na migogoro ya kivita wala uwanja kutokuwa mbaya. Lakini umeona likifanyika hilo? Kama halikufanyika hilo basi ujue CAF wameona ni kitu kisichovunja kanuni zao za mashindano.
 
Ni kweli timu inafanya mageuzi ya uendeshaji, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba hii timu ni ya kariakoo, mali ya watu wa kariakoo, dar es salaam, ni sehemu ya vitegauchumi vya kariakoo na Dar es Salaam. Mageuzi hayajauondoa ukweli huu. Kwa Yanga kucheza mechi ya kimataifa DSM inaongeza pilikapilika za kariakoo na dar es salaam kibiashara na kijamii.
Ni timu iliyoko Kariakoo ila ina mashabiki kila pembe. Yanga iliwahi kuamua kucheza mechi yake ya kimataifa dhidi Pyramids kule CCM Kirumba na hakukuwa na kelele za watu wa Dar na kariakoo kukoseshwa vitega uchumi vyao. Kama kungekuwa na uwanja mzuri mfano Arusha, na ikaonekana kuna mashabiki wa kutosha tu huko Arusha basi hata Arusha ingepelekwa huko na hiyo hoja yako ya kariakoo sijui Dar kukosa dili za ela haina maana. Yanga sio timu ya watu wa Dar bali ni ya Tanzania nzima na sasa inafanyika namna ya kuifanya Yanga ipate mashabiki Africa nzima. Acha kuwaza kizamani zamani.
 
nadhaani nadhalia ya per diem inazidi kupata nguvu kwenye hili.
Kama ingekuwa imeruhusiwa tu kwasababu ya migogoro ya kivita, na viwanja vibaya pekee basi ungeona CAF wakiwachukulia hatua, au kuwapa onyo au kuomba ufafanuzi kutoka kwa JKU na Uhamiaji kwa kuhama uwanja bila kuwa na migogoro ya kivita wala uwanja kutokuwa mbaya. Lakini umeona likifanyika hilo? Kama halikufanyika hilo basi ujue CAF wameona ni kitu kisichovunja kanuni zao za mashindano.
Nakubaliana na wewe 100% kuwa CAF haikatazi timu kuhamisha mechi; swali ni kwanini mama yetu aende kupikia chakula chetu kwa jirani; lazima mama awape sababu wanawe kwanini anakwenda kupikia kule. Unachosema wewe ni kwamba mama amekwenda kupikia chakula kule kwasababu hata kule kuna watoto pia. Watoto wangemuuliza mama yao kuwa kwani hao watoto mama yao hayupo? hata kama hayupo mama yao hayupo kwanini wao wasije kula huku kwetu?
 
nadhaani nadhalia ya per diem inazidi kupata nguvu kwenye hili.

Nakubaliana na wewe 100% kuwa CAF haikatazi timu kuhamisha mechi; swali ni kwanini mama yetu aende kupikia chakula chetu kwa jirani; lazima mama awape sababu wanawe kwanini anakwenda kupikia kule. Unachosema wewe ni kwamba mama amekwenda kupikia chakula kule kwasababu hata kule kuna watoto pia. Watoto wangemuuliza mama yao kuwa kwani hao watoto mama yao hayupo? hata kama hayupo mama yao hayupo kwanini wao wasije kula huku kwetu?

Haya twende kwenye mfano ulioleta.
Kumbe akili yako inawaza kuwa Yanga ni timu ya Dar ndio maana muda wote tunapotezeana muda.
Nikuulize maswali kadhaa ili uamshe uelewa wako vizuri
1) Yanga ni timu ya wanachama, je hao wanachama wapo Dar pekee au wapo na mikoani? Kama wapo na mikoani je ni Yanga inawahusu au haiwahusu kwavile Yanga inatokea Dar?
2) kule Zanzibar kuna wanachama wa Yanga ama hakuna? Kama wapo wanachama wa Yanga je hiyo Yanga inawahusu au haiwahusu?
Nimeanza kwa kuzungumzia tu wanachama ila mbali na wanachama kuna washabiki kibao wa Yanga ambao sio wanachama. Mfano mimi ni shabiki wa Yanga ila sio mwanachama.

Hivyo usiseme eti hao watoto mama yao hayupo bali huyo mama ana watoto kila mahali, hivyo anawajibu wa kuamua akapikie wapi kisha wengine wakamfuata ili ale.
 
Ni timu iliyoko Kariakoo ila ina mashabiki kila pembe. Yanga iliwahi kuamua kucheza mechi yake ya kimataifa dhidi Pyramids kule CCM Kirumba na hakukuwa na kelele za watu wa Dar na kariakoo kukoseshwa vitega uchumi vyao. Kama kungekuwa na uwanja mzuri mfano Arusha, na ikaonekana kuna mashabiki wa kutosha tu huko Arusha basi hata Arusha ingepelekwa huko na hiyo hoja yako ya kariakoo sijui Dar kukosa dili za ela haina maana. Yanga sio timu ya watu wa Dar bali ni ya Tanzania nzima na sasa inafanyika namna ya kuifanya Yanga ipate mashabiki Africa nzima. Acha kuwaza kizamani zamani.
Walihamishia CCM Kirumba kwa sababu za kiuchumi (wasukuma wanaingia wengi uwanjani wenyewe kuliko wazaramo) na sababu za kimatokeo (kiwanja kitakachowachosha wapinzani kuliko wangecheza Dar).
 
Haya twende kwenye mfano ulioleta.
Kumbe akili yako inawaza kuwa Yanga ni timu ya Dar ndio maana muda wote tunapotezeana muda.
Nikuulize maswali kadhaa ili uamshe uelewa wako vizuri
1) Yanga ni timu ya wanachama, je hao wanachama wapo Dar pekee au wapo na mikoani? Kama wapo na mikoani je ni Yanga inawahusu au haiwahusu kwavile Yanga inatokea Dar?
2) kule Zanzibar kuna wanachama wa Yanga ama hakuna? Kama wapo wanachama wa Yanga je hiyo Yanga inawahusu au haiwahusu?
Nimeanza kwa kuzungumzia tu wanachama ila mbali na wanachama kuna washabiki kibao wa Yanga ambao sio wanachama. Mfano mimi ni shabiki wa Yanga ila sio mwanachama.

Hivyo usiseme eti hao watoto mama yao hayupo bali huyo mama ana watoto kila mahali, hivyo anawajibu wa kuamua akapikie wapi kisha wengine wakamfuata ili ale.
Yanga ni timu ya Dar es Salaam hiyo haina ubishi, walioko nje ya dar es salaam walitamani mafanikio yake tu. Hata Man u ina mashabiki na wanachama nje ya mji wa Manchester, lakini hao ni wale walifurahishwa na mafanikio yake tu ambao hawaondoi ukweli kwamba Man U ni timu ya Manchester, Uingereza. Man United haiwezi kuhamisha mechi zake kwenda London eti kwakuwa kuna wanachama na wapenzi wake huko pia.
 
mambo mengine tunayakuza. nyie ndio mkizeeka mnakua visirani. mambo madogo hayo. siku wakicheza kwetu arumeru mtasema pia ama kisa kwa wanywa urojo?
 
Yanga ni timu ya Dar es Salaam hiyo haina ubishi, walioko nje ya dar es salaam walitamani mafanikio yake tu. Hata Man u ina mashabiki na wanachama nje ya mji wa Manchester, lakini hao ni wale walifurahishwa na mafanikio yake tu ambao hawaondoi ukweli kwamba Man U ni timu ya Manchester, Uingereza. Man United haiwezi kuhamisha mechi zake kwenda London eti kwakuwa kuna wanachama na wapenzi wake huko pia.
Jibu maswali niliyokuuliza
 
Timu za JKU na UHAMIAJI ni timu za Zanzibar kindaki ndaki kuliko Yanga. Hatukuelezwa kwanini JKU na UHAMIAJI hawakutaka mechi zao za mashindano ya CAF wachezee Zanzibar, lakini Yanga wanataka kwenda kucheza CAF championship mzunguuko wa pili Zanzibar. Kuna nini hasa hapo?

Ufafanuzi unahitajika juu ya jambo hili. Michezo ni furaha, uchumi na undugu, kwanini JKU na UHAMIAJI walihamisha furaha, uchumi na undugu unaotokana na michezo kwenda Egypt na Libya na Yanga kupeleka Zanzibar furaha, uchumi na undugu Zanzibar kutoka dar es salaam?

Je, unawaweza kuwa mkatoliki safi kumzidi Pope?; muislam fafi kuliko mufti?
hizo timu za zanzibar hazikuwa na fedha ndio zikafadhiliws zikacheze misri na libya na mkwanjacwakapewa,hivyo usiwali ganishe na yanga,pia yanga ina wanachama wengi sana zanzibar
 
Back
Top Bottom