Kiweriweri
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 2,150
- 3,086
Alipendezwa na jina lake.Sema injinia hapa kwa Chiko Ushindi alitupiga na kitu kizito sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alipendezwa na jina lake.Sema injinia hapa kwa Chiko Ushindi alitupiga na kitu kizito sana
Hadi kwenye ngao ile, tuliwapiga kimoja tuKama kawaida ya topolos ushindi huwa ni wa mbinde... 1-0, 2-1 wakibahatisha mara moja moja 2-0!!
Leo tarehe 23/04/2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, vinara wa ligi Dar Young Africans almaarufu kama Yanga watashuka dimbani kuikaribisha timu ya Namungo FC kwenye mechi la NBC Premier League
Nitakuwa nawe kukuletea yatakayojiri kwenye uwanja huo, mpira utaanza saa moja kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
=====
00' Kabumbu linaanza hapa dimba la Mkapa
01' Feisal Salum anaachia mkwaju kutoka nje ya 18 na unaenda pembeni kidogo mwa lango
03' Feisal Salum tena, almanusura aandike bao la kwanza
04' Kichuya anaangushwa nje kidogo 18 akielekea lango la Yanga, Molinga anashindwa kuutumia vyema mpira wa adhabu ndogo
09' Yanga wanacheza kwa kasi na kulishambulia lango la Namungo
15' Presha ni kubwa Yanga wanatafuta bao la mapema, Fei Toto amekosa nafasi mbili za wazi
17' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Yanga wanapata bao, Fiston Mayele anafunga baada ya beki kuukosa mpira.
23' Mchezo unaendelea kwa kasi, inaonekana Yanga wanataka kumaliza biashara mapema
25' Namungo nao wanasogea karibu na lango la Yanga, upinzani ni mkali na mchezo umechangamka
30' Yanga wanapata kona, inapigwa lakini haina madhara
31' Kipa wa Namungo yupo chini, inaonekana ana majeraha. Mchezo umesimama anatibiwa.
33' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kichuya anaisawazishia Namungo kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la boksi
Kocha Msaidizi wa Namungo, Julio anaenda kushangilia bao mbele ya mashabiki wa Yanga
37' Mchezo umebalansi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.
38' Kichuya ambaye anaonekana kuwa hatari kwa Yanga anadhibitiwa na walinzi kwa umakini.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
39' Feisal Toto anaipatia Yanga bao la pili akimalizia mpira uliopigwa kwa krosi.
43' Kadi za njano zimekuwa nyingi kwa wachezaji wa Namungo
45' Yanga wanashambulia lakini walinzi wa Namungo wanakuwa makini.
MAPUMZIKO
Kipindi cha pili kimeanza.
46' Yanga wanafika langoni kwa Namungo lakini wanaotea.
50' Kasi ya mchezo imepungua kiasi
55' Mwamuzi anawaonya baadhi ya wachezaji wa Namungo ambao wanacheza faulo mara kadhaa.
60' Yanga wanafanya shambulizi la nguvu lakini wanashindwa kutumia nafasi vizuri.
65' Yanga wanaongeza presha sasa kutafuta bao la tatu, wanafika langoni mara kadhaa lakini wanakosa utulivu
70' Kasi ya Namungo imepungua kiasi na wanaruhusu mashambulizi langoni kwao.
77' Yanga wanaendelea kufanya mashambulizi na kutawala mchezo.
78' Namungo wanarejesha majibu kwa kufika langoni kwa Yanga lakini wanashindwa kutumia nafasi.
85' Namungo wanajaribu kutafuta bao la kusawazisha lakini mambo ni magumu kwao
87' Timu zinashambuliana kwa zamu.
90' Zinaogezwa dakika 3 za nyongeza.
Hadi wewe tunakununua. Tupe bei.Game sold
Namuonea huruma mnyama mpaka basi. Kesho Orlando Pirates wanajitafunia kiulaini! halafu wakirudi Bongo, tunakuja tena kuwamalizia!Zamu yao tarehe 30
Kule bondeni Simba atafuzu kesho, usiogope kuhusu hilo.Kuna watu mioyo na akili zipo Bongo baada ya kuwa South Africa,wanaumia keshenzi na Mayele kama kawaida yake.........
Simba anafuzu kesho na tarehe 30 mnapigwa na kitu kizito utosini.Namuonea huruma mnyama mpaka basi. Kesho Orlando Pirates wanajitafunia kiulaini! halafu wakirudi Bongo, tunakuja tena kuwamalizia!
Tutafidia hizo goli nyingine tarehe 30 ya mwezi huu. Hivyo muanze mapema kujiandaa kisaikojia.Kama kawaida ya topolos ushindi huwa ni wa mbinde... 1-0, 2-1 wakibahatisha mara moja moja 2-0!!
Kesho mnyama anaoga goli za kutoshaNamuonea huruma mnyama mpaka basi. Kesho Orlando Pirates wanajitafunia kiulaini! halafu wakirudi Bongo, tunakuja tena kuwamalizia!
Bocco Ndo Anavo Wadanganya Ivo [emoji23]Simba anafuzu kesho na tarehe 30 mnapigwa na kitu kizito utosini.
😬😬😬 Kesho muda kama huu mtakuwa tayari usingizini na viatu vyenu miguuni.Simba anafuzu kesho na tarehe 30 mnapigwa na kitu kizito utosini.
😂😂😃😂wakomeKuna watu mioyo na akili zipo Bongo baada ya kuwa South Africa,wanaumia keshenzi na Mayele kama kawaida yake.........
Timu walizotegemea zitapunguza gape zote zimepigwa lazima wakose Cha kusemaManeno ya mkosaji.
Mtajua wenyewe na mechi yenu, ila bila shaka mmeinjoy burdaaaaaaniiiiiiii kutoka kwa Mayele.Kule bondeni Simba atafuzu kesho, usiogope kuhusu hilo.
Kilichoipata Mamelodi leo ndicho kitakachoipata Orlando kesho.😬😬😬 Kesho muda kama huu mtakuwa tayari usingizini na viatu vyenu miguuni.
Hata ukiganga wa jadi wa mtaa hufaiUkisimama nchale ukikimbia nchale team ya wazee leo inabondwa kwa mara ya kwanza .
Burudani yake ni kwa ajili yenu sio sisi.Mtajua wenyewe na mechi yenu, ila bila shaka mmeinjoy burdaaaaaaniiiiiiii kutoka kwa Mayele.
Na nyinyi mliotizama mechi ya leo na kuifuatilia hii thread, tar 30 kama kawa Man Mayele anatetema tena.Burudani yake ni kwa ajili yenu sio sisi.