Yanga yahamishia makazi katika Uwanja wa KMC Complex

Yanga yahamishia makazi katika Uwanja wa KMC Complex

Dawa gani ya kusisimua misuli iliyopigwa marufuku,hudungwa dk chache kabla ya mchezo kuanza?
Kwani wazee wa heroine wanaojidunga wanachukua muda gani kupata stimu?

Dawa kuanza ku take effects kwenye mwili wala haihitaji masaa mengi kama unavyofikiri

Lakini pia kumbuka dawa inayoingia kupitia mishipa huwa inaanza kufanya kazi muda mchache kuliko yule aliyetumia vidonge
 
Azam utasema walicheza mpira wa maana siku ile,goli la penalty,yanga walikua pungufu na bado Azam akapaki bus,mechi ya pili watapigwa wachakae
Mechi ya kwanza kwenye ligi msimu uliopita Yanga pia alilala kwa Azam tena wakiwa kamili.Goli lipi la penalty?Hivi mmechanganyikiwa mpaka unadai kwamba Jibril Silla alifunga kwa penalty?
Hii hoja ya kucheza pungufu Simba alishawahi kucheza pungufu akicheza na Yanga baada ya Hassan Banda kuonyeshwa kadi nyekundu.Na Simba akashinda 2-1.
Hivyo kuchezq pungufu isiwe kichaka cha kuficha udhaifu.
Na Tabora United mlicheza pungufu?
 
Kwani wazee wa heroine wanaojidunga wanachukua muda gani kupata stimu?

Dawa kuanza ku take effects kwenye mwili wala haihitaji masaa mengi kama unavyofikiri

Lakini pia kumbuka dawa inayoingia kupitia mishipa huwa inaanza kufanya kazi muda mchache kuliko yule aliyetumia vidonge
Mi nimekuuliza dawa gani mkuu,itaje
 
Mechi ya kwanza kwenye ligi msimu uliopita Yanga pia alilala kwa Azam tena wakiwa kamili.Goli lipi la penalty?Hivi mmechanganyikiwa mpaka unadai kwamba Jibril Silla alifunga kwa penalty?
Hii hoja ya kucheza pungufu Simba alishawahi kucheza pungufu akicheza na Yanga baada ya Hassan Banda kuonyeshwa kadi nyekundu.Na Simba akashinda 2-1.
Hivyo kuchezq pungufu isiwe kichaka cha kuficha udhaifu.
Na Tabora United mlicheza pungufu?
Kwa hiyo kucheza pungufu hakupunguzi nguvu ya timu?
 
Hiyo ni baada ya vipigo viwili mfululizo.

Hapa sasa ndio kuna kitu ambacho uongozi wa Yanga unatuacha njia panda sisi wadau wa soka.

Kama management iliona tatizo la wao kupoteza mechi mbili lilisababishwa na uwanja, kwanini wamuwekee vikao Gamondi usiku wa manane?

Tushike lipi sasa?

Tatizo ni uwanja au ni kocha?

Azizi Ki amekuwa extreme free kwenye kumbi za starehe akila shisha, kitu hatarishi kwa afya ya mchezaji lakini pia hata kwa regular person ambaye duties zake sio soka.

Bado hawalioni hilo kama tatizo wameenda kwenye uwanja?

Kwa research ndogo nikiyofanya kwa mashabiki wa Yanga waliokuwa wanazungumzia sababu za kupoteza kwa mchezo wengi walitaja udhaifu wa safu yao ya ulinzi.

Wengi walitaja kukosekana kwa wachezaji kadhaa ambao ni muhimili wa timu kuwa ndio sababu iliyo wagharimu kupoteza mechi.

Hii ya uwanja kuwa ni sababu sioni kama waliofanya maamuzi walifikiria sahihi au ndio zile emotions baada ya kufungwa.

View attachment 3148007
Nyie mlihama viwanja vingapi? Mmeona maajabu kwa yanga kwenu aaah? Wameamua kuhama ayo ni maamuzi yao usiwapangie kama ambavyo awakuwapangia nyie kuhama!
 
Naupongeza uongozi wa Yanga kwa kuwasikiliza mashabiki na wanachama wanataka nini na kuwapa, klabu hii ni ya wananchi na wananchi hatuutaki uwanja wa Azam hiyo ndo maana ya uongozi bora, Yanga itatisha zaidi kwa mwenendo huu.

Sasa Gamondi aangalie magoli tuliyofungwa ilikuwaje aweze kufix, japo tumeshaongea magoli yote tuliyofungwa yalitokea katikati juu kidogo ya box (uzembe wa viungo kukaba) na ndani ya box ila katikati pia (uzembe wa beki kukaba), hivi timu bora inaruhusuje wapinzani kushoot mipira golini bila bugudha, hii si Yanga tunayoijua, wachezaji wameanza kujisahau kuwa wanakamiwa kila mechi.

Pamoja na taarabu zote za Yanga kufungwa mechi mbili mfululizo , makelele kibao sana ila Yanga bingwa!!
 
Azam wanadai hata mkikimbia mechi ya marudiano itachezwa Chamazi.
Mechi iliyopita Yanga ndio walikuwa wenyeji kwa hiyo mechi ya marudiano Uwanja wa Azam Chamazi.Tabu ipo pale pale.
Kwani Azam tangu awe anacheza mechi zake dhidi ya Yanga pale Chamazi ameshinda mechi ngapi?

Kama hufahamu, Azam ndio mechi yake ya kwanza kuifunga Yanga akiwa katika uwanja wake wa Nyumbani kwaiyo ata wakirudiana pale Azam akifungwa haitakua Ajabu.
 
Kwani Azam tangu awe anacheza mechi zake dhidi ya Yanga pale Chamazi ameshinda mechi ngapi?

Kama hufahamu, Azam ndio mechi yake ya kwanza kuifunga Yanga akiwa katika uwanja wake wa Nyumbani kwaiyo ata wakirudiana pale Azam akifungwa haitakua Ajabu.
Kwani zimechezwa mechi ngapi kati ya timu hizo Chamazi?Usije ukawa unahesabu kisichokuwepo.
 
Utetezi wako umejaa bias nyingi.

Swala.la ushrikina hilo sio mjadala wa kuanza kutumia nguvu kupinga kuwa umeonewa.

Ushirikina ni sehemu ya uendeshaji wa timu yenu kwasababu misingi yenu ipo zaidi kwenye utamaduni wa kiasili.

Bodi ya ligi imewalamba faini kwa michezo hiyo hiyo ya kishirikina sasa kuwatuhumu Azam kuwa wamewafanyia mchezo kuwachafua hiyo haiwezi kukubalika.

Kusema Azam wamewatengenezea script kwa kuonyesha video inayoonesha mabomba ya sindano. Sidhani kama ni hoja ya kweli.

Kwasababu gani nasema hayo.

Ni kwasababu Azam inajua ukubwa wa hiyo tuhuma na uhatari wake endapo ikafikishwa kesi mahakamani na mlalamikaji akawa ni Yanga akidai kuchafuliwa kwa shutuma za uongo.

Kama ni tukio la uongo, Azam angewezaje kuthibitisha mbele ya mahakama kuwa tukio hilo la hayo mabomba ya sindano yanaihusu Yanga?

Maana yake mpaka Azam aliamua kuachia hizo video ni kwamba alikuwa na confidence kuwa upo ushahidi mwingine extra ambao anaweza kuji defend iwapo Yanga ikaamua kumchukulia hatua za kisheria.

Swali ni kwanini Yanga haijasema chochote kuhusiana na shutuma hizo?

Kwanini Yanga haijapeleka malalamiko kwenye ngazi za mahakama ili kumuwajibisha aliyemchafua kwa tuhuma za uongo?
Ndugu mbumbumbu kwanza inaonekana ni mchanga sana katika mambo ya mpira wa miguu ya Nchi hii.
Yanga uwa inapigwa fain kwa kua haipiti kwenye maeneo yaliyo tegwa/mwagwa ushirikina wa timu pinzani kwakua uwa Wana advance part Yao inayo wapa taarifa ya Kila kitu kinachokua kimefanywa kabla ya mchezo kwaiyo uo si ushirikina bali ni kukiuka kanuni za mchezo na ndio maana hujasikia Tff iki iadhibu Yanga kwa taarifa Yao kuhusisha na ushirikina.

Simba ndio timu ambayo kwa miaka isiyo pungua kumi mfululizo imekua ilitajwa na Tff kujihusisha na ushirikina mojakwa Moja, yaani taarifa inaitaja Simba kujihusisha kufanya vitendo vya kishirikina kabla ya mchezo na iyo si apa Nchini tu ata Nje ya mipaka na mara ya mwisho Simba ilipigwa fain na CAF kulipa Dola 10,000/=

Swala la video za kuichafua Yanga lengo lao Azam ni kuchafua Taswira ya Yanga.

Tunasema Azam wamehusika kwakua zile picha na Video zimetoka katika majengo ya Taasisi Yao na hakuna mfanyakazi anaweza ku nyonya video au picha za taasisi na kutupia mitandaoni bila mwajiri wake kuhusuka/kufahamu.

Yanga hawawezi kulipeleka swala Mahakani kwakua hairuhusiwi mambo ya soka kwenda Mahakamani labda wangepeleka Tff kwakua wanazo kamati zifanyazo kazi kama mahakama ila ki uhalisia ni mambo yanayo kosa ushahidi wa Moja kwa Moja na Yalitengenezwa ili kuharibu image ya Yanga kwenye Jamii.

Yanga hawaja Toka hadharani kuishutumu Wala kuishitaki Azam kwakua kwasasa kufanya hivyo itaonekana kama ni kutafuta sababu zisizo na Msingi dhidi ya mechi walizo poteza ila ushahidi wa ki Mazingira inaonyesha hivyo.

Itakua ni kama Wazee wa Simba walivyo kua waki Bwabwaja vitu vya hovyo baada ya Matokeo yasiyo ridhisha na kutengeneza mijadala ya hovyo Nchini.

Yanga wameamua kuchukua maamuzi sahihi ili kuto toa mwanya kwa mjadalauo ku trend na matukio ayo ya kutengenezwa kujitokeza Tena.

Kuhusu ma bomba ya Sindano, kwanza hakuna dawa anayo chomwa mchezaji wakati wa mechi inaendelea iende ika mwongeze Nguvu wakati mechi inaendelea, Kama unaifahamu itaje.
Zile picha kusudi lake lilikua ni kwa Jamii isiyo fahamu namna Sayansi ya Tiba za michezo inavyo Fanya kazi na kuichafua Klabu.

Pili Tff wanayo Doping Test na kanuni za Doping Test unaweza kufanya muda wowote wa mchezo au ata siku yoyote nje ya mchezo kwaiyo watu wa Doping Test walikua wanaweza kwenda Avic Town siku yoyote baada ya vile vipicha mshenzi kutoka na kufanya Doping Test.

Doping Test inachukua Sample ya Damu/Mkojo kwaiyo mchezaji haiwezi hawezi kuondoa vimelea vya Dawa kama uwa anautumia kwakua mtumiaji anakua amesha tumia kwa muda mrefu na zinakua katika mzunguko wa damu yake au mkojo wake na lazima ata fail Test tu.

Narudia Tena Yanga wameamua sahihi kuhama uwanja ili kuondoa propaganda za kipuuzi za kuwaondoa mashabiki mchezoni na tutarudi Azam complex wakati mwingine na kuwa Kanda kama tufanyavyo miaka yote.
 
Azam na 5imba ni Kenge, sanasana Azam, Vilabu vinavyokuja kucheza na Yanga wanawapokea na kuwapa ushirikiano, Ingekuwa jambo la ajabu Yanga kuendelea kuung'ang'ani ule uwanja. Wanaruhusu uwanja utumike kwa propaganda za kuichafua Yanga, mara sindano, mara uchawi nk. KMC hawana ushindani wowote wa nafasi dhidi ya Yanga, tofauti na Azam ambao ni washindani korofi. Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi
Vipi kama timu zingine zitaomba Azam complex uwe uwanja wao wa nyumbani?
 
Sababu ni hii
JamiiForums-789999666.jpg
 
Kila siku ni kuhama tu viwanja! Ni lini timu itamiliki uwanja wake binafsi!! Yaani KMC iliyoanzishwa miaka michache tu iliyopita, inamiliki uwanja wake!! Halafu timu imeanzishwa tangu mwaka 1935! Eti mpaka leo inahemea tu kwenye viwanja vya timu nyingine!!

Kila kiongozi anayeongoza Yanga lazima kwenye kampeni zake aahidi kujenga uwanja! Ila baada ya kupata madaraka, anaanza porojo!!

Hovyo kabisa. ☹️
Ukizingatia KMC wamejenga uwanja kutokana na mapato yanayohusiana na michezo. Miaka michache tu uwanja tayari.
 
Azizi Ki amekuwa extreme free kwenye kumbi za starehe akila shisha, kitu hatarishi kwa afya ya mchezaji lakini pia hata kwa regular person ambaye duties zake sio soka.
Mchezaji siyo mfugo mkuu ana maisha yake binafsi. Fuatilia mkataba wa Neymar utajifunza kitu.
 
Aya ndio mambo Yao lakini sisi uwa tunakua tuna wa zoom tu na kuwa Kanda.
 

Attachments

  • VID-20241110-WA0000.mp4
    2.4 MB
Back
Top Bottom