Yanga yamtaka Fei Toto arudi klabuni haraka na pia klabu ipo tayari kumuuza

Nimesema "Hazijatoa maamuzi kwenye barua aliyoiwasilisha leo kuhusu kuvunja mkataba"

Sijui unaelewa nilichokiandika hapo?
Kama alikua sahihi katika kuvunja mkataba kwa vipengele alivotumia angeenda CAS sasa maana so TFF waliamua bado ni mchezaji wa Yanga
 
Hawaruhusiwi kumvumilia?
Hakuna maswala ya kuvumiliana kwenye ishu ambayo imewekewa muongozo wa hatua gani za kuchukuliwa endapo mchezaji atafikia hatua hiyo
 
Hakuna maswala ya kuvumiliana kwenye ishu ambayo imewekewa muongozo wa hatua gani za kuchukuliwa endapo mchezaji atafikia hatua hiyo
Wao wamechagua kumvumilia. Kwa kufanya hivyo hawakiuki mwongozo wowote ule.
 
Kiukweli we haunaga kitu unajua kwenye mpira we Lete tu zile mada zako za Mzee mpili
 
Kama alikua sahihi katika kuvunja mkataba kwa vipengele alivotumia angeenda CAS sasa maana so TFF waliamua bado ni mchezaji wa Yanga
Hili ni shauri lingine na ili afike huko unakosema wewe ni lazima apitie huku kwanza
 
Kiukweli we haunaga kitu unajua kwenye mpira we Lete tu zile mada zako za Mzee mpili
Nyie bado saaana. Mnasumbuliwa na mchezaji mmoja tena mla urojo! Wanasheria wenu kila siku wako Karume jasho linawatiririka kisa mchezaji mliyeletewa kwenye mfuko wa zawadi.

Je mngekuwa na wachezaji wakubwa kama Chama, Inonga, Kapombe au Phiri, mngeweza kweli kuwasimamia nyie?
 
In short, Fei anawarudisha pale anapopataka, Kuvunja mkataba.
 
Nyie unaowaweza wachezaji mbona wanakimbia bila taarifa?

Manzoki tu kawashinda mkamleta kwenye uchaguzi aje apigw kampeni😂
 
Fei inabidi aadhibiwe vibaya sana kwa utoro... Mbona hili viongozi wangu wa yanga hamlioni.
 
In short, Fei anawarudisha pale anapopataka, Kuvunja mkataba.
Yaani ndiyo hapo hapo. Wana hamu ya kumkomoa, wengine wanapoongelea kumuweka asugue benchi hadi udenda unawatoka.
 
Reactions: Tsh
Kama alikua sahihi katika kuvunja mkataba kwa vipengele alivotumia angeenda CAS sasa maana so TFF waliamua bado ni mchezaji wa Yanga
Fei anachotaka ni kuvunja mkataba. Njia aliyotumia aliambiwa siyo sahihi, sasa kaibadili.....

CAS aende kufanya nn iwapo TFF wameshapokea ombi lake na hawajamalizana?

Ushauri wa kwenda huko unaweza mshauri baada ya TFF kusema huwezi kuvunja mkataba, kaa hapo Yanga cheza mpira.
 
Yaani ndiyo hapo hapo. Wana hamu ya kumkomoa, wengine wanaongelea kumuweka asugue benchi hadi udenda unawatoka.
Na hapa ndipo tatizo lilipo. Wanachokitaka baadhi ya mashabiki ni kukomoa. Nadhani viongozi wanataka pesa.
 
Mshabadilika sasa😂

Si mlidai hajatendewa haki katika kesi Ile na mkatuambia alikua sahihi kuvunja mkataba
 
Kuna kanuni inayotafsiri kwamba kwa kumsamehe kuna sheria iyakua imevunjwa
Kwenye sheria ambayo imeainisha hadi adhabu ya faini pamoja na kufungiwa, ukienda kinyume ni kuvunja sheria
 
Na yanga hawamtaki tena sijui sisi simba tumchukue liwe kombe letu mwaka huu
 
Nyie unaowaweza wachezaji mbona wanakimbia bila taarifa?

Manzoki tu kawashinda mkamleta kwenye uchaguzi aje apigw kampeni😂
Nani kakimbia bila taarifa?

Halafu nikwambie kitu, binafsi sikuwa na mzuka wa kihiiivyo wa Manzoki kuja Simba kwa hiyo hata iliposhindikana niliona fresh tu.
 
Mshabadilika sasa😂

Si mlidai hajatendewa haki katika kesi Ile na mkatuambia alikua sahihi kuvunja mkataba
Mm hata sikuelewi hoja yako haswa ni ipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…