Yanga yamtaka Fei Toto arudi klabuni haraka na pia klabu ipo tayari kumuuza

Si yupo Aziz Ki? Yanga waachane nae tu huyo dogo. Maana hata akirudi hatakuwa na moyo wa kuitumikia klabu
 
Na hapa ndipo tatizo lilipo. Wanachokitaka baadhi ya mashabiki ni kukomoa. Nadhani viongozi wanataka pesa.
Majuto ni mjukuu. Ni kweli wanataka pesa ila wamechelewa kuweka mazingira ya kupata pesa hiyo wanayoitamani.
 
Reactions: Tsh
Feisal ana mikataba mingapi? huo uanaosema ameuvunja ni upi? na aliopeleka barua TFF kuomba uvujwe ni upi?
 
Timu ambayo mchezaji anaweza kuvunja mkataba wake bila shuruti ni Simba na Azam tu.
Simba walimwacha lete Mzungu Dejani alipotaka tu mwenyewe kuvunja mkataba.
Azam walimwacha Sure Boy alipotaka mwenyewe kuvunja mkataba.
Yanga hawajawahi na hawatawahi kumkubalia mchezaji anayetaka mwenyewe kuvunja mkataba.

Yanga ni king'ang'anizi kweli na hawakubali kushindwa.
Fei arudi tu Yanga na kama haitaki ategee mazoezi na mechi hadi wenyewe wamfukuze au hadi mkataba wake uishe.

Yanga ni kinga'ng'anizi haijawahi kutokea.
 
Hizo taka taka ulizo taja hapo kuna hata mmoja mwenye medali ya CAF?
 
Feisal yeye binafsi ndio anataka kuvunja mkataba na Yanga SC
 
very strategic sasa asiporejea ndipo atakumbana na adhabu ya yanga
 
Wachezaji wanatakiwa waangalie Sana wanapoingia mikataba na hiyo timu. Wachezaji kama binadamu wanaweza kufikwa na lolote la kulazimika kuachana na yanga. Wakati wa kusaini mikataba wachezaji wanatakiwa kuchunga Sana vipengele vya kuvunja mikataba.
Leo kwa Feisal, kesho kwa mwingine.

Nikikumbuka like varangati la Morrison, kipande cha karatasi kilichobeba sahihi hakijaonekana hadi leo.
Kwa staili hii Kuna mchezaji yanga atafungiwa na fifa kucheza mpira. Ni timu ngumu sana kwa wachezaji. Inaweza kuwasababishia matatizo makubwa baadae. Timu haina fair hata kidogo. Timu zingine haziko hivi.
 
Feisal ana mikataba mingapi? huo uanaosema ameuvunja ni upi? na aliopeleka barua TFF kuomba uvujwe ni upi?
Yanga walivyopeleka shauri TFF kulalamika Feisal amevunja mkataba walikuwa wanakusudia mkataba upi?

Wa fremu?
 
Morrison hakuwahi kusaini kabisa Yanga.
Mkataba wake wa kwanza walifoji saini yake.
Yaani Morrison alikuja Yanga wakati dilisha la usajiri lishafungwa.

Mkataba wa pili walifoji tena saini yake katika hicho kipande cha karatasi kilicho potezwa kwa makusudi.
Mkataba pekee alio tia saini yake ni huu wa sasa.
Yanga wana figisu sana wakisaidiwa na mstaafu.
 
Una bwabwaja tu
 
Fei kachemka Sana
Eti anasema sipendi kuichezea Yanga kama vile kucheza ni swala la Mapenzi wakati ni swala la Mkataba. Hutaki kuendelea na timu, basi maliza mktaba halafu ukatae kuongezea, siyo tu kulala na kuamka kuwa hutaki kucheza. Mtot alikuwa na nafasi kubwa sana ya kumfuata Samatta ulaya lakini nadhani amejiharibia sana kwani timu za nje zitaanza kumwogopa kama siyo mtu anyeheshimu mikataba; yuko kama Putin. Hajui kama scouts wa timu za nje wanafuatilia mambo haya kwa karibu pia. Ni mambo ambayo alitakiwa ayamalize chini ya kapeti lakini yeye anapiga kelel kila sehemu.
 
Masharti ya mkataba wa Yanga na Feisal ni kama masharti ya Nape aliyotoa kwa kampuni la Starlink ya Elon Musk
Mbona hawajasonga kwenda CAS? Ili wakayaanike yale makandokando uliyosema yanayofichwa na TFF na kumpendelea Yanga

Nadhani kila siku kurudi hapo TFF ni kupiga mark time tuu
 
Fei apambane.

TFF na Yanga ni wababaishaji.

Huwezi mlazimisha mtu kufanya jambo asilolitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…