Yawezekana kama Mwanadamu Idi Amin alikuwa na Mapungufu yake ila nimegundua Afrika ya leo iliwahitaji akina Amin wengi ili kupiga hatua

Viongozi wa leo ( wa sasa ) wa Bara letu hili la Afrika na hata wa nchi yako hawajawahi Kuua Watu? Huna Akili acha Kunipotezea muda sawa?
Mbona nguvu kuu kumtetea dikteta amini,kama hakuwa muovu hizo killing chambers alijengea za nini,kwann aliruhusu utekaji wa watu wasio na hatia kwa kuruhusu magaidi watue Uganda
 
Absolute Nonsense.
 
tutajie maendeleo yeyote aliyoyafanay idi amini kwa kipindi chote alichotawala, zaidi ya kufukuza wahindi na kunyangánya/kuua biashara zao, kutupa vilema mto kagera, kula nyama za watu na kulala na wanawake.

Ugomvi wake na wahindi ulikuwa kwanini wajihesabie ni waganda, ilhali wanajitenga na waganda (ubaguzi kwa waganda weusi). Kitu kingine kilimkera Amin ni wengi wa watoto wa kihindi waliosomeshwa na serikali katika fani mbali mbali zinazohitaji utaalamu, tena nje ya nchi na kwa gharama, hawakurudi kuitumikia nchi, badala yake waliingia sekta binafsi ambazo huduma zake wananchi wa kawaida hawakuzimudu.

Alijaribu kuongea nao kuhusu hili na mengine, ila jamaa hawakumsikia. Mwisho wa siku akawaambia kama wamegoma kuishi kama waganda, wabebe vyote vilivyo vyao na waende zao ndani ya siku 100.

Amin alikuwa zaidi ya Nyerere na Western propaganda. Jaribu kusoma zaidi. Unaweza kuta Mwendazake kafanya uovu zaidi ya jamaa(facts).
 
Asante Mkuu na Siku zote GENTAMYCINE huwa naungwa mkono Hoja zangu na Watu Werevu ( Einsteins ) tu kama Wewe hapa JamiiForums na Wachache, ila Sikubaliki, Sieleweki na Kutwa nachukiwa na Mipopoma ( Mijuha ) mingi mno.
Wengi huendeshwa na chuki za kisiasa badala ya uhalisia,ushabiki wa kisiasa uliopitiliza nao ni ugonjwa kama magonjwa mengine,unakuta mtu anatamani kiongozi fulani afeli kwenye uongozi wake kisa yeye hamshabikii au kuunga mkono chama kinachotawala na kusahau kua maendeleo ya nchi ni kwa nchi na hayabagui nani anashabikia au kisa tu haungi mkono chama ambacho kipo madarakani!

Binadamu kwa kawaida kitu cha kwanza ni dini yake na Mungu wake ila kitu cha pili ni utaifa wake na nchi yake.
 
Kuna kipindi alisafiri kwenye boti..akawa anawasalimia mamba...akasema they greeting me too...

Kuna documentary Moja ilifanya nimpende Sana amin...
 
Dikteta yeyeto ni ajent wa kuzimu ndio maana ni lazima wanatoa kafara za damu za watu kwa shetani Ili kupata nguvu
Kwa muda niliofatilia hizo shuhuda
Sijawahi kuona kiongozi yeyote mzungu katajwa kuonekana kuzimu
Ikizingatiwa viongozi wazungu waliua watu wengi tu refer to Napoleon Bonaparte

Wanaotajwa Ni kutoka Africa na nchi nyingine za dunia ya tatu nyingi zikiwa Ni zile zenye uadui na wazungu wa magharibi.

Kwahiyo hakuna reference ya unachokileta hapa
 
Marehemu Idi Amin Dada....

1. Alichukia Upuuzi ( Upumbavu )

2. Alichukia Uonevu na Dharau

3. Aliwapenda sana Wananchi wake

4. Hakuwa Mnafiki na wa Kujipendekeza

5. Hakuwa Muoga kuipigania nchi yake

6. Hakuwa Fisadi ( Mwizi ) hata kidogo

7. Alikuwa Mbabe ili Kulinda nchi yake

Sasa wakati umefika kwa Waafrika Kukiri kuwa tulikosea au tulilazimishwa tu na 'Mabeberu' katika Kumchukia Idi Amin Dada hivyo tuombe Radhi kwa Familia yake na hata kwa Mwenyezi Mungu ikiwezekana.

Kwa mtazamo mfupi tu ni kwamba kama nikisema niyapime Madhambi ya Marehemu Idi Amin Dada kipndi chake na hawa Viongozi wa sasa wa Afrika tulionao Mzani wangu utalalia hasa kwa Viongozi wa sasa kwani 90% yao wanafanya ( wanatenda ) maradufu ya aliyokuwa akiyafanya Idi Amin Dada ila Waafrika wengi ama kwa Unafiki wetu au kuwa Kwetu Mapopoma ( Majuha ) au kwa Kushikiwa kwa muda Akili zetu na Mabeberu ( Wazungu ) tunaogopa Kukemea, Kukosoa na hata Kusema Ukweli juu ya Masuala Mtambuka katika nchi zetu nyingi ( kama si zote ) za Kiafrika.

R.I.P sana tu Marehemu Idi Amin Dada.
Nasimama na wewe

Huyu mwamba alikua Ni shujaa kwenye kipindi chake

Alipinga Sana uonevu wa Israel Kwa parestina
Lakini pia alikua na ndoto ya kuona Africa ikisonga mbele bila utegemezi wa nje

Alikua msitari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi Africa kusini .

Kuna mengi

Nikipata muda nitayaleta

Wanaosema alikula nyama za watu walete reference
 
Hata Mimi nilivyokua mdogo niliamini Idd Amin Dada alikua mbaya Sana,nikisikia propaganda Kali kumhusu nilivyokua nikajua ule ulikua ni uongo mkubwa kwanza jamaa alikua mzalendo Kwa taifa lake na alikua anaamini anachokisimamia japo hakua na Elimu kubwa,
Ila kuhusu vita vya kagera chanzo alikua swahiba wa mchonga yule Mwendawazimu Obotte aliyepinduliwa Kwa Ujinga wake akakimbilia bongo na kuogarnize waasi na Kuanza shambulia Uganda akitokea Tanzania hicho Ndio chanzo Cha mgogoro ule uliopelekea vita vya kagera,

Imagine umemtimua hawara Yako nyumbani kwako halafu akimbilie Kwa Mwanaume jirani Yako halafu Huyo hawara aungane na bwana yake kukuletea vurugu hata kama ni Wewe ungekubali kejeri?

Hicho ndicho nikijuacho!
 
Kwa muda niliofatilia hizo shuhuda
Sijawahi kuona kiongozi yeyote mzungu katajwa kuonekana kuzimu
Ikizingatiwa viongozi wazungu waliua watu wengi tu refer to Napoleon Bonaparte

Wanaotajwa Ni kutoka Africa na nchi nyingine za dunia ya tatu nyingi zikiwa Ni zile zenye uadui na wazungu wa magharibi.

Kwahiyo hakuna reference ya unachokileta hapa
Kuzimu wapo viongozi wa race zote wakila msoto suluba gereza moja na masikini, kule Hakuna madaraja sijui nilikuwa mfalme, tajiri au Rais duniani hivyo ni vyeo vya duniani.Wanataja viongozi wa kiafrica kulingana na ufahamikaji wa mazingira yetu, yupo hittler, mao, saddam, ossama, race zote waliokula raha kwa kutesa watu
 
Sijawahi kuona au kusikia Lincoln, King Leopold II, Alexander the great na wengine wengi wakitajwa kuonekana kule pamoja na kuua watu wengi
Lakini pia walikua na umaarufu mkubwa hapa duniani kuliko hata hao kina Idd amini
 
Kula nyama za watu mi uwa naamini ni uongo walikuwa wanamchafua ili aonekane wa hovyo.Imagine Magu hapa alijaribu kutupeleka kibabe kidogo na maendeleo tuliyaone tena kwa kasi sana but ni mangapi mabaya amesemwa na mabeberu na sisi wenyewe?Hivi tungelipata kina Magu km watano wakiongoza kwa kufululiza kwa style ya kibabe unadhani hii nchi ingefika wapi kimaendeleo!Tulingelifika mbali.Nakwambia nchi zetu bado zinahitaji viongozi wababe ili zisonge,naunga mkono mada kwani bado tunawihataji kina Idd Amin,kina Gaddaf,kina Magu ili tusonge mbele,wabongo sie tukiongozwa kwa kubembelezwa hatuwezekani tena.
Leo tunamlilia Idd Amin, kuwa alikuwa na mazuri yake. Lakini ni sisi hawa hawa tunaomtukana Magufuli. Tunamuona hakufaa! Waafrika hatujui tunachokihitaji. Nakumbuka nyakati fulani za Kikwete, watu walilalamika kuwa ni dhaifu. Wakasema imefikia wakati Tanzania tupate Rais ambae ni mkali, walau dikiteta kidogo ili nchi inyooke.

Mungu akasikia swala zetu, akatuletea Magufuli. Yaani sikuamini, alitukanwa na kubezwa. Mungu akamchukua, lakini kivuli chake bado kinawatesa watu, wanaendelea mtukana hata kama kesha tangulia mbele ya haki. Waafrika hatueleweki, tunajipendekeza tu.

Idd Amini alikuwa ni kiongozi mzuri sana, na mfananisha na Magufuli. Iddi Amini akubabaishwa na mataifa ya nje. Aliitetea Uganda. Aliwezesha wanawake wa Uganda kushika nafasi mbalimbali katika utumishi. Alipenda kunyanyua kipato cha waganda. Alipokuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika kwa wakati huo, alipendekeza liundwe jeshi la Afrika likamtoe mzungu kule Zimbabwe au Rhodesia. Alikuwa na mawazo ya kufanya Afrika yenye nguvu inayojiamulia mambo yake yenyewe.

Hata sasa wangada wamegundua Idd Amin hakuwa na mabaya tu, bali kuna mazuri aliyo tenda. Hivyo wamekuwa na maonesho maalum kila mwaka ya kumbukizi ya Idd Amin kwa yale aloyafanya wakati wa utawala wake. Ikilenga kuona alivyoipigania Uganda.

Wazungu wanataka uwarambe miguu ili wakusifie na kukutangaza dunia nzima. Mandela katoka Gerezani, hakuna alichofanya kwa wananchi wake hasa weusi. Bado ni masikini wa kutupwa. Leo Mandela anahesabika shujaa. Uwa najiuliza ushujaa wa Mandela ni nini? Ulaya na Marekani hadi Asia na hata Arabuni, nchi hizi zimepiga hatua kwakua na viongozi wenye misimamo wanaotazama maslahi ya nchi, na ni wababe.

Leo sisi tunaabudu wazungu. Hivi China ingekuwa inaabudu wazungu ingefika hapo ilipo? Nchi za Mashariki ya kati nazo je? Libya walianza waabudu tazama walivyowaharibia nchi kisha wamekimbia. Ebu tusimame na miguu yetu. Mzungu alivyo anapenda kuabudiwa, mzungu anaamini kuwa mtu mweusi ni binadamu wa mwisho katika dunia. So hata ujipendekeze vipi, atakuona weye ni mtu usiefaa, atakutumia kwa maslahi yake tu. Japo ni wachache sana tena individual wenye kuthamini utu wa mwafrika mweusi.

Nchi kama nchi tupo tupo tu, hatujui nini maono yetu. Kila wakati tunakaa kusifia wazungu, nakujikomba kwao. Wakati nchi inawasomi tena tuna vijana wana akili sana za ubunifu na utafiti. Hatuna mpango wa kuwekeza katika tafiti. Ndo maana hadi leo maadui watatu toka uhuru hatujafanikiwa kuwamaliza.

Hivi ni kweli tunashindwa kujipanga na kuhakikisha kuwa tunakuwa na huduma ya afya iliyo bora kwa kila mtanzania? Hivi tunashindwa kujipanga kuhakikisha tuna elimu nzuri ya kisasa kwa kila mtanzania?

nashukuru nimewahi fanya kazi serikalini nilijifunza mengi na kushangaa mengi. Kwa staili iliyopo, na viongozi wetu. Tanzania tutabaki tulivyo hata miaka mia ijayo. Tuombe Mungu tupate viongozi watakaofikiria Taifa na si kujifikiria wao na wapambe wao.

Kuna hizi ofisi za wakurugenzi, ebu jiulize ni kitu gani wanakifanya katika halmashauri zao na wananchi wa eneo husika wakafaidika? Wanamipango isiyotekelezeka. Kila mwaka ni ileile utasikia mchakato wawawawa....kujenga....na nana....
Miji yetu mingi haina Maktaba, haina huduma nzuri za afya, haina miundo mbinu. Lakini bajeti zinapangwa. Wamama wajawazito wanakufa kwa kukosa huduma. Huku wakurugenzi na wakuu wa idara wakiishi maisha ya kifahari na familia zao.

Naongea haya kwa machungu kwa sababu najua. Tanzania bila ubabe hakuna kitakacho fanyika. Mie mwenyewe wakati niko huko nilikuwa mbabe ili huduma ifanyike. Nilichukiwa. Nilipata malalamiko mbalimbali, watu kukataliwa kupewa huduma hospitali, nililazimika kwenda nao hospitali kulazimisha wapewe huduma. Nilitumia ubabe wanafunzi kusoma hata kama hajalipa ada. Wananchi kunyang'anywa mali zao, wengine kuuwawa.

Nilitumia ubabe kulazimisha polisi kutowaweka ndani watu bila dhamana, sikuangalia mambo ya chama. Baadhi ya viongozi ndo waliodhurumu haki za wananchi. Nilikataa hiyo dhuruma. Nilikataa fedha yoyote ya zawadi au asante kutoka kwa mtu binafsi, halmashauri, au idara yoyote ile ya serikali. Ila ili uweze haya yote inabidi uikane nafsi yako, na kuishi maisha ya kawaida.

Bila ubabe tusidanganyike kwa tanzania yetu tutaendelea kuwa tulivyo. Nimeandika haya yote na kutoa mifano kuonesha tu, bila uzalendo, na wakati mwingine ubabe hakuna kitakachofanyika.
 
Ugomvi wake na wahindi ulikuwa kwanini wajihesabie ni waganda, ilhali wanajitenga na waganda (ubaguzi kwa waganda weusi). Kitu kingine kilimkera Amin ni wengi wa watoto wa kihindi waliosomeshwa na serikali katika fani mbali mbali zinazohitaji utaalamu, tena nje ya nchi na kwa gharama, hawakurudi kuitumikia nchi, badala yake waliingia sekta binafsi ambazo huduma zake wananchi wa kawaida hawakuzimudu.

Alijaribu kuongea nao kuhusu hili na mengine, ila jamaa hawakumsikia. Mwisho wa siku akawaambia kama wamegoma kuishi kama waganda, wabebe vyote vilivyo vyao na waende zao ndani ya siku 100.

Amin alikuwa zaidi ya Nyerere na Western propaganda. Jaribu kusoma zaidi. Unaweza kuta Mwendazake kafanya uovu zaidi ya jamaa(facts).
Bahati mbaya ni kwamba JamiiForums Members ambao ni very Intelligent and good in reasoning ( Critical Thinking ) kama Wewe Mkuu na huyu The Icebreaker mpo Wachache sana ( tena wa Kuhesabika kabisa ) isipokuwa Mipopoma ( Mijuha ) ndiyo mingi tu.
 
Leo tunamlilia Idd Amin, kuwa alikuwa na mazuri yake. Lakini ni sisi hawa hawa tunaomtukana Magufuli. Tunamuona hakufaa! Waafrika hatujui tunachokihitaji. Nakumbuka nyakati fulani za Kikwete, watu walilalamika kuwa ni dhaifu. Wakasema imefikia wakati Tanzania tupate Rais ambae ni mkali, walau dikiteta kidogo ili nchi inyooke.

Mungu akasikia swala zetu, akatuletea Magufuli. Yaani sikuamini, alitukanwa na kubezwa. Mungu akamchukua, lakini kivuli chake bado kinawatesa watu, wanaendelea mtukana hata kama kesha tangulia mbele ya haki. Waafrika hatueleweki, tunajipendekeza tu.

Idd Amini alikuwa ni kiongozi mzuri sana, na mfananisha na Magufuli. Iddi Amini akubabaishwa na mataifa ya nje. Aliitetea Uganda. Aliwezesha wanawake wa Uganda kushika nafasi mbalimbali katika utumishi. Alipenda kunyanyua kipato cha waganda. Alipokuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika kwa wakati huo, alipendekeza liundwe jeshi la Afrika likamtoe mzungu kule Zimbabwe au Rhodesia. Alikuwa na mawazo ya kufanya Afrika yenye nguvu inayojiamulia mambo yake yenyewe.

Hata sasa wangada wamegundua Idd Amin hakuwa na mabaya tu, bali kuna mazuri aliyo tenda. Hivyo wamekuwa na maonesho maalum kila mwaka ya kumbukizi ya Idd Amin kwa yale aloyafanya wakati wa utawala wake. Ikilenga kuona alivyoipigania Uganda.

Wazungu wanataka uwarambe miguu ili wakusifie na kukutangaza dunia nzima. Mandela katoka Gerezani, hakuna alichofanya kwa wananchi wake hasa weusi. Bado ni masikini wa kutupwa. Leo Mandela anahesabika shujaa. Uwa najiuliza ushujaa wa Mandela ni nini? Ulaya na Marekani hadi Asia na hata Arabuni, nchi hizi zimepiga hatua kwakua na viongozi wenye misimamo wanaotazama maslahi ya nchi, na ni wababe.

Leo sisi tunaabudu wazungu. Hivi China ingekuwa inaabudu wazungu ingefika hapo ilipo? Nchi za Mashariki ya kati nazo je? Libya walianza waabudu tazama walivyowaharibia nchi kisha wamekimbia. Ebu tusimame na miguu yetu. Mzungu alivyo anapenda kuabudiwa, mzungu anaamini kuwa mtu mweusi ni binadamu wa mwisho katika dunia. So hata ujipendekeze vipi, atakuona weye ni mtu usiefaa, atakutumia kwa maslahi yake tu. Japo ni wachache sana tena individual wenye kuthamini utu wa mwafrika mweusi.

Nchi kama nchi tupo tupo tu, hatujui nini maono yetu. Kila wakati tunakaa kusifia wazungu, nakujikomba kwao. Wakati nchi inawasomi tena tuna vijana wana akili sana za ubunifu na utafiti. Hatuna mpango wa kuwekeza katika tafiti. Ndo maana hadi leo maadui watatu toka uhuru hatujafanikiwa kuwamaliza.

Hivi ni kweli tunashindwa kujipanga na kuhakikisha kuwa tunakuwa na huduma ya afya iliyo bora kwa kila mtanzania? Hivi tunashindwa kujipanga kuhakikisha tuna elimu nzuri ya kisasa kwa kila mtanzania?

nashukuru nimewahi fanya kazi serikalini nilijifunza mengi na kushangaa mengi. Kwa staili iliyopo, na viongozi wetu. Tanzania tutabaki tulivyo hata miaka mia ijayo. Tuombe Mungu tupate viongozi watakaofikiria Taifa na si kujifikiria wao na wapambe wao.

Kuna hizi ofisi za wakurugenzi, ebu jiulize ni kitu gani wanakifanya katika halmashauri zao na wananchi wa eneo husika wakafaidika? Wanamipango isiyotekelezeka. Kila mwaka ni ileile utasikia mchakato wawawawa....kujenga....na nana....
Miji yetu mingi haina Maktaba, haina huduma nzuri za afya, haina miundo mbinu. Lakini bajeti zinapangwa. Wamama wajawazito wanakufa kwa kukosa huduma. Huku wakurugenzi na wakuu wa idara wakiishi maisha ya kifahari na familia zao.

Naongea haya kwa machungu kwa sababu najua. Tanzania bila ubabe hakuna kitakacho fanyika. Mie mwenyewe wakati niko huko nilikuwa mbabe ili huduma ifanyike. Nilichukiwa. Nilipata malalamiko mbalimbali, watu kukataliwa kupewa huduma hospitali, nililazimika kwenda nao hospitali kulazimisha wapewe huduma. Nilitumia ubabe wanafunzi kusoma hata kama hajalipa ada. Wananchi kunyang'anywa mali zao, wengine kuuwawa.

Nilitumia ubabe kulazimisha polisi kutowaweka ndani watu bila dhamana, sikuangalia mambo ya chama. Baadhi ya viongozi ndo waliodhurumu haki za wananchi. Nilikataa hiyo dhuruma. Nilikataa fedha yoyote ya zawadi au asante kutoka kwa mtu binafsi, halmashauri, au idara yoyote ile ya serikali. Ila ili uweze haya yote inabidi uikane nafsi yako, na kuishi maisha ya kawaida.

Bila ubabe tusidanganyike kwa tanzania yetu tutaendelea kuwa tulivyo. Nimeandika haya yote na kutoa mifano kuonesha tu, bila uzalendo, na wakati mwingine ubabe hakuna kitakachofanyika.
Mkuu kwa post yako hii nzuri na iliyosheheni kila Madini na iko very analytical pamoja na some vivid and logical references ambayo imeniaminisha pia kuwa Wewe ni Mtu Intelligent mno naomba kuanzia sasa nikutunuku Hadhi ya Uprofesa na niwe nakuita Profesa. Umemaliza kila Kitu na Heko ( Kongole ) sana.
 
tutajie maendeleo yeyote aliyoyafanay idi amini kwa kipindi chote alichotawala, zaidi ya kufukuza wahindi na kunyangánya/kuua biashara zao, kutupa vilema mto kagera, kula nyama za watu na kulala na wanawake.
Unajua kwann aliwafukuza wahindi

Ova
 
Back
Top Bottom