Yesu ni Mungu. Kwanini alijalibiwa na kiumbe alichokiumba (shetani) Huoni kama alionyesha udhaifu wake?

Unaambiwa aliuvaa mwili wa kibinadamu, utukufu wa kiungu aliuacha mbinguni. Ndio shetani akamjaribu ili amsujudu. Elewa hilo ni somo yakupasa usiwe na tamaa ya kutaka vitu harakaraka bila kufamya kazi utageuka kuwa mtumwa. Usiwe na masikio ya utafiti utapotea
 
Haya ni kwa mujibu wa....? Maandiko au hisia zako? Kama ni maandiko tuletee utusaidie na sisi tuone na tujifunze andiko linalosema mungu alijiuvua uungu na kujivisha ubinadamu! Ili yeye mungu ajaribiwe na kiumbe alichokiumba yeye mwenyewe,ili yeye mungu ajaribiwe kiumbe alichokilaani yeye mwenyewe! Tufundishane!
 
Shetani aliujaribu mwili wa Yesu Si Roho.

Uungu wa Yesu ni katika Roho,

Mwili ulikuwa ni vazi la Muda tu Kwa KAZI maalum ya Ukombozi.

Yesu akamjibu shetani, imeandikwa, usimjaribu BWANA Mungu wako.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
 
Samson Ernest unasemaje kuhusu hili?
Napenda kukumbusha kuwa Mungu huwa anaongea na shetani kwa mjibu wa maandiko haya;

Ayu 1:6-9, 11-12 SUV
[6] Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. [7] BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. [8] Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. [9] Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?
[11] Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. [12] BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA.

Sasa kuhusu shetani kujibishana na Yesu, napenda ufahamu kuwa alikuwa na mwili, hii inatuthibitishia alikuwa mwanadamu asilimia 100 na Mungu asilimia 100. Shetani alikuwa anatumia nafasi yake kufanya anachoona kinafaa kwake.
 
1.Kama wewe ni mwana wa Mungu geuza jiwe kuwa mkate
2. Ukinisujudia nitakupa mali zote za ulimwengu

Mali zote ni za Mungu kwani Shetani ampe Mungu ahadi na masharti yote hayo?

Shetani Alikua ameshapewa ulimwengu kuwa milki yake .

Ila wakati ukifika alitakiwa aje mwenye nguvu kuliko yeye ili aweze kumnyang'anya .

Kumbuka shetani alikua ni kiumbe chenye daraja la juu sana huko kwenye ulimwengu wa kiroho .
Anajua protocol yote ya kudili naye.

Komando wa jeshi akiasi hawezi kukamatwa na askari wa kawaida ni lazima awe ni mwenye mafunzo kuliko yeye na awe na tenki ya juu .

Mungu ni ufalme kamili
 
Shetani aliujaribu mwili wa Yesu Si Roho.

Uungu wa Yesu ni katika Roho,

Mwili ulikuwa ni vazi la Muda tu Kwa KAZI maalum ya Ukombozi.

Yesu akamjibu shetani, imeandikwa, usimjaribu BWANA Mungu wako.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
Wapi yesu amesema yeye uungu wake upo katika roho? Mbona unampa dhambi ya bure mtu wa watu!

Halafu umeandika vizuri sana. yesu akamjibu shetani, imeandikwa, "usimjaribu BWANA Mungu wako"

Aliyaongea hayo wakati ambao shetani anamjaribu yeye.alipoambiwa ajitupe aone kama mungu ataruma malaika wamdake,ndio akajibu hivyo.

Hiyo inamaana kwamba yesu alikuwa na akili timamu,alikubali kujaribiwa yeye,ila swala la yeye kumjaribu mungu alilikataa,kwanini? Kwa sababu anajua Mungu hajaribiwi!
 
Sasa huelewi vipi hapo kuwa Yesu alijitambulisha kuwa ni Mungu?

Kumjibu shetani imeandikwa " Usimjaribu BWANA Mungu wako, hapo ni baada ya shetani kumusema " Ikiwa u mwana wa Mungu ".

Sasa shetani ajua Yesu alikuwa mtu katika mwili, na ni Mungu katika Roho,

Wewe kwann Fikra hazikurudii kungamua hayo?
 
Aliruhusu ajaribiwe au unasoma maandiko yapi?

Mungu alikubali ajaribiwe full stop .

Unataka kuniambia Yesu hakuwa anamfahamu shetani kabla?

Na kama alikuwa anamfahamu ilikuwaje Mungu aruhusu Yesu kujaribiwa na kiumbe ambavho yeye mwenyewe ( Yesu) anakijua nje ndani?
 
Sasa huelewi vipi hapo kuwa Yesu alijitambulisha kuwa ni Mungu?

Kumjibu shetani imeandikwa " Usimjaribu BWANA Mungu wako, hapo ni baada ya shetani kumusema " Ikiwa u mwana wa Mungu ".

Sasa shetani ajua Yesu alikuwa mtu katika mwili, na ni Mungu katika Roho,

Wewe kwann Fikra hazikurudii kungamua hayo?
Shetani mwenyewe anavomjaribu hakumuita yesu mungu,alimuita mwana wa mungu kama tulivo wana wa mungu mimi na wewe,ndio maana yesu,wewe na mimi wote tunamuita mungu BABA YETU.

halafu Kwani yesu kuzimu alipelekwa na shetani kwenda kufanya nini kama sio kujaribiwa?

Alipoambiwa na shetani kuwa kama akimsujudia atapewa miliki zote za dunia kwanini hakujibu kuwa imeandikwa usimjaribu bwana mungu,ila ikajibu Mali zote ni za mungu?
Jibu ni hakujibu hivyo kwa sababu pale alikua anajaribiwa yeye binafsi na sio mungu!

Na hata alipoambiwa ageuze jiwe liwe mkate (kwa sababu alikua na njaa),hakujibu kuwa usimjaribu bwana mungu wako,ila alijibu kuwa watu(na yeye akiwemo,kwa sababu yeye ndio aliyekuwa akijaribiwa) hawaishi kwa mkate bali kwa neno.

Hapo unaona yesu aliyakubali hayo majaribu yote mawili ila kwa sababu yeye ana akili timamu na imani juu ya mungu wake,aliyashinda!

Ila alipokambiwa KAMA ANAMUAMINI MUNGU,NA KAMA ILIVYOANDIKWA BASI AJIRUSHE ili Mungu atume malaika wamdake,
Hapo shetani alituma(alim-trick) yesu ili yesu amjaribu/AUPIME uaminifu wa ahadi za mungu juu yake,kwamba kweli atamtumia malaika wamdake kama ilivyoandikwa?
kwa kuwa yesu anaakili timamu hapa ndipo alipomjibu shetani kuwa mungu hajaribiwi!
Sijui unaelewa ndugu!!!!!!!!!!
 
1.Kama wewe ni mwana wa Mungu geuza jiwe kuwa mkate
2. Ukinisujudia nitakupa mali zote za ulimwengu

Mali zote ni za Mungu kwani Shetani ampe Mungu ahadi na masharti yote hayo?

Hakuna sehemu Yesu anajiita Mungu, bali Mwana wa Mungu. Hata shetani analijua hilo.
Ndiyo maana katika Mathayo 4 : 3, Mathayo 4 : 6 hata Luka 4 : 3, shetani alikuwa akimdhihaki/akimjaribu Yesu kwa kuanza kusema, "ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu ..."

Lakini inashangaza kuona wengi wanasisitiza kwa Yesu ni Mungu, tena Mweza Yote. Wakati kuna mengine mengi tu Yesu hayawezi wala kuyajua; soma Mathayo 24 : 36.
 
Hakuna sehemu Yesu anajiita Mungu, bali Mwana wa Mungu. Hata shetani analijua hilo.
Ndiyo maana katika Mathayo 4 : 3, Mathayo 4 : 6 hata Luka 4 : 3, shetani alikuwa akimdhihaki/akimjaribu Yesu kwa kuanza kusema, "ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu ..."

Lakini inashangaza kuona wengi wanasisitiza kwa Yesu ni Mungu, tena Mweza Yote. Wakati kuna mengine tu hawezi wala kujua.
Hii mpya kidogo!!!
 
Shetani mwenyewe anavomjaribu hakumuita yesu mungu,alimuita mwana wa mungu kama tulivo wana wa mungu mimi na wewe,ndio maana yesu,wewe na mimi wote tunamuita mungu BABA YETU.

halafu Kwani yesu kuzimu alipelekwa na shetani kwenda kufanya nini kama sio kujaribiwa?

Alipoambiwa na shetani kuwa kama akimsujudia atapewa miliki zote za dunia kwanini hakujibu kuwa imeandikwa usimjaribu bwana mungu,ila ikajibu Mali zote ni za mungu?
Jibu ni hakujibu hivyo kwa sababu pale alikua anajaribiwa yeye binafsi na sio mungu!

Na hata alipoambiwa ageuze jiwe liwe mkate (kwa sababu alikua na njaa),hakujibu kuwa usimjaribu bwana mungu wako,ila alijibu kuwa watu(na yeye akiwemo,kwa sababu yeye ndio aliyekuwa akijaribiwa) hawaishi kwa mkate bali kwa neno.

Hapo unaona yesu aliyakubali hayo majaribu yote mawili ila kwa sababu yeye ana akili timamu na imani juu ya mungu wake,aliyashinda!

Ila alipokambiwa KAMA ANAMUAMINI MUNGU,NA KAMA ILIVYOANDIKWA BASI AJIRUSHE ili Mungu atume malaika wamdake,
Hapo shetani alituma(alim-trick) yesu ili yesu amjaribu/AUPIME uaminifu wa ahadi za mungu juu yake,kwamba kweli atamtumia malaika wamdake kama ilivyoandikwa?
kwa kuwa yesu anaakili timamu hapa ndipo alipomjibu shetani kuwa mungu hajaribiwi!
Sijui unaelewa ndugu!!!!!!!!!!
Yesu mwanadamu Kwa kuvaa mwili ndiye aliyejaribiwa.

Mwili una njaa ndio maana akajaribiwa ageuze jiwe kuwa mkate,

Mwili una tamaa ya macho ndio maana alijaribiwa kupata fahari na utajiri wa duniani,

Mwili una kiburi Cha Uzima, ndio maana alijaribiwa ajitupe chini.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
 
Kilichonishangazi ni Yesu kubebwa mzima mzima na shetani na kumuonyesha ufalme wake wa dunia. Mungu aendeshwe na shetani?
Mawazo yako ni mazuri kwa upande wako boss. Lakini katika uhalisia ... Kama mkoa wa kujifunza mambo yote yataeleweka tuu kamanda
 
Yesu mwanadamu Kwa kuvaa mwili ndiye aliyejaribiwa.

Mwili una njaa ndio maana akajaribiwa ageuze jiwe kuwa mkate,

Mwili una tamaa ya macho ndio maana alijaribiwa kupata fahari na utajiri wa duniani,

Mwili una kiburi Cha Uzima, ndio maana alijaribiwa ajitupe chini.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
Mtumishi. Pongezi kwa maelezo. Ila isije ikachanganywa Yesu na Baba ni tofauti. Yesu ana baba yake . Na huko NDIO aliyekaa katika kiti Cha enzi. Pitia vizuri Ufunuo 4 na 5.
 
Back
Top Bottom