Yevgeny Prigozhin, Boss wa Wagner Group ahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege!

Yevgeny Prigozhin, Boss wa Wagner Group ahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege!

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, nini shida ndugu
Propaganda rahisi na watu wanakubali.
Nini kiliwatuma Ma commander wote wa Wagner wawe kwenye Ndege Moja?

Kwanini itokee soon after UK waseme wata itambua wagner as a terrorist group?
Yaani kuna fact nyingi zinagoma, ila nashangaa watu wanaamini.
 
Naomba ufafanuzi wako na mifano kidogo mkuu.
Kwa ufupi:
1. Admiral Nikolai Kuznetsov aliyeipigania nchi kwenye vita ya pili ya dunia akiongoza jeshi la majini baada ya vita alifukuzwa kazi mara mbili jeshini, kushushwa vyeo na kufukuzwa tena kazi na kuwekwa marufuku kujihusisha na jeshi la maji mpaka anakufa. Miaka kama 10 baadaye veterans na baada ya viongozi waliomfanyia vile kubwa wamekufa na wamestaafu ndio wakashinikiza serikali irudishe heshima yake akiwa marehemu.

2. Stalin aliua majenerali wengi jeshini kwenye Great Purge akihofia wenye uzoefu, uwezo na ushawishi watampindua. Aliua majenerali, wanasiasa, wahadhiri na kila sekta muhimu watu zaidi ya laki saba mpaka operation inaisha kama 1936 hivi. Ukitaka kujua madhara yake, vita na Finland walifanya vibaya sana sababu majenerali waliuwawa na wamefungwa wamebaki ndio mzee na wasio na uzoefu. WW2 inaanza Stalin akalazimika amtoe Konstantin Rokossovsky jela maana vilaza hawawezi ongoza jeshi na huyo jamaa akawa kati ya watatu muhimu kwenye jeshi vita ile.

3. Marshal Zhukov alifutwa vyeo baada ya kuwa maarufu vita ya pili ya dunia, akapelekwa uko mbali na akaja kurudishiwa vyeo baada ya Stalin kufariki.

4. Baada ya Stalin kufariki, mkuu wake wa usalama alihukumiwa kuuwawa wakiwa kwenye kikao cha kwanza cha kutafuta mrithi. Hapohapo kasomewa mashtaka na mtu asiye jaji, hakutakiwa kujitetea na akauwawa. Lavrentiy Beria alikuwa na roho mbaya sana yule, na aliuwa wengi yeye mwenyewe.

5. Putin alivyokuwa Rais alimuua mpinzani wake na aliyekuwa mwanasiasa makini zaidi ambaye alitakiwa ndio arithi badala ya Putin ila alikuwa mkali na amenyooka. Aliuwawa mtaani mjini Moscow mchana kweupe. Assume Lowassa alikuwa the best kuliko Magufuli, Magu achaguliwe na mafisadi, baadae aue upinzani na Lowassa apinge hiyo hatua, Magu amuue Lowassa.

6. Yuri Gagarin yule binadamu wa kwanza kwenda space alikufa kwa ajari ya ndege. That time astronomer ndio mtu wa maana sana nchi ile na anayeonekana ana akili sana. Yuri Gagarin akawa maarufu kuliko wanasiasa, wakamuua.

7. Kabla ya Sergei Shoigu kuwa waziri wa ulinzi, kuna Anatoly Serdyukov alikuwa waziri. Aliwekwa hapo baada ya Russia kufanya vibaya vita ya Georgia kanchi kadogo sana Kusini pale, na wakati huo jeshi lilitoka kufanya vibaya kwenye vita za Chechens ikaonekana hata kama inatakiwa ndiyo mzee, jeshi limeoza. Serdyukov alifanya makubwa sana ndani ya muda mfupi, huyo alichukiwa na wala rushwa wote na alikuwa very competent akaondolewa. Mageuzi aliyoianzisha yamelisaidia sana jeshi.

Hawa wapinzani wengine na waandishi wa habari wanaopewa Novichok na Polonium tuachane nao, nazungumzia mtu aliyeteuliwa na serikali akafanya kazi yake kwa ufasaha na aka-outnishe wakubwa. Usidhani IT specialists, developers, tech gurus, lecturers na wanasayansi wakubwa wanaokimbia Urusi ni wajinga. Nchi haina meritocracy kabisa ile.
 
Mimi si mshabiki wa haya mambo lakini nakataa jamaa hajapanda mwili hiyo ndege unless watuoneshe mwili wake angalau hata na mazishi yake fake angalau naweza kuamini japo kwa asilimia 15.
Russian Civil Aviation Authority wamethibitisha kwamba Yevgeny Prigozhin alikuwa ni miongoni mwa abiria 10 walokuwa kwenye orodha ya abiria katika ndege iloanguka.

Hii ni ndege yake binafsi Prigozhin na yasemwa juzijuzi ilipelekwa kwa matengenezo ya kawaida au "Routine Maintenance".

Hivyo hapo 1+1+2 =5-!
 
Mimi si mshabiki wa haya mambo lakini nakataa jamaa hajapanda mwili hiyo ndege unless watuoneshe mwili wake angalau hata na mazishi yake fake angalau naweza kuamini japo kwa asilimia 15.
kwa mtu yoyote yule anayeelewa mambo ataona kabisa hii kitu haiingii akilini......
Macommander wote wa juu wa Wagner kwenye Ndege moja.
 
Kwa ufupi:
1. Admiral Nikolai Kuznetsov aliyeipigania nchi kwenye vita ya pili ya dunia akiongoza jeshi la majini baada ya vita alifukuzwa kazi mara mbili jeshini...
Since hukuwepo wakati yote haya yanatokea, means umeyasoma na kuweka judgement zako.

Una uhakika source yako au wewe mwenyewe hamko biased?
 
Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin amefariki katika ajali ya ndege nchini Urusi, pamoja na watu wengine tisa waliokuwemo ndani pia wamefariki.

************************************************

Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin alikuwa kwenye orodha ya abiria wa kwenye ndege iliyoanguka nchini Urusi na kuwaua watu wote 10 waliokuwa ndani.

Inaaminika kuwa alikuwa ndani ya ndege hiyo.

Hapo awali, chaneli ya Telegram yenye mahusiano na Wagner, Gray Zone iliripoti kwamba ndege hiyo ilidunguliwa na walinzi wa anga katika mkoa wa Tver, kaskazini mwa Moscow.

Prigozhin aliongoza uasi wa mapinduzi yaliyoshindwa dhidi ya vikosi vya jeshi la Urusi mnamo Juni.

View attachment 2726574
BBC.
Walimuacha muacha kwanza Kwa ajili ya maandalizi ya successor wake ,mambo yamekaa mkao wamemaliza utata
 
Back
Top Bottom