Yevgeny Prigozhin, Boss wa Wagner Group ahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege!

Yevgeny Prigozhin, Boss wa Wagner Group ahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege!

Mmoja wa waanzilishi wa google ni mrusi.

Wale wanaojiita Jews family. Hao ni warusi. Fuatilia matajiri wengi marekani wana element za jews.
Siyo elements za Jews, Bali Marekani na Jews ni kama National na Panasonic.

South Africa uchumi mkubwa unamilikiwa na Jews, City of Cape Town kuna beach front panaitwa Victor & Alfred waterfront, hawa ni Wayahudi Wawili ndio wamiliki wa hiyo V&A waterfront.
 
Siyo elements za Jews, Bali Marekani na Jews ni kama National na Panasonic.

South Africa uchumi mkubwa unamilikiwa na Jews, City of Cape Town kuna beach front panaitwa Victor & Alfred waterfront, hawa ni Wayahudi Wawili ndio wamiliki wa hiyo V&A waterfront.

Hivi niambie. Tukiwa tunaongelea wayahudi hapa tunaongelea waisrael?

Mimi naongelea wayahudi wenyewe. Asilimia kubwa viongozi wakuu wa israel asili yao ni Russia Empire.

Nimekupatia mfano mmoja wa waanzilishi wa google ni mrusi.

Dunia hii ipo very complicated.
 
Kwa ufupi:
1. Admiral Nikolai Kuznetsov aliyeipigania nchi kwenye vita ya pili ya dunia akiongoza jeshi la majini baada ya vita alifukuzwa kazi mara mbili jeshini, kushushwa vyeo na kufukuzwa tena kazi na kuwekwa marufuku kujihusisha na jeshi la maji mpaka anakufa. Miaka kama 10 baadaye veterans na baada ya viongozi waliomfanyia vile kubwa wamekufa na wamestaafu ndio wakashinikiza serikali irudishe heshima yake akiwa marehemu.

2. Stalin aliua majenerali wengi jeshini kwenye Great Purge akihofia wenye uzoefu, uwezo na ushawishi watampindua. Aliua majenerali, wanasiasa, wahadhiri na kila sekta muhimu watu zaidi ya laki saba mpaka operation inaisha kama 1936 hivi. Ukitaka kujua madhara yake, vita na Finland walifanya vibaya sana sababu majenerali waliuwawa na wamefungwa wamebaki ndio mzee na wasio na uzoefu. WW2 inaanza Stalin akalazimika amtoe Konstantin Rokossovsky jela maana vilaza hawawezi ongoza jeshi na huyo jamaa akawa kati ya watatu muhimu kwenye jeshi vita ile.

3. Marshal Zhukov alifutwa vyeo baada ya kuwa maarufu vita ya pili ya dunia, akapelekwa uko mbali na akaja kurudishiwa vyeo baada ya Stalin kufariki.

4. Baada ya Stalin kufariki, mkuu wake wa usalama alihukumiwa kuuwawa wakiwa kwenye kikao cha kwanza cha kutafuta mrithi. Hapohapo kasomewa mashtaka na mtu asiye jaji, hakutakiwa kujitetea na akauwawa. Lavrentiy Beria alikuwa na roho mbaya sana yule, na aliuwa wengi yeye mwenyewe.

5. Putin alivyokuwa Rais alimuua mpinzani wake na aliyekuwa mwanasiasa makini zaidi ambaye alitakiwa ndio arithi badala ya Putin ila alikuwa mkali na amenyooka. Aliuwawa mtaani mjini Moscow mchana kweupe. Assume Lowassa alikuwa the best kuliko Magufuli, Magu achaguliwe na mafisadi, baadae aue upinzani na Lowassa apinge hiyo hatua, Magu amuue Lowassa.

6. Yuri Gagarin yule binadamu wa kwanza kwenda space alikufa kwa ajari ya ndege. That time astronomer ndio mtu wa maana sana nchi ile na anayeonekana ana akili sana. Yuri Gagarin akawa maarufu kuliko wanasiasa, wakamuua.

7. Kabla ya Sergei Shoigu kuwa waziri wa ulinzi, kuna Anatoly Serdyukov alikuwa waziri. Aliwekwa hapo baada ya Russia kufanya vibaya vita ya Georgia kanchi kadogo sana Kusini pale, na wakati huo jeshi lilitoka kufanya vibaya kwenye vita za Chechens ikaonekana hata kama inatakiwa ndiyo mzee, jeshi limeoza. Serdyukov alifanya makubwa sana ndani ya muda mfupi, huyo alichukiwa na wala rushwa wote na alikuwa very competent akaondolewa. Mageuzi aliyoianzisha yamelisaidia sana jeshi.

Hawa wapinzani wengine na waandishi wa habari wanaopewa Novichok na Polonium tuachane nao, nazungumzia mtu aliyeteuliwa na serikali akafanya kazi yake kwa ufasaha na aka-outnishe wakubwa. Usidhani IT specialists, developers, tech gurus, lecturers na wanasayansi wakubwa wanaokimbia Urusi ni wajinga. Nchi haina meritocracy kabisa ile.
Uko sahihi hapo kwenye great purge ya 1936 hadi 1937.Hii kadhia iliondoka na roho nyingi zisizo na hatia.
 
Thank you God,na iwe hivyo.Bado Putin. Binafsi nilikuwa ninasali huyu shetwani afe.
Maombi Yako kuhusu kufa kwa Putin yatapata shida sana ,kwani typo wengi tunaomuombea maisha marefu na afya njema kwa kazi nzuri anayoifanyia Dunia.

Hta hivyo maombi Yako yamekaa kibaguzi tuuu.
Mbona hukuomba wafe akina George Bush baba na mtoto,hukuomba wafe Obama na Clinton waliosanabisha vifo vingi zaidi duniani kuliko hata Putin?
Mungu anapima ujue,
 
Boss wa Wagner afe kizembe hivyo huu ni mchezo wa kina putin wanatuchezea ile mjuwe keshakufa ili mrelax kumbe mtu yupo Africa huku anapiga kazi

Russia sahv wanatumia akili kubwa mno kugain influence

Miez kadhaa nyuma hata ile mapinduzi ya wagner kuelekea moscow ilikua ni movie tu kina biden wakaingizwa chaka kumbe ilikua ni technique ya kuhamishia wapiganaji Beralus ili waizunguke vizuri Ukraine utake kumpindua mtu Putin akuache hai kwa miez yote hyo na ukiwa belarus mara africa akuache tu[emoji23][emoji23]

Huyu jamaa atakuja kuibuka mtabaki mnaduwaa hii tension ya Niger inafanya Russia na Wagner wacheze karata yao kwa umakini sana
Sasa wanamuigizia nani na ili iweje? Ingekua inabadilisha chochote hapo sawa, lakini hakuna wanachobadilisha, zaidi ya ku trend tu mitandaoni.
 


❗️Flashback to Putin's words on the 24th of June during the Wagner rebellion. (SUBTITLES)⚡️⚡️⚡️
 
Taifa liloongozwa shaghalabagala kama urusi watu mnapata wapi ujasir wa kulitetea!
 
Warusi wamemuua au drone za Ukraine zimemtundua?
Yote kwa yote ni hasara kubwa kwa warusi.

Sidhani kama ni hasara mana yeye sio alfa na omega wa hilo kundi,kitakacho fanyika ni kubadili kiongozi wa kundi mwenye maslahi na urusi
 
Wewe unamjua NIKOLA ZIGIC??

kama humjui unaishi dunia gani? Usidhani unachofatilia wewe kila mtu anakijua. We jali ulichoulizwa
NICOLA ZIGIC ni mwanasoka wa zamani wa Serbia, zamani ikiwa ni Yugoslavia. Huyu mchezaji alikuwa na uwezo wa kucheza mpira kama mshambuliaji wa kati. Jitahidi ujue na ufahamu watu wa dunia hii. Na wewe nikikuuliza Juma Nkhangaa au Sebastian Kinyondo walikuwa ni kina nani nchi hii utanijibu kweli au utabaki kung'aa macho tu?
 
Kilichompeleka kuvuruga maslahi ya Ufaransa huko NIGER ni kipi? Beberu hashikwi ndevu. Ndio maana Putin humtoi Kremlin make anajua yuko kwenye Target. Wenzake wako mkutanoni BRICS huko S. Afrika yeye kajichimbia ikulu.
Nashangaa watu wanaomsifia Putin ni mwamba kumbe jamaa muoga sana anashinda ndani tu.angeenda south Africa
 
Back
Top Bottom