Nimesoma majibu yako na mifano uliyoitoa sikumbuki kuwafahamu so siwezi sema chochote.
ila tukiielewa historia ya Russia, ndio utaelewa kwanini iko hivi ilivyo leo.
Russia kwa muda mrefu Imekuwa ni military state, Kwa sababu ya utawala wa kifalme na Mavamizi/matishio ya kutokea nje-napoleon, hitler, NATO. So taifa la dizaini hiyo, unaweza elewa mtazamo wa watawala dhidi ya wapinzani. Hatari ya historia ya mavamizi, huzaa ufisadi na ubwenye. At least baada ya Putin kuingia for 20 yrs amedhibiti power struggle iliyokuwepo kwa miaka mingi. Kwa ufupi Russia bado ni taifa linalojitafuta kuelekea kuwa taifa la 'kisasa' zaidi.
Comperatively, Marekani ina bahati kubwa ya kijiografia. BAHARI. Kuzungukwa na bahari, imeifanya kuwa na jeshi imara la majini, hivyo kuwa ngumu kuvamiwa na rahisi kujilinda.