Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Akili kubwa kabisa hii. Kweli mtu mwenye nia ya kutengeneza timu anaweza kuuza mchezaji mzuri tena wa kikosi cha kwanza kirahisi rahisi. GSM nadhani wao wapo kibiashara zaidi
 
Djuma, Aucho na Mayele hawatocheza labda ikitokea tukavuka hizi raundi na kuingia makundi ndipo tunaweza tumia zile nafasi ambazo CAF hutoa kwa timu kuongeza wachezji
Bro mbona nilisikia kama majina yao walishayapeleka huko Caf au ndio nilimquote Manara vibaya?

Hivyo zikipatikana muda wowote wanaeza?
 
Bro mbona nilisikia kama majina yao walishayapeleka huko Caf au ndio nilimquote Manara vibaya?

Hivyo zikipatikana muda wowote wanaeza?
Mi ninachojua wanatuchezea Akili tu. Kuna kipindi walisema ITC zimefika nje ya wakati, Mara zitakapofika watazipeleka,hapohapo wanasema hata kama CCL hawatacheza msijali ligi watacheza. Ni kweli majina waliyapeleka CAF ila hayana vibali hivyo mana yake CAF wameshafunga hilo zoezi hadi hapo litapofunguliwa tena!
 
Japo apunguze hasira mana kama ile juzi alipofanyiwa Sub hata maji aliyopewa aligoma kunywa.
Ile timu imekuwa na maandalizi mabovu tu,lakini wakipata muda Wa kukaa pamoja muda mrefu kidogo itakuwa nzuri sana. Ila ikijumuisha na hao wachezaji wasio na vibali siyo wale walocheza juzi pekee![emoji3]
 
Duuh! Kumbe ndio mana wakawa wanang'ata ng'ata maneno.
 
Huo ndio ukweli na wanajua mashabiki wengi wa yanga hatuwez kifikiri

Ikifuatilia hili sakata toka siku za mwanzo kabisa yule mnayemuita Eng Hersi alisema kila kitu ashamaliza tusiwe na hofu

Siku zilivyozid kwenda wachezaj wengne wanatambulishwa watu wakaanza kuhoj mbona Djuma Shaban hatambulishwi akajibu kuwa msiwe na waswas

Muda umefka wanaanza kutengeneza drama nyingi na majibu yasyo na uhalisia wowote

Kifup yanga hakuna mchezaj tuliyevunj mkataba kutoka nje tulochofanya n kuvizia wale ambao hawafai na timu zao huko na sisi tumewachukua

Mwaka wa 3 huu wanatoka wachezaj lundo tunaingiza lundo la wachezaj hiv jaman kwa utaratibu huu muunganiko utoke wapi hapo?

Makocha ndio usiseme wantimuliwa kila siku na ajabu wakamleta NABI ambaye kizungu hajui kiswahil hajui na wanajua kabisa weng was wachezaj wetu wanajua kiswahili angalau na kiingereza

Leo Dr mshindo msolwa akitaka kuongea na kocha anahitaj mkaliman na yeye ndio waongee kweli jaman hapo kuna shida mahali kwa yanga

Kuna Mahal nimesoma NCHIMBI anasema hamwelewi kocha huko mazoezn kwasababu ya lugha

Sababu ya kuona lugha n shida wakaona watujazie wachezaj wanaoongea kifaransa kutoka kongo ili kupata wakaliman

SAIDO NTOBANZOKIZA yupo yanga kwsababu ya mpira au ya ukalimani
maana hili nalo linahitaj mjadala mwingine kabisa

GSM yupo yanga kwa interest zake na si kuisaidia yanga kama tunavyoaminishwa

Tunaambiwa mechi za CAFCL hazina mashabiki lakn wao wanachangisha nauli watu waende huko NIGERIA swal la kujiuliza wanaenda kutembea au kufanya nn maana mashabiki hawaruhusiwi huko Kama timing Haina nauli ya kukod ndege so waseme tuchangie


SIUONI MWISHO MZURI WA TIMU YANGU

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mbona sisi wapole kitambo tu.
Leo mnajiita wapole sio??

Yani siku mkijshtuka Eng Hersi nae tayar ana viwanda kama GSM , [emoji23][emoji23][emoji23]

Hakuna mtu anaepiga pesa Kama huyu kwenye mpira wetu siku hz
 
Umeongea ukweli kwa kiasi kikubwa ila kuna maeneo nimecheka sana![emoji3]
 
Yapi hayo mkuu hebu yaainishe hapa kwa maslah mapana ya timu yetu mkuu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Si kwamba umekosea Bali nimecheka hapo kwa Nabi kutojua kiswahili wala kiingereza, ulivyouliza majukumu ya Saido, Nchimbi kutomwelewa mwalimu[emoji23] na hapo kwenye kuhamasisha washabiki wakate tiketi ili waende Nigeria ilihali hawatoruhusiwa kuingia uwanjani[emoji3]. Halafu hili la tiketi hata kwenye mechi ya juzi walitaka kutukatisha tiketi za viingilio mana pamoja na kujua hakutokuwa na washabiki bado wakaendelea kutoa tangazo la ukataji Wa tiketi hadi pale watu walipoanza kuhoji sana ndipo wakaachana nalo, sasa sijui huwa wanakusudia nini. Hao wachezaji Naamini watasaidia ila msaada wao hautokuwepo ktk mazingira ulipohitajika hasa, kutokana na usanii Wa viongozi wetu ktk hivyo vibali! Tusubiri msaada wao kwenye ligi kama tulivyoambiwa mana hukawii kumbiwa hata ligi hawatacheza[emoji2]
 
Mkuu kiukwel hii timu naona Kama viongoz wamefika ukomo wa kufikiri mkuu

Sasa unawaambia watu wakate tiketi za ndege halafu tunajua viwanjan hawaruhusiwi mashabiki HUONI KAMA HUU N WIZI KABISA MKUU

Unaambiwa mwenyekiti wa klabu hana nguvu kabisa yupoyupo tu

Msolwa ukimchunguza Sana hata uongeaji wake n Kama ana MTINDIO WA UBONGO VILE hayupo sawa yule jamaa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wanayanga wasipokuelewa hapa, wataelewa mbinguni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…