Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

MWINYI ZAHERA ATAJA SABABU YA KUTO MTUMIA JUMA ABDUL
.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hana tatizo na beki wa kulia wa timu hiyo Juma Abdul na anafahamu ni mchezaji mzuri lakini amesisitiza ni lazima awe 'fit' kuweza kwendana na kasi anayotaka

Kumekuwa wa presha kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wamekuwa wakihoji sababu ya Abdul kutocheza kwenye kikosi cha kwanza huku Zahera akiwatumia baadhi ya wachezaji katika nafasi wasizostahili

Mfano beki ya kulia anapokosekana Paulo Godfrey 'Boxer', amekuwa akiwatumia Ally Ally, Mustafa Suleyman, Mapinduzi Balama na Cleofas Sosopeter badala ya Abdul ambaye miaka yote amekuwa akicheza nafasi hiyo

Aidha Zahera amewataka mashabiki wawe watulivu na kuacha kuingia majukumu ya kiufundi "Unajua mashabiki wao wanataka kuwa makocha wapange wao kikosi mimi ndiye ninayekaa na wachezaji muda mwingi hivyo nafahamu nani ni bora zaidi ya mwingin" "Juma msimu uliopita hajacheza michezo mingi wachezaji ninaowapa nafasi wamecheza wakiwa katika timu zao," amesema "Sina maana kwamba ni mchezaji mbaya hapana ni mzuri na amekuwa akipambana kusaka nafasi ya kucheza muda ukifika atapana nafasi hiyo kwasasa naomba majukumu yangu niachiwe mwenyewe nisiingiliw," "Mpira wa Tanzania unaendeshwa na ushabiki wao wakipata matokeo wanasahau kabisa kuwa waliocheza ni wachezaji wasiowapenda wakikosa matokeo pia hawakosi kitu cha kuzungumza"

Abdul alikuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri Zambia wiki iliyopita ambapo mwishoni mwa wiki kilicheza Zesco United mchezo wa ligi ya mabingwa na kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1

Zahera alimtumia Ally Ally beki ya kulia huku Abdul akiwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa benchi

Pegine beki huyo anaweza kupata nafasi ya kucheza kwenye michezo ya ligi kuu ya Vodacom ambayo Yanga itacheza wiki hii

Alhamisi Yanga itacheza na Polisi Tanzania uwanja wa Uhuru kisha kurejea dimbani hapo siku ya Jumapili kuikabili Coastal Union.

Yangafulldozz
 
20191002_123412.jpg
BALAMA AONGEZA NGUVU YANGA
.
Kiungo Mapinduzi Balama amejumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kilichoingia kambini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania

Mchezo huo utapigwa kesho Alhamisi kwenye uwanja wa Uhuru

Balama amekuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza majeraha ya nyama za paja aliyopata kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United

Kurejea kwa kiraka huyo ni habari njema kwa kocha Mwinyi Zahera ambaye kesho kikosi chake kitashuka dimbani kusaka ushindi wa kwanza ligi kuu ya Vodacom msimu huu.

Yangafulldozz
 
Yanga haina mpango wowote, kelele zao ni hapa Tanzania tu tena magazetini na labda CECAFA kidogo. Hivi kati ya Simba na Yanga, ni nani mwenye mataji mengi zaidi CECAFA na ni nani mwenye makombe zaidi ya mwenzie. Jibu liko hapa, tusipende kusifia ujinga wakati ukweli uko dhahiri kabisa.
 
Back
Top Bottom