Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

KWA KAULI YA MO LEO BASI YANGA KUNA TATIZO KUBWA SANA

Anaandika @exaud_msaka_habari

Leo sasa rasmi kwa mara ya kwanza naandika kuhusu usajili wa @realclatouschama na tetesi za kwenda Yanga, na nafanya hivi baada sasa Simba kutoa kauli rasmi kuwa wamemuongezea mkataba wa miaka Miwili. Kwa mujibu wa Mo. Nlikuwa naogopa bila kuwa na chanzo

Baada ya kauli ya Leo kuwa Chama yupo Simba miaka miwili mingine, imenifanya nifikirie baadhi ya mambo ambayo timu kubwa kama Yanga nadhani walistahili wasifanye

1. Wasemaji wa Yanga wote na Baadhi ya mashabiki wao wametumia wiki mbili kuwadanganya mashabiki wao kuwa tayari wamemalizana na Chama, na hawakuwa na mafumbo walikuwa wanapost mpaka picha ya Chama mpaka kwenye gazeti la club, hii ina maana gani kwa timu kubwa kama Yanga

2. Mambo ya Usajili Yanga yanaendeshwaje?, mbona kila mtu anaongea, yani inawezekana wana mpango wa kumsajili chama ila Maneno mengi kabla ya kufanikiwa inaweza ikawa chanzo cha Kumkosa nawaza inakuwaje wasemaji wa timu wanasema kabisa wamemalizana naye wakati bado. wanawachukuliaje mashabiki wao

3. Mashabiki maarufu wa Yanga tena wale maarufu wanaoaminiwa na timu wamewaambia mashabiki wao kuwa leo Chamanzi wanaenda kimtambulisha Chama, wanawachukuliaje wanachama wa Yanga

4. Propaganda za soka zinaruhusiwa ila inawezekana Yanga hawajaelewa zinafanywaje, ukiangalia jinsi Manara anavyopost ishu ya Mukoko na jinsi Yanga wanapost ishu ya Chama ni tofauti, Manara yeye anapost kitu ambacho hata umpeleke mahakamani humkamati ila Yanga wanasema wamemalizana naye, na baya zaidi wanaopost ni wasemaji wa timu

Yanga kuna tatizo japo hawalioni na ukilisema wanaweza kukutusi ila haiwezekani kufanya propaganda kama ile kwenye swala ambalo wameshaona kabisa ni ngumu kufanikiwa

Wenzetu ulaya wanafanya vile wakiwa na uhakika wa asilimia 80 kuwa wanaweza kumpaka huyo mchezaji, ila Taarifa nilizonazo Chama amesaini Simba kabla hata Yanga hawajaanza kumpost mitandaoni na walikuwa wanajua

Baada ya yote haya sasa nimeondoka na kauli moja kuwa Simba na Yanga wote wanampenda Chama, kwahiyo hata Chama akiwa Simba ila tunajua na Yanga wanampenda sana na wanamtamani mno.

ALL IN ALL BORA LIMEISHA TUJADILI MENGINE SASA
chama_kubwa_msimbazi-___CHnJ9fPgfOT___-.jpeg
IMG-20201115-WA0008.jpeg
 
ALL IN ALL BORA LIMEISHA TUJADILI MENGINE SASAView attachment 1626943View attachment 1626945
Kumbe wew ndo yule dogo wa insta, pumbafuu
 
KOCHA wa Young Africans SC ya Dar es Salaam, Cedric Kaze, amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Oktoba msimu wa 2020/21.

Kaze aliwashinda Aristica Cioaba wa Azam FC na Francis Baraza wa Biashara United ambapo Kaze aliiongoza Yanga katika michezo mitatu na kushinda yote. Yanga chini ya Kaze ilizifunga Polisi Tanzania, KMC na Biashara United na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Cioaba aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza moja, huku Baraza akiiongoza Biashara kushinda michezo mitatu na kupoteza miwili ikipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya nne.
 
KIUNGO wa Young Africans SC ya Dar es Salaam, Mukoko Tonombe, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba msimu wa 2020/21.

Mwezi huo wa Oktoba, Yanga ilicheza michezo minne, ikiwa ndiyo timu iliyoshinda michezo yake yote na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom inayoshirikisha timu 18. Yanga ilizifunga Coastal Union 3-0, Polisi Tanzania 1-0, KMC 1-2 na Biashara United, 0-1 ambapo Mukoko alitoa mchango mkubwa katika ushindi huo ikiwa ni pamoja na kufunga bao moja dhidi ya Polisi Tanzania.

Mukoko aliwashinda mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube na mshambuliaji wa Gwambina FC, Meshack Abraham aliongia nao fainali, ambapo Dube aliiongoza Azam kubaki kileleni baada ya kuvuna pointi 10 katika mwezi huo, ikishinda tatu, sare moja na kupoteza moja, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za usaidizi wa mabao.

Kwa upande wa Meshack aliiongoza Gwambina kupata pointi nane ikishinda michezo miwili, sare miwili na kupoteza mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya 17 hadi ya 14 akiifungia timu yake mabao manne.
 
Back
Top Bottom