Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Jamani nalia na hawa jamaa.
Tafadhali rudini mkaokoe timu, itolewe kwa majambazi:-
1. George Mpondera "Castro"
2. Issa Makongoro-Mzee wa kuonga marefa.
3. Mengi - Mzee wa Yanga Kampuni.
 
Katika sababu hizo tatu , sababu pekee yenye kuleta sense ni ile ya tatu "MATOKEO YA DAR ES SALAAM".

Hata sababu hii wa kulaumiwa ni YANGA wenyewe kwa uzembe wao. Sababu zingine mbili ni upuuuuuuuzi mtupu.
 
Sababu kubwa nianavyo mimi ni viongozi kukosa Vission. ukitaka ku proove statement yangu subiri uone maandalizi ya mchezo wake na Simba March 14. watatumia resources zote ili waifunge Simba.

Inawezekana ni kosa la Wanachama wanaochagua viongozi kwa sababu kwa Yanga kiongozi mzuri ni yule anayeweza kupanga mikakati ya kuifunga Simba tu, akishindwa aidha migogoro kibao kama si bakora kutembezwa.

Imetolewa mapema wanachama tuliii kwa sababu ndiyo mfumo tuliozoea.
 
Yanga acheni kusajili wanenguaji!!!!!!! MAJINA MAKUBWA.....MSHAHARA MKUBWA......HAKUNA KITU...wachezaji wa kigeni wote hamna kitu bora mngewaongzea akina ngassa mshahara kwa hela mlizowanunulia AIBU,AIBU,AIBU MPAKA...............................................................................................................LOL!!!!
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha...
So Yanga tunajipanga na mambo yooote yatakwenda sawa...asanteni sana
 
Haya Azam...
Sisi ndo Yanga.
Sasa mrudi kiwandani kwenu Tazara mkakande mikate na Chapati....

Forza Yanga
 
Gang Chomba, Mtani Balatanda na Yebo yeboyebo wengineo nimeona niwafufulie thread yenu mpate kujipanga upya kwa msimu ujao.

Lakini tu msiwaonee Ndlovu na Maftah. Walikuwa wanajaribu kuziba jahadhi lililokwisha katika vipande vipande.

Ati na nyie mlitaka kuweka rekodi ya kushinda mechi zote za duru la pili. Thubutuuuuuuuuuuuuu
 
Nimekuwa nikufuatilia japo si kwa karibu sana maendeleo na michakato ya timu kongwe za mpira wa miguu nchini, Yanga na Simba.

Kwa muda mrefu timu hizo, kwa mtazamo wangu, zimekuwa zikiendeshwa kwa mfumo wa ujima, kwa maana kuwa hauna mtazamo wa kibiashara ama kiweledi (professionalism) kiasi cha kuzifanya timu hizo kushindwa kumudu gharama za msingi za uendeshaji na hivyo zibaki kuwa tegemezi kwa kiasi kikubwa kwa wafadhili licha ya kuwa timu hizo zina raslimali si haba ambazo kama kungekuwa na mtazamo chanya, zingeweza kutumika kama 'spring boards' za kujijengea uwezo wa kujitegemea.

mfano wa karibu hebu angalia matumizi ya jengo la Yanga na ile nyumba yao chakavu kweli kama kungekuwa na viongozi wenye mtazamo tofauti wangeshindwa kweli kuzitumia raslimali hizo kibiashara kuipaisha kimaendeleo timu yao? na hivyo kuondokana na utumwa unaotokana na utegemezi wa wafadhili ambao, kwa hali ya kawaida hawawekezi pasi kwanza kujihakikishia maslahi binafsi.

Simba nao ni kama Yanga, ingawa ki-mizania Simba wameonyesha mwanga kidogo kwa kukataa kutekwa wazima wazima na wafadhili, hususan kwa kujiwekea utaratibu wa mishahara ya wachezaji wao, na mwalimu kulipwa moja kwa moja na wafadhili wa ligi kuu ili angalau kuondoa na aibu kuwalamba miguu wafadhili wasisababishe mtafaruku klabuni kutokana na kususa kulipa mishahara na gharama za uendeshaji wa timu kwa wakati.

Sasa ni wakati mwafaka kwa viongozi wa timu na wapenzi wake kutafakari upya na kwa kina umuhimu wa timu hizo vijogoo nchini kuendeshwa kwa mfumo wa kibiashara, ambapo timu iwe kama kampuni inayojitegemea na inayoendeshwa kibiashara na wanachama na wapenzi wawe ni wabia ambao.
 
Hakuna mwenye uafadhali hapo. Kwa umri wake club hizo, hazikupaswa kuwa tegemezi bado kwa namna yoyote ile. Sijui lini watacommercialize uendeshaji wao kwa ngazi zote.

Supporters wao ni mtaji wao wa kwanza mkubwa sana kama wangeweza kuweka sokoni bidhaa zihusianazo 1 kwa 1 na vilabu hivi viwili
 
2405986_orig.jpg


Shabiki maarufu wa yanga mkoani Mtwara Suleiman Hamisi Kutoboa amefariki dunia jana Jumatatu asubuhi katika hospitali ya Mkoa wa Mtwara Ligula baada ya kuanguka mara baada ya kiungo, hillary Echesa kuifungia Simba bao la nne juzi jumapili.

R.I.P Shabiki Suleiman Hamisi Kutoboa, ama kweli nimeamini ukishabikia Arsenal ama Yanga ni presha tupu
 
Shabiki maarufu wa yanga mkoani Mtwara Suleiman Hamisi Kutoboa amefariki dunia jana Jumatatu asubuhi katika hospitali ya Mkoa wa Mtwara Ligula baada ya kuanguka mara baada ya kiungo, hillary Echesa kuifungia Simba bao la nne juzi jumapili.

R.I.P Shabiki Suleiman Hamisi Kutoboa, ama kweli nimeamini ukishabikia Arsenal ama Yanga ni presha tupu

Kakague senksi yangu ya kwanza kwako kwenye JF Mpya!
 
Na kuna mwingine alianguka uwanjani kaponea hospitali
 
uwiii yuko wapi my husband wangu ayasikie haya.....

kumbe this futboli thing can go to this extent huh??!!

RIP marehemu
 
Na kuna mwingine alianguka uwanjani kaponea hospitali

Nafikiri ni huyu hapa bana
DSC09163.JPG.jpeg

Hawa watu wanapenda mpaka kufa duh na wachezaji wanajua kuwa sasa huwa wanabeba roho za watu?

Hii ni kusema Echesa kaua huko Mtwara bila kukusuduia teh teh
 
Unazi mwingine ni kujitakia mauti tu, namshukuru Mungu unazi huo uliisha kwangu. Nakumbuka nilikuwa natoroka shule na kwenda kuruka ukuta uwanja wa Taifa na KArume ili kuiona Simba.
 
Nafikiri ni huyu hapa bana
View attachment 9616

Hawa watu wanapenda mpaka kufa duh na wachezaji wanajua kuwa sasa huwa wanabeba roho za watu?

Hii ni kusema Echesa kaua huko Mtwara bila kukusuduia teh teh

nadhani huyo wanayamsemea alikua ntwala huko... huyu wa dar labda alizinduka na kubadili timu aisee

kweli simba ni simba tu aisee... shoka moja mbuyu chini!!! Fululu-fululu watu wamekaa
 
duuh mpira tunatakiwa ku enjoy lakini saa nyingi mtu unaposhindwa kuji-control madhara yake yanakuwa makubwa sana.

r.i.p
 
Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya wachezaji watanzania wanaocheza soka nje ya nchi kwa sasa. Orodha inaonyesha mchezaji, nchi anayocheza na jina la club yake ya mwisho kuchezea kabla 'hajatimkia' nje ya nchi kucheza soka la kulipwa.

1. Muharami Mohamed - Msumbiji , former Simba player
2. Haruna Moshi “ Boban” - Sweden, former Simba Player
3. Henry Joseph Shindika– Norway, former Simba player
4. Victor Costa “ Nyumba” – Msumbiji , former Simba player
5. Renatus Njohole – Switzerland,former Simba Player
6. Athuman Machupa - Sweden, former Simba Player
7. Said Maulid – Angola – former Yanga player
8. Credo Mwaipopo - Sweden – former Yana Player
9. Nizar Khalfan – Canada, former Mtibwa player
10. Kalimangonga Remmy Mtoro Ongala –Sweden,former Kajumulo FC

Idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza nje utaona wanatokea club ya Simba SC " Wekundu wa Msimbazi"; najiuliza maswali yafuatayo
1. Je, wachezaji wa Simba wana vipaji zaidi kuliko wa Yanga ndo mana wengi wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi?

2. Je, wachezaji wa Yanga hawana mwamko wa kucheza nje ya nchi,kwa maana ingine wameridhika na "soka la bongo" ndo sababu ya idadi yao kuwa ndogo?

3. Je, viongozi wa Yanga wanawabania wachezaji wao kucheza nje ya nchi kwa maslahi yao binafsi?

Nini maoni yenu wana JF
 
Back
Top Bottom