change formula
JF-Expert Member
- Sep 8, 2020
- 729
- 1,559
Hata mimi kanishangaza sana, nimekuwa namuamini sana Lissu, lakini kwa hili la kushadadia habari za umbea!! Nimemuona ni mtu mwepesi sana.Mimi hao wengine hawanishangazi maana ndio kazi yao huko mitandaoni ila mtu kama Lisu ndio kaniacha mdomo wazi.
Kwa nafasi yake hakutakiwa kuwa na hoja za kuokoteza kama hizo, alipaswa awe na msingi wa hoja zake anazo simamia na ungekuwa ndio msimamo wake na heshima ingekuwepo, lakini kwa sasa namuona kama mlopokaji tu asie kuwa na hoja,zaidi ya kulalamika na kupinga kila anachofanya mh. Rais wa jamhuri.
Ajifunze kwa mwenzake mh. Balozi dk Slaa, kipindi yupo upinzani, alikuwa na hoja zake na misimamo yake ambayo ilimfanya kila mtu amuone ni president material,maana alikuwa akizungumza kila mtu alitaka kumsikilizaa,lakini sasa hivi Lissu watu wamempuuzia kwasababu ana ongea umbea tu. Upinzani wa tanzania bado una safari ndefu, umetukatisha tamaa sisi wengine tunaopenda sera mbadala zenye kuchochea maendeleo ya nchi yetu.