Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Amen!
Yaani una maana hospitali kubwa kama KNH inakataa kupokea wagonjwa kwa sababu yupo Magufuli! Yaani huo ni uongo kupita kiasi. Mtamuombea ugonjwa mtaugua nyie, mtamuombea kifo mwishjo mtakufa nyie. Acheni uzushi na chuki!
Men
 
Jamani tuache utani, Huyu Mh awe anaumwa tatizo la upumuaji aende hospitali kweli?

Mi ninavyomjua anavyoamini kwenye kupiga nyungu sidhani kama atakubali akahudumiwe na vifaa vya mabeberu wanaotaka kutuletea barakoa na chanjo ambazo zinataka kutuua.

Kwamba huyu huyu Mh amekiuka ushauri anaoutoa kwa raia wake kua wapige nyungu sana.

Mi nitaakua wa mwisho kuamini hadi nitakaposikia breaking news.
 
"When the wicked perish there are shouts of joy," The book of proverbs. Hii ni hatari kushangilia maradhi ya kiongozi wa nchi.
Who are the wicked and who will shout in joy in this context?
Tatizo ni kiongozi kuwa mwovu kwa watu wake kiasi cha kupelekea kumchukia...!!
 
Akitoka huko mafichoni tutajua kama ni kweli au siyo kweli. Kama ni kweli tunaona tu kwa muonekano wake. Si mlimuona Mpango alivyotoka alikuwaje?? Cov 19 haina masihala!! Ila kwa Msigwa na Abbas kushindwa kuwapa majibu Reuters inatia wasiwasi kidogo!!
 
Watanzania wa leo sio wa mwaka 1990 ambapo rais wao alikuwa anasikiliza kero zao kupitia wa wazee wa mji pale ukumbi wa Anatoglu. Leo hii kila mtanzania anaishi maisha ya kidigital zaidi ndio maana social media inatumika kupata habari kuliko print media.

Kwa kuishi maisha ya kidigital watu wanainteract sana na wanakuwa na kiu ya kupata habari mpya kila baada ya muda. Ina maana mtu anahitaji updates kila baada ya saa moja.

Kurugenzi ya mawasilano Ikulu kuwa kimya bila kuwa na updates juu ya utendaji kazi wa rais,afya yake au ratiba zake kwa wananchi ni kufanya kazi kizamani.

Nchi nyingi sasa wanafanya kazi kisasa zaidi. Maana utakuta ikulu nyingi wana Briefing rooms ambazo hutumika kutoa taarifa mpya za rais husika juu ya afya yake,utendaji kazi yake na hata kupokea kero za wananchi kila baada ya muda.


Mambo mengi sasa hivi yanaibuliwa kupitia social media pia hata kupitia print media. Tulitegemea Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu iwe inajibu mapigo ya habari zozote,kero au uzushi dhidi ya mkuu wa nchi. Maana sio vyema kukaa kimya kama vile sio watumishi wa wananchi ambao wamemchagua rais awe mtumishi wao. Tulitarajia kabisa kurugenzi ya mawasilano Ikulu ijibu juu ya hii sintofahamu juu ya rais wa JMT yupo wapi. Anaumwa? Haumwi?
 
Kwanini bwashee?

Kila panapokuwepo na ulazima wa kuhabarisha umma juu ya jambo lolote kurugenzi ya mawasiliani ikulu imekuwa ikituhabarisha.
 
Ukiona ndani ya jamii uliyomo ukipata matatizo wanasherehekea jiulize mara mbili mbili kuna nini? kwa uzoefu wangu wa miaka hii 70 niliyonayo viongozi wetu wa awamu hii wakipatwa na janga lolote wananchi wanashangilia. Kuna nini?
Ubimadam kazi
Binadam hata umpe nn haridhiki
Huwezi kupendwa na kila mtu
Kwani hao viongozi waliyopita kuitawala tz nao
Walipendwa...hiyo ni kawaida tu

Ova
 
Huu utawala wa siri siri ni utawala perfect hauna desturi ya kukili.madhaifu
1.CORONA SIRI
2.MGAO WA UMEME SIRI
3.KUUMWA SIRI
4.STATISTICAL DATA SIRI
5.KILA KITU SIRI
So tuwaache na MASIRI YAO
 
Nairobi Hospital - Kenya!?
Inamaana Kenya wanahuduma bora zaidi za afya hadi kuweza kutibu kiongozi ngazi za juu wa nchi jirani!? SITOKAA NIAMINI KABISA!
Ndiyo unajua leo? Kenya wako mbele vitu vingi sana. Mbona ni siku nyingi watanzania wakiugua na matibabu yakashindikana Tanzania, Nairobi ndiyo huwa kimbilio? Hili la kwenda India na Africa Kusini lilianza miaka ya karibuni.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…