Watanzania wa leo sio wa mwaka 1990 ambapo rais wao alikuwa anasikiliza kero zao kupitia wa wazee wa mji pale ukumbi wa Anatoglu. Leo hii kila mtanzania anaishi maisha ya kidigital zaidi ndio maana social media inatumika kupata habari kuliko print media.
Kwa kuishi maisha ya kidigital watu wanainteract sana na wanakuwa na kiu ya kupata habari mpya kila baada ya muda. Ina maana mtu anahitaji updates kila baada ya saa moja.
Kurugenzi ya mawasilano Ikulu kuwa kimya bila kuwa na updates juu ya utendaji kazi wa rais,afya yake au ratiba zake kwa wananchi ni kufanya kazi kizamani.
Nchi nyingi sasa wanafanya kazi kisasa zaidi. Maana utakuta ikulu nyingi wana Briefing rooms ambazo hutumika kutoa taarifa mpya za rais husika juu ya afya yake,utendaji kazi yake na hata kupokea kero za wananchi kila baada ya muda.
Mambo mengi sasa hivi yanaibuliwa kupitia social media pia hata kupitia print media. Tulitegemea Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu iwe inajibu mapigo ya habari zozote,kero au uzushi dhidi ya mkuu wa nchi. Maana sio vyema kukaa kimya kama vile sio watumishi wa wananchi ambao wamemchagua rais awe mtumishi wao. Tulitarajia kabisa kurugenzi ya mawasilano Ikulu ijibu juu ya hii sintofahamu juu ya rais wa JMT yupo wapi. Anaumwa? Haumwi?