Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Sitaongea mengi sana!

Lakini naomba kuwatafsiria jambo ili msipate tabu kuelewa!

LOGIC 1. Ukiona unayedhani alikuwa ni bikira anaamua kujitangaza rasmi mtandaoni kuwa ana mimba basi tambua kwamba kashajifungua mtoto tayali!

WHy? Ni kwasababu kama aliweza kuficha asijulikane kama anazini (anafanywa) , katu hawezi weka kielelezo cha kufanywa mtandaoni bila kuwa na uhakika wa matokeo (mtoto), ndiyo maana anapojifungua ndipo anaweka picha ya mimba!..

LOGIC 2. Ukimtembelea mgonjwa aliye mahututi, ukamsalimia akakwambia yuko fiti kamili gado! Rudi nyumbani kajiandae na mazishi!

Nachotaka kusema ni nini!

Ikiwa kuna taarifa imefichwa, na fununu zikazagaa juu ya uvumi huo! Basi tambua kwamba siku mamlaka ikikubali na kutangaza hadharani ukweli wa taarifa hiyo basi matokeo yake huwa si ya kufurahisha!

Mfano;
Kama uvumi ni ugonjwa, na siri ikafichwa, basi siku taarifa rasmi ikitoka huwa niyakuwaanda watu kisaikolojia kabla ya kutangaza msiba!

Ukweli ukweli ni ukweli; na Uongo uongo huwa ni ukweli Pia!

Lakini Uongo na ukweli matokeo yake huwa ni UONGO!

Hiyo ndo nguvu ya LOGIC
 
Kwenye hili wenye dhamana wamepwaya kiukweli inasikitisha kwa wananchi kumuombea mabaya mtumishi wao namba moja ila wenye dhamana ilitakiwa wasiruhusu kwa kuweka hayana kwamba mh ni mgonjwa ama si mgonjwa kuumwa sio Jambo la siri
Wala kuugua sio aibu Wala sio dhambi.wanyama wote huugua.
 
Wachache sana watakuelewa, ila subiria matusi ya mataga na uvccm.
 
Hata kwenye mathematics hii huwa ipo..Hasi mara hasi siku zote huwa chanya...chanya mara chanya siku zote huwa chanya ila hasi mara chanya huwa hasi,


Logic yako ya kwanza imekuwa ngumu sana kueleweka. Yapili nayo maelzo hayaendani na mfano..kiufupi nimeshindwa kuelewa nguvu ya logic uliyomaanisha iko wapi.
 
Endeleeni kutuwekea reference zitazotumika hapo badae😆
 
Madikteta wengi kuumwa kwao ni kama kushindwa au udhaifu au aibu.
JK alipougua tezi dume alisema mzee wa watu na taifa likawa nae bega kwa bega.
Na alisababisha watu wengi wasiionee aibu tezi dume. Nakumbuka aliporudi tu, alifanya press na wanahabari na wazee wa DSM na alijibu maswali . Hii imeperekea wananchi wengi kutokuionea haya TEZI DUME
 
Endelea bila kuchoka kumuombea rais wetu, huku ukiamini kua ni mzima na anachapa kazi na wewe chapa kazi. Kama unahitaji kumuona andika barua ya ombi hilo toa sababu kwanini unataka kumuona rais itume kwa ofisi ya rais makao makuu Dodoma. ikionekana kuna umuhimu utatengewa muda ukamuone. rais yupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. nikutakie majukumu mema.
 
Kimya kingi kina mshindo mkuu. Mazoea ya kumweka kwenye luninga kila siku yameleta haya.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…