Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Nchi imepigwa ganzi huku tetesi mbaya zikiendelea. Wenye dhamana ya usalama wa mh Rais kwanini mnaacha inafikia huku?

Mambo hayaendi hadi viboko? Tujulisheni hata kama kweli anaumwa tumwombee mpendwa wetu.
Kuna sababu za kutotangaza hata kama anaumwa.

Yeye mwenyewe alishajiweka kwenye kona ambayo watumishi wake hawawezi kumwondoa hapo.

Alishajitangazia kuwa 'mungu' ndiye mlinzi wake mkubwa, kiasi kwamba akisikika akisema anaumwa, watu wataanza kuhoji kama "imani" yake kwa mungu wake imepungua.

Maana yake ni kwamba, yeye hawezi kuugua kwa sababu imani yake kwa mungu ni kubwa.

Na hasa kama ugonjwa wenyewe unaohusika ni corona, wafuasi wake wataanzia wapi kutangaza (kujulisha) kwamba na yeye "kaugonjwa kadogo haka ka kishetani" kanaweza hata yeye kumweka kitandani? Hiyo itakuwa ni aibu kubwa asiyoweza kuivumilia.

"HOFU ni ugonjwa mbaya zaidi ya ugonjwa wenyewe", yaani hataki kuwatia HOFU waTanzania kusikia kwamba haka ka corona kanaweza kumweka kitandani hata yeye mwenye mabunduki na mabomu yote ya machozi.

Ataanzia wapi sasa kuanza kuwahimiza wananchi wavae barakoa, huku akiwatishia wasaidizi wake wasizivae mbele yake! Kukubali kuwa anaumwa ni kuutangazia umma wa waTanzania kwamba kiongozi wao ni mwongo.

Aumwe? Dawa zote zile zilizogunduliwa na wataalam wake, ikiwa ni pamoja na kujifukiza zitakuwa zimeshindwa kumkinga yeye? Itakuwaje kwa makapuku raia zake anaowahimiza wazitumie hizo dawa na waachane na zile za mabeberu wanaotafuta kutuibia utajiri wetu!

Kwa hiyo, kuna sababu lukuki zinazozuia isitangazwe kuwa mkuu wa nchi anaumwa, hata kama ni kweli alikuwa anaumwa.

Labda useme kwamba anaweza yeye mwenyewe, akishapona vizuri kuutangazia umma wa waTanzania kwamba ameushinda huo ugonjwa kwa kutumia dawa ya Bupiji, kujifukiza na njia nyingine anazoziamini yeye.

Hii itakuwa njia nzuri ya kujitangazia ushindi katika anayoyaamini yeye; na bila shaka atajizolea sifa nyingi na kuwapata wafuasi wengi katika imani yake hiyo.

Na kama itakuwa hivyo, tujiandae kwa jeshi lake lililopo humu JF; maana ukumbi mzima utakuwa ni wa kwao.

Na kwa wale wengine wetu; kama ikidhihirika kuwa ni corona ndiyo ilikuwa imemnyamazisha..., tutashukuru kwamba Mungu amamlinda kiongozi wetu, lakini pia tutaridhika kwamba angalau amepata uzoefu wa kuonja joto ya jiwe ya Corona. Hatukumtakia imuue, lakini fundisho atakuwa amelipata hata kama ataendelea kushupaza shingo kwa sababu ya kuona AIBU kwa msimamo wake uliomfikisha huko.
 
Kusema Corona haipo wakati ipo ni sawa na kumchezea Mungu. Hatuwezi kuwa wabishi wa kidini kuliko hata ma sheikh, mapadre na wachungaji tueshimu Mungu na sayansi.

Tumesema fanyeni chanjo! Sifa zitawauwa
 
Tumuombee apone haraka kama anaumwa pia tofauti za kisiasa zisifike kwenye mambo ya afya.
Hapana.

Kwa kukosa faraja toka kwake wananchi wake yanapowapata mabaya; sio vibaya sana kumtakia na yeye yampate ( mradi asife).

Pengine uzoefu huo utamgeuza moyo kuwa wa ubinaadam zaidi kuliko alivyo sasa.
 
What you need to know:

Multiple sources confirmed that the leader who has reportedly been ailing since late last month.

The country has recently softened its stance on the pandemic.

The leader of an African country who has not appeared in public for nearly two weeks is admitted to Nairobi Hospital for Covid-19 treatment, even as his government remains mum on his whereabouts.

The leader, who regularly addresses church congregants and public rallies when inspecting or launching government projects, was last seen in public on February 27.

The Nation cannot disclose his name as officials from both governments declined to officially confirm his admission to Nairobi Hospital, citing diplomatic protocol.

Multiple sources, however, confirmed that the leader who has reportedly been ailing since late last month, flew to Kenya on Monday when his health deteriorated.

Tens of senior government officials and religious leaders in the country have died from suspected Covid-19 infections in recent weeks.

Last public appearance

While addressing a gathering in one of his last public appearances, the leader advised his citizens to take precautions against the Covid-19 pandemic.

His government has, however, remained adamant against enforcing public health measures such as wearing face masks, sanitising and banning of large gatherings.

Opposition leaders who spoke to the Nation said diplomatic sources had indicated that the leader has been on a ventilator.

They chided government officials for holding onto information on the leader’s whereabouts and health.

Account of infections

There has been no official information from the government on whether the leader is unwell or merely taking a break.

His government faced a lot of criticism over the way it handled the Covid-19 pandemic in since its onset early last year.

Unlike most countries across the world including Kenya and the rest in the continent, the country did not go into lockdown to slow down transmissions.
Health officials in that country do not give a daily account of infections.

It has also refused to tap into the supply of Covid-19 vaccines, arguing that the drugs need to be verified by local scientists and health experts first.

Mass hysteria

In recent weeks, however, the country has softened its stance on the pandemic, its top officials arguing that it was managing mass hysteria, rather than denying the existence of the Covid-19 pandemic.

The change of tune came after the clergy mounted pressure for more disclosures about Covid-19 and measures to be put in place to stop its spread.

The Catholic Church in the Africa country recently said its top clerics had died from ailments with symptoms similar to those of Covid-19.

It then distributed guidelines to bishops of various dioceses on measures to protect themselves against Covid-19 while conducting mass, weddings, prayers and other services.

The World Health Organization has also repeatedly pressed the country to disclose its Covid-19 infection numbers and issue public warnings against the deadly virus.
 
Mike sonko na Raila odinga pia wamelazwa nairobi hospital kama sikosei ndiyo hospital aliyokuwa amelazwa Tundu lissu

Kwa kawaida Kenya wanahabari huwa hawafichwi habari za kiongozi kuumwa.
Hawana utamaduni huo maana wanafahamu binadamu kuumwa ni jambo la kawaida na hakuna haja kujificha.

Mfano habari hizi toka kumbukumbu za media za waKenya


February 9 , 2021

Mike Sonko alilazwa hospitali February 9, 2021



July 2020
Odinga in Dubai for treatment
Mombasa Governor Hassan Joho and Suna East MP Junet Mohamed on Thursday July 2020 left for Dubai to see ODM leader Raila Odinga. In pictures shared on Twitter, the two were seen in a lavish private jet as they sat side by side with snacks and fruits in front of them
 
Taratibu si unajua hata Baba wa Taifa tuliishia kuambiwa hali yake Ni mbaya kwa miezi kadhaa.

Hali ya Mjomba wa Taifa hopefully Ni nzuri. Tumuombee!
 
Watanzania tunapenda sana umbea kuliko kazi...tupe picha caption tutaweka wenyewe...tupe title tu script tutaandika wenyewe...

Uwongo always hupanda lift na kuwahi kufika, bali ukweli kupanda ngazi na kuchelewa kufika coz human being prefer bad news over good news.

Tupo hapa tuna speculate na tutaendelea ku speculate mpaka pale ukweli utakapo tufikia.

Its up to the people who knows the truth to either come forward au wakae kimya wakituangalia tukihangaika na urongo.
 
Kweli Magufuli anaweza kwenda kutibiwa Kenya?! Si watammaliza hata kama ugonjwa wake ungetibika?!
Nawe umetoa wazo la kufikirisha.

Kwa kweli litakuwa jambo la kushangaza kama kweli sehemu pekee ya kumpeleka ni huko.

Ikitokea kuwa hivyo, basi kuna mengi tutakayoyasikia huko mbele za safari.
 
Wapinzani wa bongo raha sana,ukiwakuta wanavyolalamika sasa mara sijui wanauliwa mara vile mara vile. Ila hao watu wenyewe sasa wanaolalamika ndio kwanza wapo busy kuzushia watu maradhi na vifo yani ndio mambo ya msingi kwao.
Wamezuiwa kufanya wichotakiwa kukifanya.
 
Hizi tetesi zlianzia kwa Lissu Tundu...ambaye ni alwatan hospitali za Nairobi,anao marafiki wengi fani ya afya.... Baadaye ghafla wakasitisha bidhaa za shamba(mahindi) kuingia Kenya kupitia boda moja ya Namanga(ambayo ni karibu na Nairobi)...amri iliyokiuka taratibu nyingi za diplomacy... Bwashe akawaka..baadaye kimya...shigella naye akajidai na ya kwake,kuwa yeye kama rais wa mkoa...mambo yako shwari(??rais wa Arusha hajui kazi)...kimya kikafuata..
Ni imani hizi ni tetesi,kama ilivyo kwa yule DC...,hata wakati ule wa moshi wa ajabu... Daima tumwombee Afya njema Kiongozi wetu mkuu
 
""Nililisema hili hata wakati wa zile tetesi nyingine wakati ule. Rais ni mwanadamu, hata Kama wakati mwingine anazungumza kama mwenye ufunguo wa mbinguni""
 
Ndoto Niliyoota Leo.

Kiongozi wetu Mkuu wa Nchi alikuwa kwenye ukumbi fulani akigawa Zawadi kwa Watu mbalimbali.
Akatoa tangazo kuwa pamoja na Yeye kuwapa Hao watu Zawadi kutokana na utumishi wao, hata yeye alistahili Zawadi lakini ameamua kutupatia watanzania Wote Zawadi!

Zikaandaliwa Ngoma Kadhaa na Kisha Mkuu akachukua vijiti na kuanzia kutoa Burudani kwa kupiga Ngoma huku akicheza.

Katika kuonyesha uzoefu wa kucheza alitoa ile staili ya kuruka na kutua na makalio/matako ile anatua chini hakunyanyuka. Ndipo wakaanza kumuita lakini hakuitika, shika hapa na pale lakini hashtuki! Ikabidi wambebe kumtoa nje nadhani kumpeleka hospital. Na Nikashtuka Usingizini.

Ninakemea Roho Ya Mauti kea Viongozi wa Nchi Yetu. Na ikitokea Bwana umewaita, wajalie Kifo Chema. Ila si nipendavyo mimi bali upendavyo wewe.
Mapenzi Yako yatimizwe.

Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu. Amina.
 
Sijazisikia ila lisemwalo lipo na kama halipo limjiani linakuja. Sasa sijajuwa wala kuelewa ni tetesi gani ,ila kila nikikaa naona kuna tetesi,kama unazielewa tuambie.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…