Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Nani alijua kuwa Maalim Seif Sharif amepelekwa Muhimbili ,ila alipofariki siri zote zikatoka,ila nakumbuka tu yule Kigwogwo ndie alievujisha kuwa yupo huko. Na Hili twamsubiri kigogo azidi kupanda chati
Ila Magu akija juu basi amfukuze msemaji wa serikali hafai hata kuwekwa bawabu.
Kwanini Msemaji wa Serikali asijitokeze hadharani kuondoa wingu hili? Hivi wanaona ni sawa tu Mkuu wa nchi kufanyiwa haya yote? Wanaharibu taswira ya nchi na huyu mtu binafsi. Wameshindwa kuwajibika kutetea taswira ya mkuu wa nchi wakati ndio jukumu lao kubwa kwa Taifa. Hata Usalama wa Serikali wanapaswa kuingilia kati hili suala maana limevuka mipaka ya utu wa Mtu. Kama walitaka kupima upepo kuona Mzee anaonekanaje mbele ya jamii wameshaona tayari. Vinginevyo basi nao ni vilaza.
 
Ndugu kwa sasa tuache chuki, Tumuombee muheshimiwa Rais huko aliko,

Uwezekano wa kuwa mgonjwa upo, naye ni binadamu kama sisi.

Ila na wana ccm nao waache kushangilia mateso wanayo yapata chadema

Tulipo fika siyo kabisa, sijawahi kuona taifa ambalo lina watu wengi wanafurahia kiongozi wao akipata majanga.

Watanzania tupendane

Umwombee kwa lipi, umeambiwa lini na nani kuwa anaumwa?

Acha uzushi wewe utaleta taharuki.
 
Mkoa unaongoza kumchukia magufuli ni watu watu arusha, ikifuatiwa na Mbeya.

Ni wale watu waliozoea kitonga mteremko madili yapigwe serikalini wao watereze tu Sasa mkulu kawabana Kila mtu ale kwa jasho lake halali.

Hivi hamjiulizi Kama kweli magu yupo india mbona viongozi wakubwa wote wapo nchini jafo .mh.waziri mkuu.

Madua yenu ya kipuuzi yatawarudia nyie wenyewe endeleeni kuomba upumbavu.
 
Pamoja na yote hayo. Umepata picha gani ya jamii kwa huyu jamaa yako aliye kwenye mfungo wa Kwaresma? Uwe mkweli toka rohoni. Lengo ni kurekebisha palipobomoka.
 
Mbona huko Mbeya na Arusha hakuna hata mbunge wa upinzani na mzee alizoa kura za kutosha. Unasemaje watu hao hao waliompa kura za kutosha yeye, wabunge na madiwani wake?
 
Hili linaloendelaea sasa linatotakana na ujinga na uzushi ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu ukiachwa kwa kisingizio kuwa ni uzalendo.

Musiba,huyu ameumiza watu wengi sana kwa habari za uongo,lakini hashikiki kwa sababu kuna watu wanafurahishwa na anayoyafanya.

Ushangiliaji huu kama Taifa tunapaswa kutafakari kwa nini sasa?

(1)Wazushi wa hizi habari wana faida gani?

(2)Kwa nini vigelegele?

(3)Kwa nini vitisho na si majibu?

Ewe Mtanzania ni vyema kujua serikali ipo kazini.si vizuri kucheza kila ngoma.
 
Ila kwa kweli pamoja na kwamba siyo vizuri kumuombea mabaya mwenzako lakini utawala huu ujitafakari ni kwa nini unachukiwa kiasi hiki? Kuna nini? Mawaziri wakiugua wananchi wanafurahi, sasa uvumi tu wa mzee kuumwa imekuwa sherehe kila kona. Kuna nini? Something is wrong somewhere. Akina JK, Msekwa, Mwinyi, Bujiku, Mangula, N.k muyaone haya na kushauri ipasavyo
 
Ndugu kwa sasa tuache chuki, Tumuombee muheshimiwa Rais huko aliko,

Uwezekano wa kuwa mgonjwa upo, naye ni binadamu kama sisi.

Ila na wana ccm nao waache kushangilia mateso wanayo yapata chadema

Tulipo fika siyo kabisa, sijawahi kuona taifa ambalo lina watu wengi wanafurahia kiongozi wao akipata majanga.

Watanzania tupendane
wewe huzuiwi na mtu kumwombea mabaya rais.maana ndipo ilipo amani ya moyo wako.

lakini Mungu hafanyii kazi matakwa ya mtu mmoja kwa hatina ya wengi.

rais ni mzima wa afya tele.
 
Hili linaloendelaea sasa linatotakana na ujinga na uzushi ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu ukiachwa kwa kisingizio kuwa ni uzalendo.

Musiba,huyu ameumiza watu wengi sana kwa habari za uongo,lakini hashikiki kwa sababu kuna watu wanafurahishwa na anayoyafanya...
Matabaka yamejengwa wa wapinzani njaa kwa sababu tu wanayataka madaraka na ukweli ni kuwa hawatayapata.
 
"According to Tanzania’s constitution, Vice President Samia Suluhu Hassan would take over for the rest of the five-year term if the president is unable to discharge duties"

But is it possible?
 
Alianza huyo mgonjwa, wakati akisema hapeleki maendeleo kwa wasio wake, unafikiria madhara yangekuwa nini?

Hili linaloendelaea sasa linatotakana na ujinga na uzushi ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu ukiachwa kwa kisingizio kuwa ni uzalendo.

Musiba,huyu ameumiza watu wengi sana kwa habari za uongo,lakini hashikiki kwa sababu kuna watu wanafurahishwa na anayoyafanya.

Ushangiliaji huu kama Taifa tunapaswa kutafakari kwa nini sasa?

(1)Wazushi wa hizi habari wana faida gani?

(2)Kwa nini vigelegele?

(3)Kwa nini vitisho na si majibu?

Ewe Mtanzania ni vyema kujua serikali ipo kazini.si vizuri kucheza kila ngoma.
 
Ndoto za abunuwasi
"According to Tanzania’s constitution, Vice President Samia Suluhu Hassan would take over for the rest of the five-year term if the president is unable to discharge duties"

But is possible?
 
"According to Tanzania’s constitution, Vice President Samia Suluhu Hassan would take over for the rest of the five-year term if the president is unable to discharge duties"

But is possible?
Ungeweka na vifungu vya sheria
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom