Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Ukiona ndani ya jamii uliyomo ukipata matatizo wanasherehekea jiulize mara mbili mbili kuna nini? kwa uzoefu wangu wa miaka hii 70 niliyonayo viongozi wetu wa awamu hii wakipatwa na janga lolote wananchi wanashangilia. Kuna nini?
Hayo ni matatizo ya watu wachache wasiokubali kuwajibika kwa magumu wanayokutana nayo. Husukumia wajibu wao kwa watu wengine hasa viongozi wakuu!! Mtu ana maisha magumu badala ya kutafuta namna ya kukabiliana nayo anaona wengine ndio wanaohusika kusababisha ugumu huo! Watu wa jinsi hiyo huwa hawatoboi katika maisha! Mpaka anazeeka huwa hafanikiwi!
 
Duh, nimepitwa na jambo kubwa kama hili, pole sana wana CCM kwa kuuguliwa iwe ni kwlei au uongo.

Ugonjwa ni jambo la kawaida kikubwa tuombeane heri tu, msikimbilie kununua majogoo kwa ajili ya sherehe kwanza, tuombeane ndio uungwana, muda ukifika pilau italiwa tu iwe ni kwako au kwake. Kikubwa watoke waseme ni wapi alipo.

MUNGU mbariki John Joseph Magufuli apone (kama anaumwa). Sisi ni wa MUNGU tuombeane heri
 
Taarifa ni jambo jema sana kuliko kukaa kimya.
Tupo tunaompenda Rais wetu, tungeanza maombi rasmi kwa ajili yake ili Mungu amponye haraka.
 
Maneno yako hayafai, hayana adabu wala heshima, yamejaa uongo na sijui ni kwa faida ya nani?
Maneno yapi mkuu, ambayo "hayafai, hayana adabu wala heshima, yamejaa uongo..."?

Ningeyaona ningeyatetea maneno hayo yaliyokufanya uandike hivyo.
Kipimo chako cha adabu, heshima, pengine sio kile kinachotumiwa na watu wote.

Kwa hiyo usijione wewe kuwa ndiye mpima adabu na heshima.
 
mwaka jana kuna watu waovu walizusha maneno kama haya na kusambaziana wakilishana ujinga. wakaja ona aibu baada ya kuja mwona Mh Rais akiendelea na majukumu yake akiwa mzima bu kheri wa afya. wakaona aibu hawakuwa na maneno yoyote ya kuelezea upuuzi waliofanya.

mwaka huu tena watu wamezusha maneno hayo na kwa kuwa watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri wanabeba bango kama hilo bila kurudi nyuma kufikiria kipindi kile wanaambiwa ameenda tibiwa ujerumani then akajitokeza katika majukumu yake ya kitaifa walipewa ufafanuzi gani na wazushi. leo wanadanganyika tena kipumbavuh kabisa na kuanza bebelea maneno ambayo hawana uhakika nao.

rais yupo salama ameamua ku chill tu si lazima kila wakati aonekane. na mnasahau kuwa wakati mwingine huwa mnalalamika kuwa rais anaonekana sana.kila sehemu yeye yupo na kila siku anataka yeye awe ndo habari ya nchi. akiamua kutulia kuwaacha ninyi muwe habari ya nchi mnakosa la kuongea zaidi ya kumzushia kuwa yu mgonjwa. wakati kumbe mngetumia nafasi hii vizuri kuonekana kwenye vyombo vya habari na kumfunika. matokeo yake tena anapotaka yeye kuwa kimya ninyi mnamfanya yeye ndo mada kuu.

kesho akionekana mzima mtasemaje? kapona kwa miujiza? maana kwa ujinga huu safari hii mmeamua mseme kaenda tibiwa hapo karibu tu Nairobi Kenya. sababu mnajua mkisema tena Ujerumani akajitokeza mtambuka vibaya.

hii tabia ikome. tujadilini mambo ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
 
Hayo ni matatizo ya watu wachache wasiokubali kuwajibika kwa magumu oaks wanayokutana nayo. Husukumia wajibu wao kwa watu wengine hasa viongozi wakuu!! Mtu ana maisha magumu badala ya kutafuta namna ya kukabiliana nayo anaona wengine ndio wanaohusika kusababisha ugumu huo! Watu wa jinsi hiyo huwa hawatoboi katika maisha! Mpaka anazeeka huwa hafanikiwi!
Kwani wakati wa utawala wa wenzake maisha yalikuwa rahisi? Mbona kwa mfano mimi kwa sasa nipo nafuu kiuchumi kuliko utawala wowote wa nchi yetu ila jamaa hapana! Kwangu mtu asiyejali utu wa mwingine simkubali hata akitununulia Noah sisi wote.

Utu kwanza, vitu baadaye. Haiwezekani unaamuru watu wampige risasi binadamu mwenzako kisa siasa. Haiwezekani watu wanaokotwa kwenye viroba wewe unachekelea tu. Waandishi wa habari za uchunguzi wanatekwa na kupotezwa mchana kweupe wewe meno nje tu.

Haiwezekani! Kazi kuwapandikiza vibaraka eti wadai uongezewe muda wa kutawala ili ufanye nini cha ziada? Unawakemea hadi viongozi wa dini wanaohamasisha watu kuchukua tahadhari ya magonjwa ya kushindwa kupumua, unawazodoa watumishi waliochukua tahadhari ya afya zao na za wengine kwa kuvaa barakoa. Wewe nani?
 
Tuombeane mema ndugu
zanguni,haijalishi tunayo
mengi kiasi gani mioyoni.
Mungu ibariki Tanzania,
Tubariki watoto wa TZ.
 
Hayo ni matatizo ya watu wachache wasiokubali kuwajibika kwa magumu wanayokutana nayo. Husukumia wajibu wao kwa watu wengine hasa viongozi wakuu!! Mtu ana maisha magumu badala ya kutafuta namna ya kukabiliana nayo anaona wengine ndio wanaohusika kusababisha ugumu huo! Watu wa jinsi hiyo huwa hawatoboi katika maisha! Mpaka anazeeka huwa hafanikiwi!
Kweli kabisa ndugu,inashangaza sana
 
Wabongo kwa speculation hamjambo jiwe yuko fit anaendelea na kazi za ujenzi wa taifa rais sio kama kina diamond awe anauza sura kila siku kwenye media nae anahitaji privacy afanye mambo kwa utulivu usikute yuko mahali kuna pisi anaichakata
Rais hana privacy halafu hizo kazi anapigia uvunguni?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom