Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Ohoo, hivi mtu akikwambia kutembea na mwanafunzi kutakufanya uende jela miaka 30 anakua amekutisha sio?
Mfano wako sio sahihi, unatumia lugha kama una mamlaka ya kufanya au kutekeleza hayo unayoyaandika humu. Hakuna mtoto mdogo humu na ni vyema ukatumia lugha ya kukumbushia na sio mikwara mbuzi unayoleta.
 
USICHOFAHAMU NI KWAMBA PALE NAIROBI HOSPITAL LISSU NI KAMA NYUMBANI KWAO KULE KIJIJINI SINGIDA, HIVYO INATARAJIWA ANA VYANZO VINGI KUHUSU HILI ANALOLIZUNGUMZA. VYOMBO VYA HABARI VIKUBWA KAMA REUTERS, TELEGRAPH, BBC, THE GUARDIAN (UK) SIO WAPUUZI KUMFANYA SOURCE. LAKINI JAMBO KUBWA KABISA BADALA YA KUMSHAMBULIA LISSU KWANINI USIPIGE KELELE SERIKALI YETU ITUELEZE RAIS WETU KIPENZI YUKO WAPI MAANA NI HAKI YETU KUJUA!

Hao kina guardian, bbc unaowasifia ni wadaku kama wadaku wengine. Juzi juzi, rais wa N.korea alivyokuwa kimya kajichimbia, wakaanza uzushi kama kawaida yao. Baadaye wakaumbuka. Halafu siyo hilo tu. Wameumbuka mambo kibao, wakaanza kuomba msamaha.
 
Mfano wako sio sahihi, unatumia lugha kama una mamlaka ya kufanya au kutekeleza hayo unayoyaandika humu. Hakuna mtoto mdogo humu na ni vyema ukatumia lugha ya kukumbushia na sio mikwara mbuzi unayoleta.
Sio kila lugha usiyoipenda ni mkwala mbuzi zingne ni elimu.
 
Wasalaam

Limejitokeza wimbi la taarifa za mtaani kuwa kiongozi wetu mkuu wa nchi anaumwa hizi taarifa hazijathibitishwa na serikali wala hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyekanusha wala Taifa halijapata public notes/official statement kutoka mamlaka husika kuwa kiongozi wa nchi haumwi.

Mh.kutokuoneka wiki ya pili kwenda ya tatu sasa ndo kunatoa ukakasi kwamba huenda ni kweli kiongozi wetu anaumwa ,ila zinatumika nguvu nyingi huku mtandaoni kuaminisha umma kuwa kiongozi huyo sio lazima aonekane kanisani kwa sababu sio paroko,sio lazima aongee ongee kwa sababu yeye sio msemaji wa club kama Manara,sio paroko kwamba amepangiwa misa aende kubuhiri,sio sio sio zimekuwa nyingi.

Katika jambo ambalo kiongozi kwa sisi tunaomjua asingenyemaza kimya ni hili la mahindi kuzuiliwa mpakani Mh.Rais ni binadamu ,kama walivyo binadamu wengine wa kawaida , binadamu anaziliwa,anaishi ,anaugua,anakufa pia.

Kama ilivyo kawaida yake Mh.Rais ni mtu anaependa kuonekana hadharani kila mara,lakini awamu hii ya amependa kukaa kimya akiwa ofisni hilo kwetu sisi wananchi halitupi tabu sana.

Kwa nini sasa Mawaziri,wabunge na baadhi ya wateule wake watumie nguvu kumsifia na kupost kwenye mitandao kama vile wanamuombea afya njema na kumtia nguvu kipindi ambacho ndo kuna sintofahamu ya alipo rafiki yetu huyu Mh.Rais ,je kufanya hivo si ndo kuleta taharuki zaidi mtaani na maswali lukuki ya kujiuliza.

Makamu wa Rais wa zamani wa serikali ya Zanzibar Mh. Sharif alivyougua tuliambiwa hadi umauti unamkuta sio chama chake sio serikali ya Zanzibar ilikanusha.

Mwalimu Nyerere alipougua kansa ya damu na kwenda kutibiwa Uingereza tulijulishwa.

Mkapa alipoenda Uswiswi kutibiwa nyongwa tulijulishwa. Kikwete alivyougua tezi dume na kwenda Marekani kutibiwa tezi dume tulijulishwa sio hao tu kuna maraisi Africa wamekua wakienda kutibiwa Ulaya dunia inajulishwa pia TANZANIA yetu kigugumizi kinatoka wapi kwani Rais kuugua ni dhambi ?

Ni vizuri kuacha uvumi wa mtandaoni na serikali ije ikanushe jambo hili kuwa Rais haumwi yupo zake IKULU magogoni au CHAMWINO, sio kila waziri ana tweet au ana post kwenye mitandao yake hovyo hovyo na kuongeza taharuki kwa wananchi

Taharuki yoyote inayogusu maisha na afya ya namba moja lazima ijibiwe na mamlaka husika.

CCM na baadhi ya wateule wa Rais ,acheni kupost post hovyo hovyo mtandoni kana kwamba hamna akili
(Jokate,Mwana FA,Babu Tale,mliofanya ni utoto na ujinga kwenye mitandao yenu).

Rais wetu kama upo ofisini jitokeze tukuone tumekuzoea
Mh.Rais kama unaumwa pia tujulishwe ili tuzidishe maombi upone haraka urudi katika hali yako ya kawaida.

Ijumaa Kareem
Huyu alishajipa umungu mtu na wateule wake wanaamini ni mungu hivyo hawezi kuugua.The only thing najua,Kama kweli amepata covid- 19 kwa umri wake na afya aliyonayo- kufa ni lazima,let's wait labda watazika kimya kimya au watakaa na maiti hadi 2025
 
..Nadhani Gerson Msigwa anapwaya.

..Yule dogo ni MC zaidi, siyo mwandishi wa habari anayeweza ku-manage masuala ya Ikulu na Raisi.
Kwenye hiyo Serikali Nani anatumia ubongo wake kufanya kazi wote wanasubiri maelekezo ndio maana wanaweka mpaka clip za miaka iliyopita

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Huyu alishajipa umungu mtu na wateule wake wanaamini ni mungu hivyo hawezi kuugua.The only thing najua,Kama kweli amepata covid- 19 kwa umri wake na afya aliyonayo- kufa ni lazima,let's wait labda watazika kimya kimya au watakaa na maiti hadi 2025
Alijipa u mungu mtu mpaka kufikia mchakato wa mitano tena. Kweli tumeuona uwezo wake Bwana.
 
..kama bwana mkubwa ni mgonjwa, na hawezi kutimiza majukumu yake, they have to tell the nation.

..tena Ikulu wakiwa wametangulia kutoa taarifa kunakuwa hakuna uwezekano wa watakaofuata kuzusha uongo.

..na kama bwana mkubwa sio mgonjwa walitakiwa wakanushe haraka kwa ushahidi usioweza kutiliwa mashaka.

..but Gerson Msigwa has done none of that. Na ndio maana nasema huyu bwana mdogo ni mwepesi. Nafasi yake inahitaji mwandishi mbobezi anayejua dhima ya kuwa muandishi wa habari wa Raisi na Ikulu.

cc Nyani Ngabu, Nguruvi3, Richard
Tangu Serikali ya Magufuli iingie madarakani Nani anatumia ubongo wake wote wanatumia wa Magufuli

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Wasaidizi wa rais wakitumia uoga inaweza kuzua balaa kubwa na tharuki kubwa kutokea
 
It’s impossible

Sky hahahaha ata kama unachuki wewe imezidi sasa ndugu yangu. Kwa kua una uhakika na taharifa na ushatoa hiyo taharifa kwa nini usitulie usubilie watangaze mama yangu khaaa. Kifo ni fumbo la imani.
 
Huyu mtu ni mwanasayansi, aliskia, aliona, kasoma kila kitu. Je kipi kimempa kiburi kiasi cha kudharau mambo wazi kama haya? Why clever (learned) and intelligent) people like Magu believe stupid things? Kwamba corona ikikupata utapona kwa sala??
Hakuwa anafikiria kinachokuja baadae, ni mzuri wa kusolve immediate issues. Ule uchaguzi hakuangalia kuwa bila wabunge wa ipinzani itakua issue.

Kwenye Covid aliwaza kuokoa pesa. This is what came next.
 
Upinzani wako ni wa kipumbavu sana na utakufa wewe kabla yake
1615525618230.png
 

Lissu asema Magufuli amehamishiwa India akiugua Covid-19​

Na Iddi Ssessanga
Kiongozi mkuu wa upinzani Tanzania, Tundu Lissu, amesema Alhamisi kuwa rais John Magufuli, ambaye hajaonekana hadharani kwa karibu wiki mbili, yuko India akitibiwa virusi vya corona na kwamba yuko katika hali mbaya.

Tundu Lissu, ambaye alishindwa na Magufuli kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana, ametaja duru za kiafya na usalama kama vyanzo vya taarifa kwamba rais Magufuli amehamishwa kutoka hospitali nchini Kenya na kupelekwa India akiwa hali mahututi - lakini hakutoa ushahidi.
huyu naye aisee.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom