Yusuph Makamba: Tusimfundishe Rais Samia kufanya kazi, hatumtendei haki

Yusuph Makamba: Tusimfundishe Rais Samia kufanya kazi, hatumtendei haki

Hivi kweli nyie watu mlikuwa hamjui kabisaaa kwamba fedha za Serikali zinaibiwa kila siku na karibu kila idara? Yaani mpaka mmeletewa report ya CAG ndio mnakuja kwa kushangaa? Halafu mnataka sijui Katiba Mpya, sijui mfumo! Hizi Sheria zitawasaidiaje ikiwa nyie wenyewe hamuoni wala hamjui kama mlikuwa mnaibiwa!
Bila kusubiri ripoti ya CAG nani kati yetu anaweza kuingia kwenye hizo ofisi zao ili kujua nini kinachoendelea?

Au unataka tupige ramli?!
 
Kumwambia Rais awashughulikie wezi sio kumfundisha kazi, ni kumkumbusha atimize wajibu wake kwasababu anaonekana amelala.

Huyu Makamba anataka Rais aachwe tu aendelee kuwatazama wezi kwasababu inawezekana nae ni mnufaika wa huo wizi kwa namna moja au nyingine.
Ndio msimponze Samia maana alishaambiwa kuwa wazuri hawafi hivyo akae kwa kutulia ili aendelee kubaki kuwa mtu mzuri.
 
Ye ni nani wa kutupangia? Ni haki yake kutoa maoni mzee wetu ila anapitiliza asidhani kuna watu wana hati miliki na nchi hii! Tunajua anahangaika sana kwa sababu ya maslahi yake…..
 
Report ya CAG imewavua nguo baadhi ya Mawaziri na wakuu wa taasisi mbalimbali.
-Taarifa imegusa baadhi ya watoto wa viongozi wa Chama na serikali waliostaafu,
-CAG apewe au aongezewe ulinzi,mafisadi wanajipanga.Asali ni tamu
 
Ni mwaka gani au hawamu ipi walikuwa na rais mbaya nawakajitokeza nakusema kuwa safari hii tumeuvaa.
 
Back
Top Bottom