Zakazakazi: Yanga sio Mabingwa mara 29 na Simba sio Mabingwa mara 22

Kwa hiyo swali langu liko pale pale, timu 3 zilizotoka bara kwenda kushiriki kombe la Muungano, je aliyeshika nafasi ya kwanza katika hao 3 alikuwa anatambulika "Bingwa wa Tanzania Bara" na kupewa kombe au wote 3 walitambulika tu kama wawakilishi wa Tanzania Bara katika Kombe la Muungano?
 
Wa kwanza alikuwa Bingwa wa Tz Bara.
 
changaule
Tate Mkuu
Bila bila

Someni hapo

Kumbe ligi ya muungano ambayo leo hii mnaiona inferior ndio iliyokuwa yenye hadhi kuliko ligi zetu na mmetulia tu
Nililisema hili toka mwanzo. Na pia huu mjadala unawahusu wale waliokuwa wanabeza CAF Cup kwa hoja ya kuwa na timu chache au kuwa ya mtoano. Inaonyesha katika vipindi tofauti, hata ligi yetu ilikuwa na mfumo huo.

Huu mjadala sijapata mzuka sana wa kuutafutia data zake maana najua kuna ugumu wa kuzipata hizi mitandaoni hasa mabadiliko ya ligi yaliyokuwa yanatokea. Kwa hiyo I hope hizi taarifa anazotoa ni sahihi na tutaendelea kuzitumia mbele ya safari.

Ingekuwa vizuri akaandika sasa mwaka kwa mwaka na kueleza mfumo gani ulitumia kupata bingwa katika kila mwaka.
 
Notts County ilianzishwa mwaka 1862 kabla hata ya shirikisho.
Kwenye almost every nation ni lazima kuwe na founding members.

Yaani vilabu vilivyopelekea kuanzishwa kwa FA.


Issue ya Notts County FC Bado sio sababu tosha ya kusema msimu wa ligi wa mwaka 1990/91 ulikuwa sawa na Ndondo Cup kwa sababu tu EPL haikuwa imeanzishwa.
 
Sasa kukosa urasmi si ilikuwa sawa na ndondo cup.
 
Itoshe kusema hajui hata anacho hoji,K M.K.M na Malindi zimeingiaje kwenye ligi ya Bara?
 
Aliyeshika nafasi ya kwanza anakuwa bingwa wa ligi husika na pia anapewa na kombe. Zanzibar ilikuwa na ligi yao na bingwa anapewa kombe, alikadharika Tanzania bara kulikuwa na ligi yao na bingwa wa ligi ya Tanzania bara (anayeshika nafasi ya kwanza) anapewa kombe
 
Ukiachana na source ya website ya yanga je kwenye vyanzo vingine vinaonesha mara ngapi?
Yanga nayo imekuja kubadilisha siku za hivi karibuni

Angalia kwenye ule uzi wa mwaka jana tuliokuwa tunabishana, waliandika mara 27 lakini miaka ukiihesabu inafika 22
 
Nimeshuhudia utetezi wa nguvu sana kwenye huu mjadala.

Wengine wameonesha kukubali ligi mbili kuunganishwa na kutaka washindi wa ligi zile za mwanzo kabla hazijaunganishwa waendelee kuhesabiwa ushindi wao

Wakati Simba ilipocheza CAF Cup walisema ambayo saizi ni Caf confederation, walisema ile aliyocheza Simba ni Abiora kwakua CAF Confederation Cup imeanza 2004.

Ngoja tuendelee kumsikilizia aje na Makala nyingine huwenda hayo unayoyasema akayaweka
 
Kwanza unatakiwa ujue kuwa ilianza timu ndio ikaja ligi.

Hiyo ni hesabu rahisi sana.

Kasome historia ya Gongowazi kwenye website yao, utaona wameanza lini na hicho kipindi walikuwa wanacheza michuano gani ambayo ni rasmi.
 
Itoshe kusema hajui hata anacho hoji,K M.K.M na Malindi zimeingiaje kwenye ligi ya Bara?
Soma Makala zote wewe nimeweka hapo.

Hiyo ni continuation bado hajamaliza ndio maana kuna maneno "itaendelea"
 
Yanga nayo imekuja kubadilisha siku za hivi karibuni

Angalia kwenye ule uzi wa mwaka jana tuliokuwa tunabishana, waliandika mara 27 lakini miaka ukiihesabu inafika 22
Ishu sio website, hoja iliyopo hapa na ndio uliyowasilisha wewe hapa kupitia Zaka Zakazi ni kwamba Simba na Yanga ni waongo. Tuje kwenye fact ziweke list ya mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara kwanzia ianze ni timu zipi zilizochukua kombe ili tuone kama Simba na Yanga record zao zina uongo. Tatizo mnachanganya mambo Yanga wanajinadi ni kuwa ni mabingwa wa ligi kuu bara mara 29. Elewa neno "Tanzania bara"
 
Caf cup ni tofaut na caf confederation hilo tumeshalieliza sana tena kwa mifano halisi. Africa cup winner's cup ndio ilikuwa ni sawasawa na caf confederation cup na ndio maana mshindi wa Africa cup winner's cup alikuwa akicheza caf super cup dhidi ya mahindi wa Africa cup of champions club. Mbona lipo wazi hilo, hili swala halifanani na hoja uliyomuwakilisha Zaka Zakazi.
 
Fact kupitia chanzo kipi ambacho tunapswa kukubaliana tangu mwanzo?

Mi hapa ndio napoliona tatizo lilipo
 
Yanga bingwa mara 29..

Ifuatayo ni miaka ambayo yanga alichukua ubingwa.

1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985,1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2021–22, 2022–23

Sources; Mzee Juma Rasheed kibaigwa wa Malindi.
 
CAF cup sio confederation mshindi wa hilo kombe alicheza super cup 1994?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…