Zanzibar 2020 Zanzibar: Hali ilivyo mapokezi ya Mgombea Urais Kupitia ACT- Wazalendo, Maalim Seif na Bernard Membe. Ni Mafuriko

Unyama, ukatili, ushenzi na uhayawani wa wazi uliokuwa unafanyika kwenye chaguzi za marudio kila mtu alijionea. Hao mawakala walikuwa wanatishwa na hata kupigwa na jeshi la polisi ili kusaini matokeo fake ya uchaguzi, ndio maana sasa hivi tume ya uchaguzi imekuja na sheria kuwa sio lazima kutoa fomu ya matokeo kwa mawakala. Kama hujui hayo basi uyajue.
 
Hiyo ndio siasa mkuu. Lakini hayo maneno uliyomalizia hapo chini. Nakupinga sana. Ninyi imarisheni chama chenu. Kwenye suala la ulinzi na usalama wa ndani, Tanzania ni mfano wa kuigwa duniani. Tuishie hapo.
 
Maalif Seif akielekea Chama kingine Act nayo itajifia huko Zanzibar, Hao ni wafuasi wa Maalim si wanachama wa Act.
Kwahiyo siku Mungu akimchukua Maalim hao wafuasi wanakuwa wafuasi wa nani?
 
Hiyo ndio siasa mkuu. Lakini hayo maneno uliyomalizia hapo chini. Nakupinga sana. Ninyi imarisheni chama chenu. Kwenye suala la ulinzi na usalama wa ndani, Tanzania ni mfano wa kuigwa duniani. Tuishie hapo.

Ulinzi na usalama wa kuhakikisha ccm ndio wanatangazwa washindi bila ridhaa ya umma?
 
Hiyo mbona iko wazi mkuu?

Lisu hawezi kupata walau 20% ya kura! Tena kama kule zanzibar ndio ataambulia 0 kabisa
 
Siasa ina mambo mengi mkuu. Tatizo cdm imepoteza ushawishi. Ile piiiiiipooosssssss pawaaaaa imepoteza radha miaka ya hivi karibuni.
Huko unaposikia chama cha upinzani kinaongoza kura za urais , sio kazi ndogo mkuu. Chama tawala huwezi kukitoa kwa kuwekeza kwenye mitandao pekee.
 
sasa hiki ndo tunaita chama cha upinzani sio unapungia miti
Umenichekesha sana mkuu. Kua lissu alikua anapungia mkono miti, mwenzake membe huko Zanzibar amepungia mkono maelfu ya watu.
 
Hiyo mbona iko wazi mkuu?

Lisu hawezi kupata walau 20% ya kura! Tena kama kule zanzibar ndio ataambulia 0 kabisa

Ukitaka kuwa rais wa JMT hata usipopata kura moja ya Zanzibar, unakuwa rais bila shida yoyote. Wapiga kura wote wa Zanzibar hawazidi laki 6, huku wapiga kura nchi nzima kama ni kweli kwa mujibu wa tume isiyo huru ya uchaguzi ni 29m+. Lisu hata akipata asilimia 2 acha hiyo 20, hizo zitakuwa ni za halali, kuliko asilimia za ccm za maagizo ya rais.
 
Umenichekesha sana mkuu. Kua lissu alikua anapungia mkono miti, mwenzake membe huko Zanzibar amepungia mkono maelfu ya watu.

lakini tuliwaambia apa chama kikuu saaahv kinatokea ACT ama NCCR wakasema lissu ameangaliwa na mabilion ya watu dunia nzima, madhara yake kaenda kuchukua form hakuna mtu ana ham nae. kabaki kupungia miti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…