Toa mifano hai usitoe mifano mfu ilmradi uhalalishe uporaji wa ardhi ya Tanganyika.
 
Nakumbuka kwenye mijadala ya Bunge la Katiba Mhe. Lissu aliwahi kuongea mazito kuhusu huu Muungano hadi akachukiwa na Watawala.

Kwa kifupi hili Koti la Muungano linatubana Watanzania Bara.

Inakuwaje Nchi ya Zanzibar ambayo iliungana na Tanganyika imiliki eneo la Tanganyika.

Hata kama iliuziwa, lakini sheria ya Ardhi imetoa Umiliki wa Ardhi kwa Taasisi/Mtu binafsi kwa kipindi kisichozidi miaka 99 ingawa kwa sasa imepunguzwa hadi miaka 33.
 
Mkuu acha kutetea ukengeufu. Usitutolee mifano mfu. Serikali ya Zanzibar imeishauza visiwa vyote kwa mabeberu. Kama wana uchungu na ardhi kwanini wauze ardhi yao halafu waje kupora ardhi ya Tanganyika? Kuwa mzalendo kwa taifa lako, acha mawazo ya kitumwa.
 
Ishia hapo hapo. Ukitaka kutuletea mipaka ya kikoloni, Zanzibar yote itaamgukia ndani ya Tanganyika. Bora tu ukae kimya. Usichokoze nyuki ilhali huna uwezo wa kutimua mbio, shauri yako!
 
binafsi sijaona umuhimu wa huu muungano, saa una nunua bidhaa zanzibar ukiingia nazo bara unalipia ushuru kana kwamba ni nchi mbili tofauti hata kama muungano huu upo kwa maswala ya kiusalama bado haileti mantiki, watu wana serikali yao,bunge lao ,kwanini wasiachiwe wajitawale tu kama inchi.
 
Rais wa Tanganyika ni nani. Tuanzie hapo

 
kule visiwani Tanzania bara wanamiliki ardhi gani? tuanzie hapo
 
na sisi ndio hapo tunawapiga za pua. walipe kodi hadi wakome kabisa.
 
Huu ni mfano mmoja wa jinsi katiba ya sasa inavyompa Rais wa Jamhuri mamlaka yasiyo na mipaka katika kufanya maamuzi yoyote. Nimesoma eti hiyo ardhi walipewa na Nyerere ili wafanye mradi wa ranchi. Lakini kama Serikali ya Zanzibar imeshindwa kuitumiq hiyo ardhi kwa malengo ya kuzalisha nyama, kwanini bado waendelee kuimiliki? Kwa kigezo au vigezo gani?
 
na kwanini wapewe ardhi wakati sisi kwao hatupewi ardhi? hivi huu mzigo wa muungano tutautua lini?
 
Hi kitu nlijuaga tokea zamani kuwa ranchi hiyo inamilikiwa na wazenji

Ova
 
Mambo ya ccm hayo kura waibe,ardhi waibe ,uraia waibe hata haki za Watanzania wanaiba kila siku.
CCM wameamua kuuza ardhi yetu wakiwa wamechutama. Wameona wakiuza wima wima tutawashtukia. Itakuwa wamewatumia wazanzibar kuchota ardhi wawauzie mabeberu wagawane fedha. Hizi fedha zitawapeleka watu jehanamu.
 
Yaani kati ya mambo ya ajabu aliyotufanyia Nyerere ni kutuunganisha na hawa viumbe wa ajabu kutoka nchi ya kusadikika. Nyerere tunamheshimu alituletea uhuru lakini kwa hili la muungano wa mchongo, alikosea sana.
Smz kumiliki ardhi huku Tanganyika sio kosa.
 
Sasa si mjitenge au mpaka kwanza mpore ardhi ya Tanganyika, tena kiulani bila kumwaga jasho, ndipo mjitenge? Ukijitenga na Tanganyika una uwezo wa kushindia urojo na madafu au unajitutumua bure kama chura aliyebanwa na mlango?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…