Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
Nimeshangazwa mno kusikia kwamba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imejimegea kipande kikubwa cha ardhi nchini Tanganyika huku serikali ya Tanganyika imekaa kimya. Haiwezekani uvamizi huu ufanyike mchana kweupe kila mtu akiona. Lazima kuna jambo limejificha nyuma ya hili sakata. Inawezekana serikali ya mapinduzi ama inataka kuipindua Tanganyika au imechoshwa na muungano; sasa wanataka kuleta chokochoko ili muungano ufe wagawane mbao. Kufulilah! Lolote liwalo na liwe....kama mbwai iwe mbwai! Wasitutishe.

View attachment 2642276
MAONI YANGU
Tangu zamani mimi niliwaambia kuwa huu muungano wa mchongo hauna maana yoyote hamkunisikia. Kiko wapi sasa, si mnaona wao wenyewe wameanza uchokozi? Moja ya makosa makubwa aliyofanya Nyerere ni kuinganisha Tanganyika na hawa wala urojo.

Kama Zanzibar wanaona nchi yao ni ndogo sasa wanataka kuja kupora ardhi ya Tanganyika ni bora waseme wamegewe mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kisha tuweke mipaka mipya kila nchi iendelee na mambo yake badala ya huu uhuni wanaofanya kupora ardhi ya Tanganyika kinyemela. Inauma sana.
Tuliza mshono Mangi hii ardhi wakipewa tangu awamu ya kwanza kwa minajili ya kuanzisha ranchi ya mifugo kupeleka vitoweo kwao wakati huo hakukuwa na wafanya biashara binafsi.
Ni sawa na mmiliki wa AS Roma kumiliki maelfu ya ekari nchini.
 
Serikali ya China inamiliki ardhi kubwa tu USA kwahiyo sishangai.. umiliki wa ardhi Tanzania si kwa mtu/taasisi yoyote? kama sheria zenu wa kumiliki ardhi ni dhaifu hata Somalia itakuja kununua ardhi huku.
Mambo yote yanaenda kisheria !! Na Mahakama zipo !!
 
Halafu mbona uvamizi umefanyika kipindi hiki? Kuna jambo limejificha nyuma ya pazia. Let us wait and see.
Hapana. RAZABA ipo kitambo sana, nenda Bagamoyo kawaulize wakazi wake ili ujiridhishe.
 
Kusema Zenji eti ni nchi ni sawa na kusema Mkoa wa Pwani ni Daressalaam.
Zanzibar ilikuwa nchi miezi 3 tu hadi siku ya 26 April 1964 zilipofutwa nchi mbili ziwe moja. Mengine ni taarabu tu.
 
Usijiokotee vihoja uchwara unakuja kutujazia uchafu humu JF ili ututoe kwenye reli. Tetea hoja kwa ushahidi kuntu, acha poroja na hadithi za Alfu Lela Ulela. Hazitakusaidia chochote.

Cheki dola ya himaya kubwa ya Zanzibar

1685626152608.png
 
Tanzania ni nchi moja ya JMT, ambapo Zanzibar ni sehemu ya JMT, SMZ na Mzanzibari yoyote yuko huru kumiliki Ardhi huku kwasababu kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki Ardhi.

Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Zanzibar Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Helingoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
P
paragraph ya kwanza umeandika kwa upande mmoja tu hujabalansi habari kama mwandishi nguli ,proffesional.Naomba rudia hiyo paragraph ya kwanza kwa kubalansi pande zote
 
kwanini mnapenda kupotosha habari?hajasema mTanganyika yeyote bali amesema mtu,kikundi au taasisi yeyote....unapata faida gani ukipotosha
kwahiyo mtanganyika anaruhusiwa ila mtu ndio haruhusiwi?
 
Mbona hilo eneo lipo miaka mingi tu. Ukiwa unaelekea bagamoyo sugar pale njiani kuna bango kubwa. Ni maeneo ya tafiti mbali mbali kama sijakosea.

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Heligoland Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Heligoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.

Ni kweli SMZ Ilipewa eneo la Makurunge litumike kama Ranch na Stock Holding point, kwa ajili ya Mifugo inayo safirishwa kutoka Mainland kwenda Z"bar.
 
Tanzania ni nchi moja ya JMT, ambapo Zanzibar ni sehemu ya JMT, SMZ na Mzanzibari yoyote yuko huru kumiliki Ardhi huku kwasababu kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki Ardhi.

Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Zanzibar Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Helingoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
P
je wanamiliki hiyo ardhi kwa utaratibu wa umiliki wa ardhi wa sheria za wizara ya bara , au kwa utaratibu wa sheria za zbar !? kwa sababu kwa sheria za Tanzania hii ya huku kwetu hakuna umiliki wa ardhi ya kudumu ndio maana kila mwaka tunalipia Kodi ya ardhi!! naomba kujuzwa hapo.

Ili tujue mapema Kama ile ardhi siku muungano ukavunjika , hiyo ardhi inakuwa imemegwa moja kwa moja au , inarudi!???
 
Kusema eti Zenji ni nchi ni sawa na kesuma Mkoa wa Pwani ni Daressalaam. lilikuwa pori la waingereza na mwajiriwa wao Sultan waliomtoa Oman hadi mwaka 1964 walipokombolewa na kina Oscar Kambona Waziri wa ulinzi wa Tanganyika.
Ikawa nchi miezi 3 hadi Muungano wa 26 April 64 uliofuta nchi 2 kuwa moja.
Lakini wazee wa vidole juu haiwaishi kusema wao bado ni nchi hadi leo. Taarab tu hio.
 
Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Heligoland Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Heligoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.

Ni kweli SMZ Ilipewa eneo la Makurunge litumike kama Ranch na Stock Holding point, kwa ajili ya Mifugo inayo safirishwa kutoka Mainland kwenda Z"bar.
Juzi juzi mwaka huu tu mmepora kisiwa kimoja mbele ya Dar mkasema ni cha Zanzibar. Hivyo Dar haina bahari. Kilikuwa kinaitwa Fungu Latham sasa mmejifanya kuiita "Fungu Kizimkazi"
 
Nimeshangazwa mno kusikia kwamba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imejimegea kipande kikubwa cha ardhi nchini Tanganyika huku serikali ya Tanganyika imekaa kimya. Haiwezekani uvamizi huu ufanyike mchana kweupe kila mtu akiona. Lazima kuna jambo limejificha nyuma ya hili sakata. Inawezekana serikali ya mapinduzi ama inataka kuipindua Tanganyika au imechoshwa na muungano; sasa wanataka kuleta chokochoko ili muungano ufe wagawane mbao. Kufulilah! Lolote liwalo na liwe....kama mbwai iwe mbwai! Wasitutishe.

View attachment 2642276
MAONI YANGU
Tangu zamani mimi niliwaambia kuwa huu muungano wa mchongo hauna maana yoyote hamkunisikia. Kiko wapi sasa, si mnaona wao wenyewe wameanza uchokozi? Moja ya makosa makubwa aliyofanya Nyerere ni kuinganisha Tanganyika na hawa wala urojo.

Kama Zanzibar wanaona nchi yao ni ndogo sasa wanataka kuja kupora ardhi ya Tanganyika ni bora waseme wamegewe mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kisha tuweke mipaka mipya kila nchi iendelee na mambo yake badala ya huu uhuni wanaofanya kupora ardhi ya Tanganyika kinyemela. Inauma sana.
Hilo shamba tangu 1970s. Cha ajabu nini?🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom