BabuFey
JF-Expert Member
- Feb 13, 2023
- 1,659
- 2,913
Tuliza mshono Mangi hii ardhi wakipewa tangu awamu ya kwanza kwa minajili ya kuanzisha ranchi ya mifugo kupeleka vitoweo kwao wakati huo hakukuwa na wafanya biashara binafsi.Nimeshangazwa mno kusikia kwamba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imejimegea kipande kikubwa cha ardhi nchini Tanganyika huku serikali ya Tanganyika imekaa kimya. Haiwezekani uvamizi huu ufanyike mchana kweupe kila mtu akiona. Lazima kuna jambo limejificha nyuma ya hili sakata. Inawezekana serikali ya mapinduzi ama inataka kuipindua Tanganyika au imechoshwa na muungano; sasa wanataka kuleta chokochoko ili muungano ufe wagawane mbao. Kufulilah! Lolote liwalo na liwe....kama mbwai iwe mbwai! Wasitutishe.
View attachment 2642276
MAONI YANGU
Tangu zamani mimi niliwaambia kuwa huu muungano wa mchongo hauna maana yoyote hamkunisikia. Kiko wapi sasa, si mnaona wao wenyewe wameanza uchokozi? Moja ya makosa makubwa aliyofanya Nyerere ni kuinganisha Tanganyika na hawa wala urojo.
Kama Zanzibar wanaona nchi yao ni ndogo sasa wanataka kuja kupora ardhi ya Tanganyika ni bora waseme wamegewe mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kisha tuweke mipaka mipya kila nchi iendelee na mambo yake badala ya huu uhuni wanaofanya kupora ardhi ya Tanganyika kinyemela. Inauma sana.
Ni sawa na mmiliki wa AS Roma kumiliki maelfu ya ekari nchini.