Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
Basi kama ni hivyo inabidi waachiane hayo maeneo kila mmoja abaki na eneo lililo upande wake!
Tatizo la mipaka yetu ni ukweli kuwa hatukujiwekekea wenyewe ila iliwekwa na watu wenye maslahi yao binafsi. Afrika haikuwa na kitu kwenye mkutano wa Berlin Mkuu.
 
Sishangai, kwa sababu Nchi ina Raia wapumbavu haijawahi tokea, kutwa nzima ni Yanga na Simba unategemea nini? Yaani watu ni Yanga na Simba huku watawala wakiineemeka na keki ya ncni
Na hizo Yanga na Simba zilianzishwa kimkakati ili kuzubaisha Watu.
 
Tanzania ni nchi moja ya JMT, ambapo Zanzibar ni sehemu ya JMT, SMZ na Mzanzibari yoyote yuko huru kumiliki Ardhi huku kwasababu kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki Ardhi.

Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Zanzibar Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Helingoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
P
Kama ZMZ ni sehemu ya JMT inawezaje kumiliki ardhi ambayo yenye ni sehemu mojawapo? Dar es Salaam inawezaje kumiliki ardhi ndani ya Morogoro?
 
Tanzania ni nchi moja ya JMT, ambapo Zanzibar ni sehemu ya JMT, SMZ na Mzanzibari yoyote yuko huru kumiliki Ardhi huku kwasababu kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki Ardhi.

Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Zanzibar Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Helingoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
P
Najisikia vibaya sana nikiona mtu kama wewe ukitupotosha!
RAZABA ( Ranch of Zanzibar in Bagamoyo) ilikuwa ni eneo halali la Tanganyika hadi ilipofika 1977 ambapo Aboud Jumbe (kutokana na udogo wa Zanzibar kieneo) alimuomba Mwalimu Nyerere sehemu ya ardhi ya Tanganyika ili itumike kwa ajili ya mifugo na kilimo na Nyerere alikubali na toka wakati huo eneo hilo limekuwa mali ya SMZ.
 
Biashara ya mchanga wa ujenzi kutoka Tanzania bara kwenda Zanzibar iangaliwe upya.Iwe na uwazi.
 
Km wakenya wapo huko ifakara, kilosa, wanalima bila wasiwasi na kusafirisha mazao Yao mpk Kenya nn cha kushangaza Zanzibar kumiliki hizo hekari. Vijana wa hii nchi wapo usingizini fofofo
Kwaiyo ni sawa ekari 6000 za bagamoyo kuwa sehemu ya Zanzibar?
 
Duuh🙄
Ukifuga pimbi anaota mkia.
Au ni maelekezo kutoka juu?!
Ukute wanatikisa tu kiberiti halafu wanasikilizia!!!
Dawa ni kugeuza Zenji iwe wilaya mojawapo ya mkoa wa Pwani
Kila kitu kina mwisho,ninachoamini hiki kizazi kinachokuja kwa kasi hapa baada ya kizazi cha nyerere na watoto wake kumalizika,hakitaruhusu na kitavunja Muungano,toka nazaliwa sijawahi ona manufaa ya zanzibar kwa mtanganyika ,na hivi hamna uraia pacha kila mtu abaki na nchi yake,na kama mzenji yupo huku achague huku ama kule
 
Kwa sababu wewe sio mzanzibari,
Sio kila mtanzania ni mzanzibari, lakini kila mzanzibari ni mtanzania
Kula kitu kina mwisho,kuna kizazi kitapinga hii kila mtu afe na chake jiandaeni kisaikolojia,Muungano lazima uvunjwe kinachosubiriwa ni kizazi fulani kipite tu
 
Mbona limeibuka kipindi hiki na si wakati uliopita mkapa kikwete magufuli Kuna kitu hakipo sawa
 
Back
Top Bottom