uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 2,085
- 2,996
Kwa muda gani kiongozi? isijekuwa miaka 99, maana hata kiwanja unachokimiliki umekodishwa na serikali lakini tukijenga tunasema nyumba ni zetu.Acha kupotosha Rais Mwinyi alieleza jambo hili in full canera kuwa visiwa vinakodishwa
Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Viongoz washauza kila kitu Kwa sasa wameelekeza akili zao kuuza viwanjwa vya polisi na wakivimaliza vya polisi wata amia maeneo ya Jwtz na magerezaKuanzia miaka hiyo mpk leo na hatujui mkataba ule upoje,wanyama wanapakiwa kwenye ndege huko huko kimya kimya,watanzania tunaendaga kufanya vibarua vya ujenzi mkuu,Pori la Loliondo ni nchi ya muarabu
Mbona kwenye swala la kukopa hwakopi kama nchi Wana tegemea Samia akawakopee aje awagaiye?Fuatilia vizuri juu ya hili mkuu.
Tunasema hivi, Zanzibar ni nchi kamili na ina mamlak na ardhi yake. Tunasema hivyo kwa vitendo na hatusemi kwa maneno maneno tu.
Halafu nikuweke tu sawa, hakuna kipande cha ardhi kinachouzwa. JMT kuna mambo itaiachia Zanzibar ili ifanye inavyoona inafaa kwa Wazanzibari.
Wangefanya siri, usingejua!! Ungeshtukia tu Kisiwa X kinamilikiwa na Elon Musk!!Kama itapotosha, lawama moja kwa moja yaenda kwa serikali kwa kulifanya hili siri kwa Watanzania. Ningetegemea kwanza wangetangaza kwa raia na kutoa ufafanuzi. Pia wangewapa raia wa Tanzania kipa umbele. Sipingi kwa ujumla jambo hili, ingawaje tajriba inaonesha katika ku deal na wenye pesa na nguvu, tahadhari kubwa lazima ichukuliwe (Nyerere hakukosea).
Katiba yetu mbaya sana. Inampa mtu anaeitwa Rais mamlaka za kimungumutu.Kuanzia miaka hiyo mpk leo na hatujui mkataba ule upoje,wanyama wanapakiwa kwenye ndege huko huko kimya kimya,watanzania tunaendaga kufanya vibarua vya ujenzi mkuu,Pori la Loliondo ni nchi ya muarabu
Wewe unajua Zanzibar hakuna vyanzo vingine vya mapato? Je unajua hayo mapato mengine yametumikaje Hadi uhoji haya ya kukodisha visiwa tuu? Ebu tueleze mapato mengine yametumikaje Hadi huoni hayo ya kukodisha visiwa yalivyotumika.Juu ya hayo yote, hizo Fedha walizovuna kwenye biashara hiyo ya visiwa wamezitumia vipi?
Swala la Ardhi sio la Muungano acha wapambane waoZanzibar ni sehemu ya JMT, kwa maana ya kuuzwa kwa kipande cha ardhi ndani ya JMT ina maana gani kwa mamlaka ya JMT?
Je watu wanaonunua visiwa hivyo watatawalwa kwa sheria zipi? za JMT, SMZ, au za nchi zao?
Na ndiyo jiwe akazivunja nyumba Za watu bila wasiwasiKwa muda gani kiongozi? isijekuwa miaka 99, maana hata kiwanja unachokimiliki umekodishwa na serikali lakini tukijenga tunasema nyumba ni zetu.
Uvamizi hauna sheria wala KatibaSwala la Ardhi sio la Muungano acha wapambane wao
Viongoz washauza kila kitu Kwa sasa wameelekeza akili zao kuuza viwanjwa vya polisi na wakivimaliza vya polisi wata amia maeneo ya Jwtz na magereza
Ndiyo katiba ya Mapinduzi ilivyoKatiba yetu mbaya sana. Inampa mtu anaeitwa Rais mamlaka za kimungumutu.
Mbaya zaidi hahojiwi popote awe madarakani au akiwa nje ya madaraka.
KATIBA MBOVU SANA HII
Kuna siku nilichangaia mada fulani kwamba, ikiwa nchi ina viongozi waaminifu na waadilifu, siyo vibaya kuuza eneo la nchi na kupata pesa nyingi za kuendeleza maeneo mengine, kwa sababu hakuna sababu ya kuishi maisha magumu utafikiri tumehamia hapa Duniani.
Kwa mfano, kuna ubaya gani mwekezaji anataka kuinunua mbuga ya Serengeti kwa trilion 500? Hiyo hela itajenga SGR, bandari, mashule, hospital nk. Mbuga za Wanyama zipo nyingi tu. Au Geita ya dhahabu ikiuzwa kwa trilion 400-500 kuna ubaya gani wakati madini yapo kila kona ya nchi?
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Katiba mpya inahitajika ama marekebisho ya katiba kwenye kipengele kinachohusu ardhi na mipaka ya Zanzibar kuondoa hii sintofahamu.Hapana mkuu,
Kwenye maisha kuna fantasy na reality. Yaliyoandikwa kwenye katiba ya JMT kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na reality ilivyo ni tofauti kabisa.
In reality Zanzibar ni nchi kamili, hayo mengine tunawaachia nyinyi na nadharia zenu. Ndio maana kwenye moja ya post zangu huko juu nikasema "ACTIONS SPEAK LOUDER THAN WORDS"
Sawa mkuu ila hii itakuwa ni mada nyengine.Serekali ya Zanzibar si uwakilishi wa wazanzibari, Kura za wananchi hazikuheshimiwa waliongia madarakani waliingia kwa mtutu wa bunduki.
Na ndio maana katika hili sikuweka uchama mbele.Ucwe na jazba mm c Cuf c CCM Wazanzibar tumecheleweshwa xana Kwa dizain izo hapo weka Uzanzibar wako mbele wacha kuhemkwa hizi NI rasilimali zetu sote regardless chama chak au itikadi yako
Mimi sina jazba mkuu. Nadhani suala tumelizungumzia vya kutosha kwamba kinachofanyika ni kwa maslahi mapana sana ya Zanzibar na watu wake.Punguza jazba, tuambie kwaupole tukuelewe vizuri.
Mkuu,Relief Mirzska ni kada mtiifu wa CCM, musipate tabu nae kabisa.
Nchi inauzwa kiholela yeye kifua mbele yupo anatetea.
Mkuu hiyo sio lease price, lease price itatofautina from one area to the other based on different factors.Samahani hii USD 2,500,000 ni Capital anayotakiwa awenayo investor ama ni lease price?
OkHujajibu kitu. Ulichofanya ni kuongeza suspicion kuwa kuna kitu kinafichwa. Hamna haja ya kumbeza mtu aliyekuuliza swali kwa sababu hupendi tu jinsi alivyoliuliza. Kwa majibu hayo aliyeuliza ataenda kuyapeleka kwa hao wananchi ambako hautakuwa na njia ya kumsahihisha. Obfuscation haisaidii.
Kujificha nyuma ya pazia kuwa serikali inafanya yote hayo kwa maslahi ya raia wake hakusaidii maana kuna mifano mingi tu ya wananchi kuumizwa kutokana na mikataba ambayo serikali yao imeingia kwa niaba yao. Mpe heshima yake kwa sababu ni kodi yake na za watu kama yeye ndio kwa kiasi kikubwa inaipa serikali yake uwezo wa kufanya hayo inayofanya. Na ni kodi yake ndio itakayotumika kurekebisha makosa yoyote yanayoweza kutokea hapo baadae.
Wewe kama unaweza kulipia chumba cha dola 2000 usimdharau yule anaedhani kuwa anakatazwa hata kuogelea katika maji yaliyozunguka kisiwa cha Bill Gates. Kama anatuhusiwa, mueleze hivyo kwa lugha ya staha ambayo wewe ungependa aitumie. Muonyeshe kwa mfano.
Amandla...