Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?


Taasisi ipi ndiyo inayoratibu haya. Maana ninataka kuwapa ushauri wa kitaalam bure kwa nchi yangu.
 
Ndio maana unapayuka kumbe NI miongoni WA wadaidika WA keki ya Taifa tuambie Wazanzibar WA Matemwe,Tumbatu charawe Kisiwapanza Kengeja wamefaifdikaje usitwambie ulivyofaidika ww na jamaa yako tu
Sheikh usitake kuniletea ubishi wako na hoja zako za ki CUF CUF hapa.

Huyo ninaekwambia anashika managerial position mnemba ni Mmatemwe, nenda Matemwe kigomani kule ukaone kituo cha afya kilichojengwa na &beyond, na wazanzibari wanafaidika. Nenda Matemwe ukaone miradi wa skuli ya kisasa kabisa unavyowanufaisha watoto wa ki Matemwe, unadhani ule sio kwa sababu ya sera bora za SMZ?? Jielewe hebu sio kila kitu kupinga pinga tu ebo!
 
Sisi Mwenyezi Mungu aliotujaalia kuwa na ardhi, hatuelewi maana ya kukosa ardhi. Tena tunaona ardhi ni cheap. Kuna nchi kadhaa duniani zinatafuta ardhi kwaudi na uvumba!
Kwani nani kakwambia Ardhi hii haitakuwa yetu?? Mkuu kwenye decision making tunatumia taarifa mbali mbali kufanya maamuzi flani.

Vizazi vyetu haviwezi kukosa ardhi ya kilimo wala ya makaazi. Nenda Cheju huko ukajionee, nenda kandwi huko ukajionee, nenda kiwengwa huko ukajionee. Serikali haiangalii leo tu kufanya maamuzi, inaangalia miaka 20 ijayo. Hivo visiwa vipo tangu karne na karne, tumefaidika navyo vipi sisi ????

Vitakuwepo for another 3000 years, tutafaidika navyo vipi?? Why not benefiting from today??
 
Mawazo ya kitumwa visiwa vikae tu visiingize pesa wakati vinaweza kukodishwa na maisha ya wazenji yakaboreshwa.
 
Mkuu Sijali hebu jaribu kupitia haya madini pengine utaelewa kidogo.

Watu wengi humu wanaendeshwa na mihemko, au wanaongea vitu kwa sababu hawana taarifa kamili juu ya mambo mbali mbali
 
Mkuu Offshore Seamen umemaliza vizuri, asiyeelewa hapa atakuwa mlemavu
 
Waachieni Wazanzibari wafanye maendeleo yao. Kwa miaka zaidi ya 56 tumewang'ania utadhani ni mkoa wa Morogoro. Hawapati mgao nzuri wa misaada toka nje kupitia Muungano, hawapati mikopo toka nchi za Kiislamu kama OIC.

Huu ndiyo muda mwafaka wakati Rais wa Muungano ni Mzenj na wa Zenj naye Mzenj. Wakikosa sasa kujipanga wamekwisha
 
Sawasawa..
 
Mkuu,

Hatuongelei kuuza, tunaongelea kukodisha visiwa ambavyo hatuvitumii. Kwani mkuu inakuuma Zanzibar kukodisha visiwa vyake?
Inauma kwa sababu mainland wamewekewa kauzibe hauwezi hata uziwa eneo la choo , mzanzibar anamiliki maeneo kama yote mainland huku Yuko busy kuuzia beberu visiwa ambavyo kama si Zanzibar kuikalia bara kimabavu vinatakiwa viwe vyetu sote. Huo si uroho wa kombamwiko baba ?
 
Wewe umechanganyikiwa. Kinachofanyika visiwa vinavyokodishwa kwanza havifiki ukubwa huo. Utaratibu wa kukodisha ni kuwa unasema unataka kutekeleza mradi gani. Masharti pia kufanyike SIA (Strategic impact assessment) ya eneo kulingana na Mradi na Mamalaka ya mazingira itoe vibali. Pia kuna timu ya wataalamu kutoka Sekta mbalimbali ambao wanachambua maombi hayo. Moja ya masharti ni kuwa wananchi waendelee kuvitumia visiwa hivyo kwa shughuli zao za kijamii na kiuchumi
 
Pole mkuu wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…